Mambo ya Wafungwa Wa Kike, hasa hasa Wafungwa Wajawazito na Watoto Wao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo ya Wafungwa Wa Kike, hasa hasa Wafungwa Wajawazito na Watoto Wao

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Gabriel3266, Aug 4, 2010.

  1. G

    Gabriel3266 New Member

    #1
    Aug 4, 2010
    Joined: Aug 2, 2010
    Messages: 4
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Hey, habari zenu wanaJF? Jina langu ni Gabriel, nipo Dar, na nafanya kazi kwa shirika la kienyeji, na tunatengeneza mradi wa kuwatetea wafungwa wa kike, hasa hasa wafungwa wajawazito na watoto wao, na kuwapatia mahitaji ya msingi. Nimeorodhesha maswali kadhaa kuhusu mambo haya, na ningependa sana kuwasiliana na ninyi kuhusu masuala haya. Asanteni sana. Nawatakia kila la heri.
    · Tovuti rasmi ya Wizara ya Mambo ya Ndani inaorodhesha magereza 122. Na ndani yake kuna wafungwa wa kiume 43000, na nusu ya idadi hii ni mahabusu, idadi hii inazidi uwezo wa kuchukua kama takriban asilimia 200.
    · Ijapokuwa mahabusu wanatakiwa kupata hukumu yao mahakamani sio zaidi ya siku 15 baada ya kukamatwa, wengi wanakaa magerezani kwa muda mrefu zaidi kwa ajili ya upungufu wa mashahidi, majaji, au upelelezi wa kiaskari unaoendelea, miongoni mwa sababu nyingine.
    · Lakini tovuti rasmi ya Wizara ya Mambo ya Ndani inasema kwamba kuna wafungwa wa kike 1361 tu, na kuna gereza moja la wanawake lilipo Kingolwira, mkoani Morogoro. Je, takwimu hizi ni sahihi?
    · Nilidhani wafungwa wa kike 1361 kulinganishwa na wa kiume 43000 haikuwa sawa, hii ni idadi ndogo zaidi, lakini niligundua kwamba kwa barani afrika kote, wafungwa wa kike ni asilimia 4-5 ya umma mzima wa wafungwa.
    · Kwa wafungwa wa kike nchini kote, wangapi ni mama wajawazito au wana watoto waliomo gerezani pia? Ila Kingolwira, wafungwa wa kike wanakaamagereza yapi?
    · Nilisoma kwenye Sheria ya Magereza ya 1967 kwamba mama na watoto wao wanatakiwa kupata huduma zote au huduma maalum, lakini, kwa mujibu wa uchunguzi wangu, haitokei, hawapewi mahitaji na chakula cha kutosha.
    · Mwaka jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Khamis Kagasheki, alisema serikali haina uwezo wa kujenga magereza maalum ya wanawake kwani hakuna msongamano wo wote wa wafungwa wa kike. Aliendelea kusema kwamba magereza mengi hayana wafungwa wa kike wowote au ni wachache sana tu.
    · Vilevile, Bwana Kagasheki alidai kwamba kuna wafungwa mama wajawazito 15 tu, je ni kweli?
    · Tarehe ya 26, Mwezi wa 4 Mwaka huu, 2010, Rais Kikwete aliwapa msamaha wafungwa wa kike na wafungwa wajawazito wangapi? Vilevile, wafungwa wa kike hawa walikaa magereza yapi?
     
Loading...