Mambo ya valentine europe

Glucky

Senior Member
Dec 16, 2009
123
40
Mgahawa wa Mildred's Temple Kitchen wa mjini Toronto nchini Kanada umeibuka na staili ya ajabu ya kuwavutia watu kwenye mgahawa huo kusherehekea siku ya wapendanao (februari 14).

Mgahawa huo unawaalika wateja kufanya mapenzi kwenye vyoo vya mgahawa huo.

Meneja wa mgahawa huo, Rory Gallagher, alisema kuwa katika kusherekea siku ya wapendanao, kuanzia februari 12 hadi februari 15 watu wataruhusiwa kufanya mapenzi kwenye vyoo vya mgahawa huo.

Gallagher aliendelea kusema kuwa ili kufanya mambo yote yaende sawa, mgahawa huo umeandaa wafanyakazi ambao watakuwa na jukumu la kuviweka safi vyoo hivyo wakati wote.

Akiongea na gazeti la The Toronto Star, mmoja wa wamiliki wa mgahawa huo, Donna Dooher, alisema "Watu wamekuwa wakifanya mapenzi kwa siri kwenye vyoo vyetu, tunataka siku ya wapendanao iwe ya kipekee".

Hata hivyo mmiliki huyo alisema kuwa wateja watatakiwa kuja na kondomu zao wenyewe.

Katika hali ya kushangaza zaidi, Ofisi ya masuala ya afya ya jamii ya Toronto imeuruhusu mgahawa huo kuendelea na mipango yake hiyo huku ikitoa taarifa kuwa mgahawa huo hauvunji sheria yoyote kwakuwa vitendo vya kujamiiana havitafanyika jikoni, vitafanyika kwenye vyoo ambavyo vitawekwa safi wakati wote.
 
Kumbe mji wa Toronto nchini Kanada ni Europe, this is news to me, asante mwanzisha thread.
 
DAh kweli hii ni hatari sana, tutaiga kila kitu, Valentine imeanza kuingia BONGo miaka ya 1994-95 nadhani na kuendelea, Redio One waliitangaza sana na kuwafanya wadanganyika waige haya mambo, kabla ya hapo hakukuwa na vitu kama hivi na maisha yaliendelea vizuri tu, siku hizi vibinti/vivulana na hata watu wazima maskini wanateseka sana hii siku, heartbreak kibao zinakuwepo siku hii, kwa kweli sioni umuhimu wa hii siku kwani unashindwa kumtunuku mpenzi wako siku hizi nyingine mpaka ifike hiyo siku? kama si kuhalalisha NGONO zisizo na mpango? siku hiyo ikifika saa mbili hupati chumba kwenye gesti zote zinakuwa zimejaa, UZINZI MTUPU!!!
 
safi sana, maana hata wasingetoa ruhusa bado watu wangefanya tu.
 
hii ni hatari sasa naona watu wamechanganyikiwa na maisha

Hiyo ndiyo dunia. Binadamu siku zote anatafuta kitu tofauti ili kimpatie uzoefu wa kukumbukia ingawa wakati mwingine huishia kuchefua. Ni busara tu inahitajika, vinginevyo hawa jamaa waweke na vitanda kabisa halafu walipishe VAT!!
 
Mgahawa wa Mildred's Temple Kitchen wa mjini Toronto nchini Kanada umeibuka na staili ya ajabu ya kuwavutia watu kwenye mgahawa huo kusherehekea siku ya wapendanao (februari 14).

Mgahawa huo unawaalika wateja kufanya mapenzi kwenye vyoo vya mgahawa huo.

Meneja wa mgahawa huo, Rory Gallagher, alisema kuwa katika kusherekea siku ya wapendanao, kuanzia februari 12 hadi februari 15 watu wataruhusiwa kufanya mapenzi kwenye vyoo vya mgahawa huo.

Gallagher aliendelea kusema kuwa ili kufanya mambo yote yaende sawa, mgahawa huo umeandaa wafanyakazi ambao watakuwa na jukumu la kuviweka safi vyoo hivyo wakati wote.

Akiongea na gazeti la The Toronto Star, mmoja wa wamiliki wa mgahawa huo, Donna Dooher, alisema "Watu wamekuwa wakifanya mapenzi kwa siri kwenye vyoo vyetu, tunataka siku ya wapendanao iwe ya kipekee".

Hata hivyo mmiliki huyo alisema kuwa wateja watatakiwa kuja na kondomu zao wenyewe.

Katika hali ya kushangaza zaidi, Ofisi ya masuala ya afya ya jamii ya Toronto imeuruhusu mgahawa huo kuendelea na mipango yake hiyo huku ikitoa taarifa kuwa mgahawa huo hauvunji sheria yoyote kwakuwa vitendo vya kujamiiana havitafanyika jikoni, vitafanyika kwenye vyoo ambavyo vitawekwa safi wakati wote.
Avatar yako mmmmhhh, inatutega....
 
Back
Top Bottom