mambo ya siku ya ukimwi duniani

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
Haya wengine wanaiita zana wengine ...
Nilimkumbuka jamaa yangu mmoja alikuwa kashauriwa na dakitari atumie uzazi wa majira, na njia mojawapo ni kutumia hii zana. Akasema vyema, ngoja niende dukani.
Duka la kwanza, akamkuta muuzaji ni jamaa yake anayemfahamu sana, na anamjua kuwa yeye ni ustaadh, sasa atamwambiaje ili ampe hiyo dhana. Akapiga stori na kuulizia hiki na kile. Baadaye akifikia hiyo zana.
'Na hizi zana, duu siku hizi sipo sampuli mbalimbali, hivi mtu akitaka kununua anakuulizaje, manake..mmh' akawa anazichungulia
'Ustaadhi bwana, hayo waachie hawo wanaoutumie, wewe siumeoa, hayakuhusu hayo..' jibu lile likamkatisha tamaa, akaondoka bila kuaga.
Akaona atafute duka la mbali kidogo, ambapo hawamjui. Alipofika akauliza vitu vingi, mwishowe akaona asipoteze muda.
'Na zana zipo humu?' akauliza
'Zana ni kitu gani mzee' Muuza duka akawa anashangaa
'Mhh, zile pale zinaitwaje?' akauliza
'Hizi condomu, umepata nyumba ndogo nini...' akasema muuza duka na pale akaingia mama mmoja wa heshima.
`Hapana, nilikuwa natanaia tu...basi kwaheri..'
Alihangaika hivi wiki nzima na hakupata nafasi ya kununua , ndipo wazo likamjia, akaenda maduka ya jumal, akaandaa karatasi ya vitu uvya kununua na mojawapo ni boksi la kondomu. Vingine vyote akatiki, kuwa keshapata, lakini ile sehemu ya zana akaicha wazi.
'Bwana mzee unajua siku hizi tumeambiwa kila duka uweke zana,mmmh, hiii hapa, sasa mnauzaje?'
'Bei yake ni shilingi...nikupe boski ngapi
'Nipe moja, siunajua tena sisi wazee...' akasema
'Nyie wazee, siumesema ni za dukani mzee au ndio...'
'Ni za dukani nasema sisi wazee ukiuza pale dukani unona aibu watu wakija kukulizia, bei yake...
Ndio akapata boksi moja...
Hii ni dhahirinimeinyofoa kwa michuzi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom