Mambo Ya Prof. Kohi Na Mkewe

Ibambasi

JF-Expert Member
Jul 25, 2007
9,277
4,682
Ndugu wanaJF,napenda kuchukua nafasi hii kuwaletea kitu kidogo kuhusu Prof. Kohi aliyekuwa Mkuu wa COSTECH.Sasa sijui hii habari inapaswa iwe kwenye vibweka vya wakubwa au hapa,admn. ataamua.

Anyway here we go:

Pale nyumbani kwake bwana Kohi Mbezi Beach Tangi Bovu pembeni ya barabara ya kwenda Goba ndipo anapoishi. Habari yenyewe ni kuwa alikuwa na mlinzi/gatekeeper kijana mmoja wa Kisukuma anafahamika kwa jina la Ngosha (jina lake halisi ni Mahona). Sasa kijana huyu amechishwa kazi na mkewe Kohi kwa sababu wanazozifahamu wao.

Ila cha kusikitisha ni kwamba baada ya kumfukuza kazi kijana huyo,mke wa Prof. Kohi akamnyang'anya ATM card yake ambayo ndiyo ilikuwa inatunza mshahara wa kijana huyo. Mpaka dakika hii kijana huyo hana pa kwenda kwa vile ATM card yake kanyang'anywa.

Kwa sasa kijana huyo anakaa kwa marafiki zake na hajajua afanye nini?

Jamani huu ni ubinadamu kweli? Mbona yeye Prof. kaondolewa kazini lakini hajanyimwa stahili zake? Ila inasemwa pia kuwa mke wa Prof. naye alikuwa tayari keshajenga kiburi sana, sijui ni kwa sababu ya cheo alichokuwa nacho mzee?
 
Aisee kama account alifungua kwa jina lake na anaimiliki kisheria kitendo cha huyo mama ni kosa na ni unyanyasaji wa hali ya juu. Cha msingi huyo kijana aonane na mwajiri wake ambaye ni Prof amweelze khali halisi other wise appitie njia nyingine za kisheria kama kwenda mahakamani. Japo mahakamani kuna gharama na unyanyasaji pia kwa kijana kama Ngosha haki haitatendeka sana kwa mfumo wa mahakama za kitanzania.

Alternatively ni kuishushia hiyo familia yao P kabisa. Na njia moja wapo ni kwenye kwenye vyombo vya habari, na kuwa mashirika ya haki za inadamu na kulalamika publicly na umma uelewe imekuwa je. Haki ya mtu haipotei hivi hivi hata kidogo. Aende zake Kwenye magazeti ya udaku na ze Komedy kwanza hawana habari za kutoa kwa sasa watamshukuru sana.
 
Aende Bank akawaeleze kuwa ATM card yake imenyang'anywa, ktu ambacho bank watadeem kama imeibiwa na watablock matumizi ya ATM kwenye account yake na anaruhusiwa kuapply ATM card nyingine. Maadam yeye ndiye mwenye account, hakuna mtu anayeweza kuwa na madaraka na maamuzi ya account yake, provided bank wamekuwa informed...nampa pole sana
 
He can apply another ATM card after having a police ticket. However, this is not different from that of Lucy Kibaki.
 
Anaweza kufanya kiutawala kwa kuiomba kadi yake toka kwa huyo mama au mzee kohi mwenyewe. Ila kisheri hilo ni kosa la jinai tena linaangukia katika makosa ya unyang'anyi wa kutumia nguvu. Huyo kijana anaweza kwenda polisi kuripoti hilo tukio halafu polisi watamuelekeza namna ya kulifikisha suala hilo mahakamani, au anaweza kwenda kwenye vituo vya msaada wa sheria kama vile kituo cha Msaada wa sheria Magomeni kilicho chini ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu.
 
Mambo mawili yanahitajika hapa. Kadi ya ATM na fedha. Kijana anahitaji card yake ili aweze kuchukua fedha yake atumie. Lakini pia kijana huyo bila shaka anahitaji fedha yake sasa. Suluhisho la kupata fedha yake sasa ndilo lenye kazi ngumu, kwenda kushitaki na kuwawajibisha hao waajiri wake.

Kuhusu kupata hiyo ATM card yake, anachopaswa kufanya ni kuripoti hilo tukio polisi ambako watampa nyaraka zinazoonesha kwamba kadi hiyo imeporwa. Atazipeleka hizo nyaraka kwenye benki yake ambako ataelekezwa utaratibu wa kuomba kadi mpya, ambayo kwa uzoefu wangu itachukua si chini ya wiki 3. Je katika kipindi cha hizo wiki 3 atakazokuwa anasubiri atakuwa anaishije?

Hapo ndipo watu wenye mapenzi mema wanapopaswa kuingilia kati, kwa kumchangia na kulipeleka hilo suala kwa watetezi wa haki za binadamu.

Namshauri awe mpambanaji, apeleke malalamiko kila mahali anapoweza, polisi, aende hadi kule kwa Mama Bisimba (watetezi wa haki za binadamu, hapo watamtetea bure kabisa, ofisi zao ziko Buguruni ninavyokumbuka kama hawajahama), aandike barua tume ya haki za binadamu na utawala bora (wako pale karibu na ikulu, huwa wanapokea barua hata iliyoandikwa kwa mkono na wanafuatilia), ashitaki hata kwa mjumbe wa nyumba kumi, kwenye vyombo vya habari, kila mahali ilimradi amfanyie vurugu za kutosha. Atarudisha hiyo kadi na hela atalipa na fidia juu. Nina uhakika.
 
Akishapata Police loss report tayari bank watamruhusu kuchukua pesa dirishani, na akishajaza form za kuomba ATM, taratibu za benki zitachukua mkondo wake sasa km kawida, kile watakachompa bank wakt anasubiria ATM yake ndiyo itakuwa kitambulisho chake.

Sema kunakuwa na usumbufu just in case anataka kuchukua pesa kutoka kwenye tawi ambalo siyo lake
 
Ndugu wanaJF,napenda kuchukua nafasi hii kuwaletea kitu kidogo kuhusu Prof. Kohi aliyekuwa Mkuu wa COSTECH.Sasa sijui hii habari inapaswa iwe kwenye vibweka vya wakubwa au hapa,admn. ataamua.

Anyway here we go:

Pale nyumbani kwake bwana Kohi Mbezi Beach Tangi Bovu pembeni ya barabara ya kwenda Goba ndipo anapoishi. Habari yenyewe ni kuwa alikuwa na mlinzi/gatekeeper kijana mmoja wa Kisukuma anafahamika kwa jina la Ngosha (jina lake halisi ni Mahona). Sasa kijana huyu amechishwa kazi na mkewe Kohi kwa sababu wanazozifahamu wao.

Ila cha kusikitisha ni kwamba baada ya kumfukuza kazi kijana huyo,mke wa Prof. Kohi akamnyang'anya ATM card yake ambayo ndiyo ilikuwa inatunza mshahara wa kijana huyo. Mpaka dakika hii kijana huyo hana pa kwenda kwa vile ATM card yake kanyang'anywa.

Kwa sasa kijana huyo anakaa kwa marafiki zake na hajajua afanye nini?

Jamani huu ni ubinadamu kweli? Mbona yeye Prof. kaondolewa kazini lakini hajanyimwa stahili zake? Ila inasemwa pia kuwa mke wa Prof. naye alikuwa tayari keshajenga kiburi sana, sijui ni kwa sababu ya cheo alichokuwa nacho mzee?
Hiyo kesi iliishaje?
 
Back
Top Bottom