Mambo ya muhimu unayopaswa kumpa mtoto

Sema Tanzania

JF-Expert Member
May 18, 2016
251
465
Ingawa yapo mambo mengi unayopaswa kumpa mtoto wakati ukimlea, leo tunazungumzia mambo unayoweza kuyaita tunu za maadili. Tunu hizi zitahakikisha anakuwa mtoto muadilifu na mtu mzima mwenye kuishi na watu vizuri.

Upendo.

Mzazi au mlezi unapaswa kumuonesha mtoto wako kuwa unampenda kwa maneno na kwa vitendo. Tunaposema kwa maneno tuna maana ya kuwa unamwambia “nakupenda sana mwanangu” kila mara na kila wakati unapata fursa ya kufanya hivyo. Vilevile tunaposema kwa vitendo maana yake ni kuwa karibu naye pale anapokuwa na hofu, uoga au huzuni kwa kumkumbatia na kumweleza jinsi gani hali kama hiyo ni sawa kumtokea binadamu, n.k. Upendo kamwe hauhesabu mabaya na upendo wa mzazi kwa mtoto ni bidhaa adimu Dunia ya sasa.

Mfundishe kuabudu

Jukumu la kulea linakuja na uwakilishi wa matakwa ya ibada bila kujali dini zetu. Mzazi unao wajibu wa kumuelekeza mwanao namna ya kufanya ibada, kumtegemea Mungu na ukimueleza uwepo wa Mungu kadiri umri unavyoongezeka.

Kumsikiliza

Tenga muda wa kufurahi na mtoto wako, kuishi maisha yake na kumsikiliza. Malezi hujumuisha uwepo wako kwa mtoto – hii ni fursa adimu kwako kupanda mbegu za matarajio yako kwa mwanao. Hivi unajua anacheza staili zipi pindi muziki unapowashwa. Ukiambiwa utabisha, mwanangu? Minenguo? Bongo fleva? Hasha! Fursa pekee ya kujua anacheza staili zipi ama vinginevyo ni kucheza naye. Mkanye pale anapoiga mitindo isiyo-sawa na umri wala maadili unayoyatarajia. Kufanya hivyo kutamsaidia sana mtoto kujenga ukaribu na mazingira rafiki kati yenu.

Ukarimu.

Mtoto huanza kuwa na marafiki mapema hata kabla ya kuanza shule na anapofikia umri wa kuanza shule idadi ya marafiki huongezeka na itafika wakati atakuja nao nyumbani kusoma au kucheza. Mzazi au mlezi unapaswa kumrithisha ukarimu kwa marafiki zake. Anza kwa kuwakarimu rafiki zake, bila kujali umri wao na atajifunza toka kwako. Michezo ya watoto hupendeza sana kama wakicheza kwa kushirikiana. Msaidie kujua na kuthamini mchango wa wenzake katika michezo na maisha yake kwa ujumla.

Msamaha.

Funzo la msamaha humwingia mtoto kwa vitendo zaidi ya maneno tu. Unapaswa kumsamehe mwanao pale anapokosea ili aonje ladha halisi ya msamaha. Hii itamsaidia kujifunza namna ya kuishi na watu ambao watakuwa wanamkosea. Mpe pia fursa za kukusamehe wewe unapoteleza katika maamuzi. Kufanya hivyo mtoto atakuwa huru kukueleza pale alipokosea kwa kusema ukweli pindi tu utakapomuuliza.

Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook, Instagram & Jamii Forums: Sema Tanzania; Twitter: @SemaTanzania na www.sematanzania.org
 
Hapo kwenye Ibada ndiyo huwa mnawalisha sumu watoto. Unamfundishaje mtoto anapofikia kwenye wakati mgumu apige goti na kulia, badala ya kusimama na kugangamala?!!
 
Licha ya yote tusisahau kuchagua mazingira na jamii rafiki ya kulelea watoto
Amini nakwambia mazingira na jamii inayotuzunguka yana nguvu kubwa kuliko wazazi katika familia
 
Ingawa yapo mambo mengi unayopaswa kumpa mtoto wakati ukimlea, leo tunazungumzia mambo unayoweza kuyaita tunu za maadili. Tunu hizi zitahakikisha anakuwa mtoto muadilifu na mtu mzima mwenye kuishi na watu vizuri.

Upendo.

Mzazi au mlezi unapaswa kumuonesha mtoto wako kuwa unampenda kwa maneno na kwa vitendo. Tunaposema kwa maneno tuna maana ya kuwa unamwambia “nakupenda sana mwanangu” kila mara na kila wakati unapata fursa ya kufanya hivyo. Vilevile tunaposema kwa vitendo maana yake ni kuwa karibu naye pale anapokuwa na hofu, uoga au huzuni kwa kumkumbatia na kumweleza jinsi gani hali kama hiyo ni sawa kumtokea binadamu, n.k. Upendo kamwe hauhesabu mabaya na upendo wa mzazi kwa mtoto ni bidhaa adimu Dunia ya sasa.

Mfundishe kuabudu

Jukumu la kulea linakuja na uwakilishi wa matakwa ya ibada bila kujali dini zetu. Mzazi unao wajibu wa kumuelekeza mwanao namna ya kufanya ibada, kumtegemea Mungu na ukimueleza uwepo wa Mungu kadiri umri unavyoongezeka.

Kumsikiliza

Tenga muda wa kufurahi na mtoto wako, kuishi maisha yake na kumsikiliza. Malezi hujumuisha uwepo wako kwa mtoto – hii ni fursa adimu kwako kupanda mbegu za matarajio yako kwa mwanao. Hivi unajua anacheza staili zipi pindi muziki unapowashwa. Ukiambiwa utabisha, mwanangu? Minenguo? Bongo fleva? Hasha! Fursa pekee ya kujua anacheza staili zipi ama vinginevyo ni kucheza naye. Mkanye pale anapoiga mitindo isiyo-sawa na umri wala maadili unayoyatarajia. Kufanya hivyo kutamsaidia sana mtoto kujenga ukaribu na mazingira rafiki kati yenu.

Ukarimu.

Mtoto huanza kuwa na marafiki mapema hata kabla ya kuanza shule na anapofikia umri wa kuanza shule idadi ya marafiki huongezeka na itafika wakati atakuja nao nyumbani kusoma au kucheza. Mzazi au mlezi unapaswa kumrithisha ukarimu kwa marafiki zake. Anza kwa kuwakarimu rafiki zake, bila kujali umri wao na atajifunza toka kwako. Michezo ya watoto hupendeza sana kama wakicheza kwa kushirikiana. Msaidie kujua na kuthamini mchango wa wenzake katika michezo na maisha yake kwa ujumla.

Msamaha.

Funzo la msamaha humwingia mtoto kwa vitendo zaidi ya maneno tu. Unapaswa kumsamehe mwanao pale anapokosea ili aonje ladha halisi ya msamaha. Hii itamsaidia kujifunza namna ya kuishi na watu ambao watakuwa wanamkosea. Mpe pia fursa za kukusamehe wewe unapoteleza katika maamuzi. Kufanya hivyo mtoto atakuwa huru kukueleza pale alipokosea kwa kusema ukweli pindi tu utakapomuuliza.

Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook, Instagram & Jamii Forums: Sema Tanzania; Twitter: @SemaTanzania na www.sematanzania.org
Ibaada? Yaani nimfundishe mwanangu kupiga magoti kulialia badala ya kupambana na ukweli kurafuta suluhu? Hahhahahhaaa, bangi za ukoloni zilitumaliza akilo
 
Back
Top Bottom