Mambo ya msingi kuyafanya kabla ya kuoa/kuolewa

Kitokororo255

Member
Sep 22, 2016
29
12

Ndoa nyingi zinaingia kwenye migogoro kwa sababu ya mambo ya kukurupuka na kufanya haraka bila wahusika kufahamiana vizuri, hebu tuzingatie yafuatayo ili tusiseme 'NINGEJUA NISINGEOA/NISINGEOLEWA'

1. Chanzo cha uhusiano wenu kiwe ni upendo wa dhati
2. Chunguza kwa mwenzio juu ya tabia:nidhamu, adabu, hasira, ulevi na umalaya
3. Mpeane muda wa kutosha kufahamiana
4. Mtembee pamoja maeneo tofautitofauti kama michezoni, bar na out mbalimbali ili muone interest za kila mmoja
5. Muwe wa imani moja. ila kama mmeshibana sana na mwaweza kuvumiliana hata wa imani tofauti ni sawa.
6. Wajue ndugu wa mwenzio ili kupata habari zao zitakazokufahamisha mwenzao pia yukoje
7. Pimeni afya zenu bila aibu. kuna maradhi mengi kama HIV/AIDS na mengine.
8. Kama ni Mkristo au Muislam funga ndoa Kanisani au Msikitini na siyo Bomani.
9.Kwa Wakristo ndoa haina talaka. huu ni mpango wa Mungu. kuachana na kuoa mwingine ni dhambi.

N.B: kama mwenzio ana tabia usiyoipenda, usifunge ndoa naye ukitegemea atabadilika.abadilike wakati mkiwa wachumba na siyo kwenye ndoa, labda kama umeshamkubali kama alivyo
 
Usisahau kuziba masikio na kufunga madirisha. Ndoa nyingine nyingi zinaharibika sababu ya kusikiliza watu wa pembeni, ikiwa ni pamoja na marafiki na hata ndugu
 
Umenena vyema...
Ila kingine ni kusikiliza ya pembeni... Wapambe ni nuksi sana... Utakuta yao yanawashinda wanashadaia ya wenzao...

Mkiweza to over come that... Mtaishi kwa raha sana...


Cc: mahondaw
 
Binafsi nadhani mifumo/njia sahihi ya Urafiki---> Uchumba---> Ndoa hata haifuatwi. Hivyo, matatizo katika ndoa hayataisha, tume-import western culture za kufikia ndoa, usitegemee ndoa kuwa za furaha na amani.
 
Back
Top Bottom