SoC01 Mambo ya lazima kwa wananchi ili kuvuka uchumi wa kati

Stories of Change - 2021 Competition

jeff mahugi

Member
Jul 15, 2021
7
16
Habari zenu wanajamvi ni matumaini yangu wote ni wazima. moja kwa moja nianze kuelezea namna wananchi watakavyo fanikiwa kulivusha Tiafa letu kutoka katika uchumi huu wa kati. yafuatayo ni maelekezo yenye kusisimua namna ya kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja hadi kufikia ngazi ya kitaifa.

MFUMO WA KUINUANA: huu ni mfumo ambao unahusisha kila mwananchi athamini kila kinachofanywa na mwananchi mwenzake ikiwa ni kwa kumuungisha mwananchi mwenzie au kwa kumsaidia kumtafutia wateja katika biashara yake, kumpatia mbinu bora za kuinua biashara. jambo la muhimu na lakuzingatia ni kwamba kila jambo unalofanya na wewe utafanyiwa. ikiwa watu watano wakajumuika kumuungisha muuza karanga basi na wao wajue kuna watu watajumuika kuwasapoti katika biashara zao.kama taifa mfumo huu tumekua tukiutumia hasa hasa kwa watu maarufu ndio maana utaona watu Mashuhuri/maarufu wanazidi fanikiwa kwa kuwa sisi wananchi tumeungana kusapoti kila kinachofanywa na hao na tumesahau kua katika kila mtaa kuna watu wanafanya biashara na wanalalamika biashara zao hazina wateja.

UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI DHAIFU msemo huu unatumika sana katika uhamasishaji watu lakini kiuhalisia sisi hatuutumii ipasavyo katika maisha yetu ya kila siku bali tumekua tukiutumia kwa kinyume yaani tumekua tukiutumia katika sherehe, ugomvi n.k
hatuutumii katika kuimarishana kimaisha. kuna baadhi ya jamii huutumia huu mfumo kwa watu wao yaani kama kaka anapesa atamuangalia mdogo wake aliyedhaifu atamfundisha biashara na kumfungulia biashara. nakuendelea kwa ndugu wa ukoo huo hatimaye ukoo unakuwa na matajiri wengi.

WASANII WANAVYO FANYA: msanii anauna kombinesheni na ma dj na vyombo vya habari vyombo vya habari vinamtanagaza msanii mpaka msanii anafanikiwa. na sisi wananchi tunaungana na vyombo vya habari TUNAMSAPOTI msanii mwisho wa siku msanii anapata mafanikio makubwa wakati wewe bado. simaanishi tusiwasapoti hapana namaanisha huu utaratibu usiishie kwa wasanii na watu mashuhuri bali huu mfumo uje katika ngazi ya mtaa kwa mtaa tukifanya hivi hamna kitu kitakacho tufanya kama taifa kuvuka hapa tulipo. kwa sababu mzunguko wa pesa utakua upo kwa kiasi kikubwa mno na Taifa litasonga mbele. niwatakie utekelezaji mwema wa majukumu ya ujenzi wa taifa wasalaam.
 
Back
Top Bottom