Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,397
Wakati ukivinjari kwenye mtandao wa inteneti unapotembelea tovuti mbalimbali au #MitandaoYaijamii unapaswa kuwa mwangalifu na kutunza usalama wako dhidi ya watu wenye nia ovu: Kumbuka mambo yafuatayo ili kujihakikishia usalama wako
Usifungue kiunganishi au barua pepe kutoka kwa mtu usiyemfahamu: Wadukuzi hutumia mbinu ya kutuma links au viunganishi wanavyoviambatanisha na jumbe za kuvutia. Endapo utafungua kiunganishi hicho basi unampa uwezo mdukuzi wa kuingia mawasiliano yako
Tumia nywila au password iliyoimara na bora zaidi: Jitahidi kuifanya nywila yako kuwa siri na kuitunza kwa njia sahihi, epuka kutoa nywila yako kwa mtu yeyote. Endapo nywila yako itaingia katika mikono ya wahalifu wa mtandaoni basi taarifa na mawasiliano yako yatakuwa shakani
Tumia kivinjari(Browser) inayojali usalama wa watumiaji wake: Wataalamu wengi wa #UsalamaWaKidigitali hushauri watu kutumia vivinjari vifuatavyo, Tor Browser, Firefox, Brave, Yandex Browser, Epic, Freenet na I2P
Usikubali urafiki kutoka kwa mtu ambaye unamashaka na akaunti yake: Inashauri wa kuichunguza akaunti iliyokuomba urafiki kabla ya kukubali na kuanza kuwasiliana nayo. Ipo mifano ya watu kutumiwa meseji na kuombwa kutoa barua pepe zao kutoka kwa watu ambao si rafiki zao kwenye mtandao
Wadau naomba mchangie mengine zaidi ili kujenga uelewa mpana...