JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Barakoa hufanya kazi ya kunasa matone yaliyo na virusi tunayotoa tunapoongea, kukohoa au kupiga chafya. Husaidia katika kujilinda wewe na wanaokuzunguka dhidi ya virusi
Ikiwa unaona barakoa inakukosesha amani usiache kuvaa bali badilisha aina tafuta nyingine mpaka utakapopata inayokufaa
Barakoa zinaweza kuleta unyevunyevu lakini katika hali hiyo, vaa ya kitambaa cha pamba ambayo itarahisisha kupumua kuliko polyester.
Ni kweli zinaweza kukuumiza masikio. Katika hali hiyo pata barakoa yenye kamba inayozunguka masikio iliyofunikwa kwa kitambaa laini ambacho hakitasumbua ngozi yako
Barakoa inaweza kuweka ukungu kwenye miwani kama wewe ni mvaaji wa miwani. Katika hali hiyo, vaa miwani yako ya macho juu ya barakoa ili kushikilia barakoa vizuri na miwani kutoingia ukungu