Mambo ya kuzingatia unaponunua tairi za gari

Nawasoma tu ahsanteni sana wataalamu. Kuna wengine hata leseni tuliletewa nyumbani.
Very educative. JF idumu dawamu!
 
Ni thread nzuri. Ni vizuri kucheki hizo spec zilizowekwa hapo juu ikiwa pamoja na maximum load capacity ya kila tairi, na maximum speed. pia date manufacture. Muchunguze kuhusu hilo. Ni muhimu kwa garu lako.
 
Kwa kweli tumefaidika sana na maelezo haya msione wengine tumekaa kimya... Tunajifunza!! Wengine wetu tumegundua makosa mengi ambayo tumekuwa tunafanya kwenye magari yetu!

Bila shaka kuna watu hapa wamekaa kimya lakini sasa wanakwenda kufanya tyre rotation kesho!!
Imebidi niseme tu, haki ya nani wametuelimisha pakubwa, mimi nilikua nafika tu nawaambia wajaza upepo nijazieni upepo hata sijui kupima wala cha nini, tire rotation ndio nilikua siijui kabisaaaa, lakini sasa nitakua napima upepo vizuri, nafanya tire rotaion na mengine mengi sana nilojifunza humu. Mungu awabariki wote waliotuelimisha!
 
mkuu unaendesha gari gani, nataka kujua ili nikujuze , D, 1, 2,3 +1/_2 kama zipo
Hapo msaada tutani mi nina Honda ina D1 mpka D4 kisha N, R, na P vip hizi zinatumika wapi, mi daima natumia D4 muda wote
 
Mkuu, tairi zinaishi miaka 4 toka siku zimetoka kuivishwa kiwandani, so wanachoandika kwenye tairi Ni siku ilipotengenezwa, na wanaandika wiki ya ngapi na mwaka!

mfano (2414)- Hii maana yake ilitengenezwa wiki ya 24 mwaka 2014.

Au (1017) - Hii maana yake ilitengenezwa wiki ya 10 mwaka 2017,

So hapo sasa ukishajua imetengenezwa lini unahesabu miaka mi4 mbele ndo unakua mwisho WA maisha ya tairi husika.
Shida ya hii kitu ni kwamba ukienda kununua tairi unakuta iko wrapped kwenye zile nylon zake kiasi kwamba huwezi kuona ndani na mwenye duka anakwambia ukiivua ili uione lazima uinunue sasa hapo ndo mushkili
 
Shida ya hii kitu ni kwamba ukienda kununua tairi unakuta iko wrapped kwenye zile nylon zake kiasi kwamba huwezi kuona ndani na mwenye duka anakwambia ukiivua ili uione lazima uinunue sasa hapo ndo mushkili
Na wewe si umpe condition Mkuu, mwambie nalipia na naifungua hapahapa ila kama haijatengenezwa mwaka huu unanirudishia pesa yangu... Kwani duka ni moja?
 
Ni muhimu kuzingatia vipimo unaponunua tairi za gari yako for a safe and comfortable drive.

Tairi zikitofautiana even a single dimension ni tatizo.

Tairi mbili za mbele na tairi mbili za nyuma au tairi zote lazima zilingane vipimo.

Namna ya kuangalia vipimo vya tairi :

Mfano tairi imeandikwa 205/70R14 au P 205/70R14 maana yake;

P = Passenger ie gari binafsi au ya abiria
205 = Upana wa tairi ni 205mm
70 = Urefu wa tairi ( kutoka ardhini hadi inapoanza rim) ni 70% ya Upana.
R = Muundo wa tairi ni Radial
14 = Diameter ya rim ni 14 inch.

Vipimo vinakuwa kwa mfumo kama ilivyo katika mfano huo hapo juu na vinaandikwa pembeni kwenye tairi.

Angalia mfano wa picha hapo chini.
Tire-sizing.gif

Pia waweza tembelea

Mkuu nimekuoa kwa nguvu ya tano maana hii kitu kwangu ilikuwa ni kitendawilo sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ovedrive ni gia kubwa ya mwisho kwenye automatic transmission. Mfano: Kwa kawaida automatic transmission ina gia tatu pamoja na gia ya overdrive ambayo ni gia namba nne. Overdrive gia inawezesha engine kuzunguka mara chache kwa kila dakika ( less Revolution Per Minutes - RPM) lakini wakati huohuo kuipa gari speed kubwa na hivyo kupunguza matumizi ya mafuta. Unapoweka Overdrive On, maana yake unaruhusu Gearbox ibadili gia hadi gia hadi kufikia gia namba nne pale gari inapofikia certain level of speed (ambayo imesetiwa na manufacturer - commonly inakuwa around 40 - 50 Km / Hr). Overdrive inapokuwa Off maana yake uruhusu Gearbox ibadili gia hadi kufikia gia namba tatu tu hata kama speed yako inafaa Gearbox i-shift to 4th gear.

Inashauriwa katika uendeshaji wa kawaida mfano wa mjini Dar es Salaam, Overdrive inatakiwa kuwa On. Inatakiwa kuwa Off pale unapoendesha maeneo yenye milima au ikiwa unavuta gari lingine. Aidha, inashauriwa Overdrive kuwa Off pale unaposhuka mlima mkali mfano mlima Kitonga. Hii inasaidia kutumia engine braking na hivyo kusaidia brake from overheating.

Kwa hiyo, Overdrive ina involve issue ya efficiency kwenye matumizi ya mafuta na si kwamba inafanya gari kukimbia. Watu wengi wanadhani unapoweka overdirve maana yake unafanya gari likimbie sana. Hi ni No No tena No. Overdrive is just choosing the shift pattern.

CC: mandingo6262
Kaka hapa mbona kama mi ninamtizamo tofauti na wako.!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninatunia gx110 ilikua na rim size17 ila nataka kuweka rim size 18 je hii italeta tatizo manaa lengo ni kuifanya gari kuwa juu kidgo
 
Ukute mchina kakuandikia traction A,temperature A cjui nn A...sasa ingia hapo road ndo utajua kwann wale jamaa ni wafupi.
 
Back
Top Bottom