Mambo Ya Kuzingatia Unapokuwa Kazini Ili Usije Ukaishi Maisha Ya Majuto

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
421
1,048
0x0.jpg

Wengi tunapokuwa kazini yapo maisha ambayo yanasababisha majuto kwa baadae. Hali hiyo inawatokea wengi sana hasa vijana wanaopata kazi mapema, mwisho wake wanaishia katika majuto.

Unachopaswa kujua au kuelewa, upo msingi wa maisha unatakiwa kuishi nao unapokuwa kazini ili baadae usije ukaishi maisha ya majuto na kujilaumu sana hasa pale unapofikia uzeeni kwako.

Katika makala haya itafafanua mambo ya kuzingatia unapokuwa kazini ili maisha yako ya baadaye yawe ya uhakika na usije ukaishi maisha ya majuto. Sasa twende pamoja ili tuweze kujifunza mambo hayo:

1. Tumia pesa zako kwa busara
Kwa namna yoyote ile unapokuwa kazini na unapata pesa zako wakati upo kazini, jitahidi sana usiishi maisha ya kujisahau. Watu wengi wanapopata pesa wanakuwa wanajisahau na kujua mshahara kwao ndio kila kitu.

Kwa mfano, utakuta pesa unazipata kweli lakini matumizi yako yanakuwa hovyo sana, kiasi kwamba unafika mahali huelewi hata hizo pesa zako unazitumiaje. Kuishi maisha haya ni kutafuta janga kubwa la kushindwa kwa baadaye.

Ili kuepuka kuishi maisha ya majuto baadaye, ishi kwa mipango, pesa zako zipangilie vizuri na ishi kwa kusudi maalumu.

2. Kamilisha mambo yako ya msingi mapema
Kama unajielewa wewe upo kazini na umeamua kufanya kazi kweli, hebu kamilisha mambo yako mapema. Yapo mambo ya msingi unayotakiwa kuyakamilisha mapema kama vile kusomesha watoto na kujenga nyumba.

Ni kosa kubwa sana, kuendelea kufanya kazi kwa muda mrefu pasipo kujiandaa kujenga nyumba yako na kusubiri hadi kustaafu kwako. Jenga nyumba mapema, maliza kusomesha watoto wako mapema na usiache jukumu hilo kwa watoto wengine wakajisomesha wao wenyewe.

Kitu kingine cha muhimu ni kuhakikisha unatengeneza kipato nje ya ajira yako, mfano tengeneza kitu cha ziada ambacho kinaweza kuingiza kipato nje ya mshahara, inawezekana ukafanya biashara au ukaweka uwekezaji.

Unapokamilisha majukumu yako mapema inakupa uhuru wa kuishi maisha bora pale unapokuwa umestaafu.

Kwa kifupi, hayo ndiyo mambo unayopaswa kuyazingatia hasa pale unapokuwa kazini na wakati huo unajiandaa kutengeneza maisha bora uyatakayo.

Nakutakia wakati mwema na uwe na siku njema, fanyia kazi haya na kila kheri katika kufikia mafanikio yako.
 
Kuna wengine wametokea maisha ya chin anapata kazi yeye ndo aanze kuwajengea nyumba wazazi wake, kuwalipia ada wadogo zake, kuimarisha uchumi wa nyumban alipotokea alaf sasa ndo aje kweny kujiendeleza kiuchumi yeye hapo takriban ishapita miaka 10 unafkir mtu kama huyo ana majukum mangap kwa mshahara wa mwsho wa mwez?
 
Wengi tunapokuwa kazini yapo maisha ambayo yanasababisha majuto kwa baadae. Hali hiyo inawatokea wengi sana hasa vijana wanaopata kazi mapema, mwisho wake wanaishia katika majuto.

Unachopaswa kujua au kuelewa, upo msingi wa maisha unatakiwa kuishi nao unapokuwa kazini ili baadae usije ukaishi maisha ya majuto na kujilaumu sana hasa pale unapofikia uzeeni kwako.

Katika makala haya itafafanua mambo ya kuzingatia unapokuwa kazini ili maisha yako ya baadaye yawe ya uhakika na usije ukaishi maisha ya majuto. Sasa twende pamoja ili tuweze kujifunza mambo hayo:

1. Tumia pesa zako kwa busara
Kwa namna yoyote ile unapokuwa kazini na unapata pesa zako wakati upo kazini, jitahidi sana usiishi maisha ya kujisahau. Watu wengi wanapopata pesa wanakuwa wanajisahau na kujua mshahara kwao ndio kila kitu.

Kwa mfano, utakuta pesa unazipata kweli lakini matumizi yako yanakuwa hovyo sana, kiasi kwamba unafika mahali huelewi hata hizo pesa zako unazitumiaje. Kuishi maisha haya ni kutafuta janga kubwa la kushindwa kwa baadaye.

Ili kuepuka kuishi maisha ya majuto baadaye, ishi kwa mipango, pesa zako zipangilie vizuri na ishi kwa kusudi maalumu.

2. Kamilisha mambo yako ya msingi mapema
Kama unajielewa wewe upo kazini na umeamua kufanya kazi kweli, hebu kamilisha mambo yako mapema. Yapo mambo ya msingi unayotakiwa kuyakamilisha mapema kama vile kusomesha watoto na kujenga nyumba.

Ni kosa kubwa sana, kuendelea kufanya kazi kwa muda mrefu pasipo kujiandaa kujenga nyumba yako na kusubiri hadi kustaafu kwako. Jenga nyumba mapema, maliza kusomesha watoto wako mapema na usiache jukumu hilo kwa watoto wengine wakajisomesha wao wenyewe.

Unapokamilisha majukumu yako mapema inakupa uhuru wa kuishi maisha bora pale unapokuwa umestaafu.

Kwa kifupi, hayo ndiyo mambo unayopaswa kuyazingatia hasa pale unapokuwa kazini na wakati huo unajiandaa kutengeneza maisha bora uyatakayo.

Nakutakia wakati mwema na uwe na siku njema, fanyia kazi haya na kila kheri katika kufikia mafanikio yako.
watu wa Daslam hawakuelewi hapa.....dezo wamuachie nani !.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Kuna wengine wametokea maisha ya chin anapata kazi yeye ndo aanze kuwajengea nyumba wazazi wake, kuwalipia ada wadogo zake, kuimarisha uchumi wa nyumban alipotokea alaf sasa ndo aje kweny kujiendeleza kiuchumi yeye hapo takriban ishapita miaka 10 unafkir mtu kama huyo ana majukum mangap kwa mshahara wa mwsho wa mwez?
Kiongozi akikujibu naomba unitagi
 
Mwenye kazi zao, huo hapo ujumbe kazi ni kwenu, sisi ambao, hatuna ajira tutabaki kutoa macho tu.
 
Back
Top Bottom