Mambo ya kuzingatia ukiwa katika nchi za bara la Asia, Ulaya na Marekani

Boss Man

JF-Expert Member
Feb 10, 2022
458
991
Ndugu Watanganyika Mungu ni Mwema, sifa kwake kwa kutujalia Uhai

Ikiwa una Mpango wa kwenda nchi yeyote Ile Duniani hasa Nje ya bara la Afrika jitahidi kuijua nchi hiyo japo kwa machache mambo ya kuzingatia ukiwa huko pamoja na tamaduni zao, kufanya hivyo itakusaidia sana kuishi kwa amani na kuepuka matatizo ambayo siyo ya lazima.

Naenda kuelezea mambo ya kuzingatia na ambayo hutakiwi kufanya pindi unapokua MAREKANI. nitakuelezea baadhi ya nchi nyingine pia kwa uchache

MAREKANI
Ndugu Mtanzania ukiwa marekani peana mikono (handshake ) kama salamu ya kawaida, japokuwa hii kwangu sio lazima sana kwasababu tu ya ngozi yangu nyeusi, nikiwa Marekani Mimi Binafsi kwenye hili swala la handshake mm Nina principal zangu huwa siwi wa kwanza kutoa mkono nasubiri mwenzangu aanze lakini pia hii nai apply sana hapa Bongo, maana mswahili hakawii kusema nataka kumuibia nyota

Ukisalimiwa "How are you" take it as if they are saying “You good?” na ujibu "Good" au "Good thank" jibu hivyo hata kama unahisi kufa sekunde zijazo, Marekani salamu haimaanishi kumjulia mtu hali, ni changamsha genge tu. Sasa wewe salimiwa halafu jichanganye kwa kutoa maelezo marefu.

Pia usisahau kuonesha katabasamu kwa mbali unaposalimia au unapojibu salamu. Marekani tabasamu ni ishara ya ukarimu, ndugu Mtanganyika usije ukafika Marekani watoto wa kizungu wakawa wanakutabasamia ukazani wanakutaka na wewe ukajimix kuwatongoza, utaharibu kila kitu, chonde chonde hizo hisia ziache Bongo.

Ndugu Mtanzania ukifika Marekani usifanye mazungumzo moja kwa moja na watoto usiowajua. Watoto wa Marekani wanafundishwa tangu wakiwa wadogo kuogopa wageni, na ukianza kuzungumza na mtoto asiyekujua utamtia kiwewe mtoto wa watu, na kama kuna mtu aliye karibu atafikia hitimisho lisilo sahihi kuhusu nia yako. Ikiwa una kitu cha kumwambia mtoto, mwambie mtu mzima aliye naye.

Ndugu Mtanzania ukifika Marekani usitoe maoni ya kudhalilisha kuhusu serikali au jeshi lao. Wamarekani wanathamini uhuru wao wenyewe wa kukosoa serikali na jeshi lao, lakini hawataki kusikia wageni wakikosoa nchi yao.

Ndugu Mtanzania hii point ninayoenda kueleza ni Muhimu sana, haswa ikiwa wewe sio Mzungu: Unaposimamishwa na polisi, USITOKE NDANI YA GARI LAKO NA KUMFUATA ASKARI. Kaa ndani ya gari lako na askari anapokaribia gari lako, weka mikono yako mahali ambapo askari anaweza kuiona.

Tatizo ni kwamba katika nchi nyingine au hapa Tanzania inachukuliwa kuwa ni adabu kumfuata police pale alipo, Kwa Marekani ni kosa kubwa sana askari anaweza kuwa na wasiwasi haraka sana ukifa hivyo, na hiyo inaweza kusababisha madhara makubwa, shuka kwenye gari pale tu atakapokuamlisha

VITU VYA KUFANYA UTAKAPOSHIKWA NA POLICE MAREKANI

(1) Zima injini ya gari lako
(2) Washa taa za ndani ikiwa nje ni giza (usiku)
(3) Teremsha kioo Cha mlango wa gari lako kama kipo juu
(4) Weka mikono yako kwenye usukani ambapo afisa wa polisi anaweza kuiona kwa urahisi
(5) Ukifuatisha hayo yote hapo juu then fuata kwa upole maagizo ya polisi (isipokuwa kwa maagizo ambayo hayafai, kama vile ombi la kupekua gari bila hati au sababu inayowezekana)

Ndugu Mtanzania narudia tena, Usitoke kwenye gari hadi uamliwe kufanya hivyo. Sasa jichanganye utoke kwenye gari utafurahia show.

Vivyo hivyo, usiguse pochi yako au kitambulisho hadi uulize. Ukianza kujigusagusa Police atadhani una bastora unataka kumdhuru, kwasababu Marekani kuwa na Bastola ni kitu cha kawaida na Sheria inawaruhusu yani ni kama wewe tu kuwa na namba za NIDA.

Inatosha kwa Marekani Wacha nikupe hints fupi fupi kwa nchi tofauti tofauti

ITALY
Italy: usivae nguo za Kiitaliano.

JAPAN
Japani: Ukifurahia huduma Nzuri iwe hotelini au mahala popote pale ndani japani usijidai Mshua saana ukatoa tip (Usitoe tip) ni ishara mbaya kwao, hawatachukulia kama wewe unavyoichukulia

UTURUKI
Ndugu Mtanzania ukifika Uturuki ukipewa chai usikatae kubali na inywe kwa amani ya moyo

INDIA
Ndugu Mtanzania ukifika India na Ukiona madume mawili wameshikana mikono huku wanatembea ni sawa kwao, inakubalika kijamii, usidhani kuwa wao ni mashoga. Nyingine kwa India ni kwamba usikanyage pesa, pesa inachukuliwa kuwa toleo la mungu wa kike katika dini ya Kihindu.

Hayo ni mambo baadhi kwa nchi ya Marekani na baadhi ya nchi nyingine kwa uchache pia unaweza nitajia nchi ambayo unataka kwenda au unataka kujua vitu gani havitakiwi kufanywa huko au ni mambo gani ya kuzingatia unapokuwa katika nchi ngeni na nitakujibu nikishindwa Watanganyika wenzangu watanisaidia

Huu uzi ni wa kila mtu, kuwa huru kueleza chochote kile unachokijua ili kutusaidia sisi Watanganyika wenzako

NB: Swala la kwamba utafikaje huko hilo ni juu yako Sina msaada wowote katika jambo hilo we niambie ushafika au unatarajia kwenda kwa namna unayoijua wewe then Mimi nitakupa hits.

MUNGU NI MWEMA

Screenshot_20220620-095839.jpg
 
Italians wamejaa bongo mpaka wamezaliana huku na wanaishi vizuri tu but huko kwao wanaongoza kwa ubaguzi hatar sana!
 
Naongezea ukifika Saudia ama Kuwait chonde chonde kama wewe ni Mkristo hakikisha usivae rozali wala usiweke Biblia kwenye begi wala picha ya yule Yesu wa kwenye snema na hakikisha simu yako haina password na huna hata picha ya mkeo kwenye simu na pia usiwke miziki yoyote ya kimagharibi kwenye simu na ikitokea umeingia kipindi cha mfungo wa Ramadhani usipige mihayo hadharani ukiwa umeacha mdomo wazi na mfano umeenda sokoni ukanunua ndizi ukiimenya unavyo taka kula ishike kwa mkono wa kushoto then wa kulia ndio umenye kisha ikate kwa mkono ndio ule usije ukala ndizi kwa ule mtindo wa kama unanyonya icecream aisee umeondoka maana hayo mataifa wanafuata shariya na tena zinafanya kazi kwa wageni tu.

Kufanya hivyo itakusaidia sana kuishi kwa amani usije ukadhani umejificha maana kila baada ya hatua kwenye maeneo ya public na roads zote ni mwendo wa cctv.Utashangaa tu polisi mwenye kanzu akaja kukuzoa hapo ndio utaelewa.
 
Naongezea ukifika saudia ama Kuwait chonde chonde kama wewe ni mkristo hakikisha usivae rozali wala usiweke biblia kwenye begi wala picha ya yule Yesu wa kwenye snema na hakikisha simu yako haina password na huna hata picha ya mkeo kwenye simu na pia usiwke miziki yoyote ya kimagharibi kwenye simu na ikitokea umeingia kipindi cha mfungo wa Ramadhani usipige mihayo hadharani ukiwa umeacha mdomo wazi na mfano umeenda sokoni ukanunua ndizi ukiimenya unavyo taka kula ishike kwa mkono wa kushoto then wa kulia ndio umenye kisha ikate kwa mkono ndio ule usije ukala ndizi kwa ule mtindo wa kama unanyonya icecream aisee umeondoka maana hayo mataifa wanafuata shariya na tena zinafanya kazi kwa wageni tu.Kufanya hivyo itakusaidia sana kuishi kwa amani usije ukadhani umejificha maana kila baada ya hatua kwenye maeneo ya public na roads zote ni mwendo wa cctv.Utashangaa tu polisi mwenye kanzu akaja kukuzoa hapo ndio utaelewa.

Sasa hapa kwa hawa washikaji mbn sheria nying snaa afu ndogondogo kwa mtu mgeni sio rahis kuzimaster kwa wakat mmoja utajisahauu afu itakulaa kichwaa
 
Haya wale wa kwenda South Korea

Ukifika huko ukiwa unapatiana au unapokea kitu basi Hakikisha unatumia Mikono miwili, usitumie mkono mmoja Ikiwa unatoa zawadi au unapokea business card au hata kupeana mikono, haupaswi kutumia mkono mmoja bali yote miwili. Ishara hii inafanywa kama ishara ya kuonyesha heshima.
Screenshot_20220620-125718.jpg
 
Back
Top Bottom