Mambo ya kuzingatia kwenye zoezi la usajili wa NIDA na taasisi nyingine

Samwel Ngulinzira

JF-Expert Member
Aug 5, 2017
1,829
1,958
Kutokana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia kumekua na mabadiliko mengi kuhusu utunzaji wa taarifa, hasa utunzaji wa taarifa kibiolojia. Mfano kuna zoezi la usajili wa vitambulisho vya wapiga kura, zoezi la utoaji wa passport za kusafiria, zoezi la vitambulisho vya taifa na utoaji wa TIN number.

Mazoezi haya yamekua yakikumbwa na changamoto kama ifuatavyo:

1. Ukosefu wa vitendea kazi vya kutosha. Nikichukulia mfano zoezi la usajili wa vitambulisho vya kupigia kura, kulikua na mashine 8,000 nchi nzima wakati wahitaji ni Zaidi ya milioni ishirini hali iliyopelekea watu wengi kukosa haki ya kujiandikisha. Pia hali hii imetokea kwenye zoezi la usajili wa vitambulisho vya uraia.

2. Ubovu wa miundombinu au miundombinu kutokua rafiki wakati wa zoezi la usajili. Hapa nazungumzia ukosefu wa intaneti yenye kasi maeneo ambayo zoezi linafanyika. Kazi ya intaneti ni kusaidia upakiaji wa taarifa za wanachama kwenye mfumo (online) pia kuzuia muingiliano wa taarifa za wanachama.

3. Wingi wa hatua za kufuata wakati wa usajili wa vitambulisho mfano itakulazimu kupanga foleni ndefu sana ili upate kuingiza taarifa zako mfano jina, kabila, umri, mahali ulikozaliwa na mahali unakoishi.

Baada ya hapo itakubidi upange foleni nyingine ili taarifa ulizoandika kwenye karatasi ziingizwe kwenye kompyuta (zipakiwe online kwenye mfumo wa usajili). Pia utapiga picha, kuchukua alama za vidole na kuweka saini ya kielektroniki ili kuzalisha kadi.

4. Kushindwa kufanya kazi kwa mashine husika. Ikumbukwe kila kituo kilikua na mashine mbili kwa mikoani na Zaidi ya mashine moja kwa Dar-Es-Salaam (vitambuisho vya uchaguzi). Unakuta mashine moja inachemka hadi inashindwa kufanya kazi inabaki mashine moja ambayo inachukua wastani wa dakika saba kuingiza taarifa na dakika saba zingine kukaa sawa sababu inakua imechemka sana.

Haya ni kwa uchache sana ingawa yapo mengi yanayohitaji kujadiliwa.


Nini kifanyike?

Ili kutatua changamoto hizi zilizojitokeza napendekeza yafuatayo yafanyike:

1. Zoezi la uandikishaji vitambulisho vya uraia liwe na awamu mbili zaidi. Baada yahii awamu ya kwanza ije awamu ya pili na awamu ya tatu ili Watanzania wengi zaidi wapate huduma hii ambayo ni haki yao ya msingi.

2. Uingizaji wa taarifa za awali (preliminary information) ifanyike on-line kama wanavyofanya bodi ya mikopo (HESLB) au watu wa uhamiaji kwenye electronic passport ambapo taarifa unaingiza mtandaoni kupitia kwenye linki iliyopo kwenye tovuti yao baada ya hapo unaprint copy unaipeleka ofisini kwao.

Hii itapunguza usumbufu wakati wa uingizaji wa taarifa hali inayowalazimu watu kupoteza muda wao kuingiza majina kwenye mifumo ya mamlaka husika wakati lingeweza kufanyika kabla halafu mtu anakwenda kukamilisha hatua zilizobaki.

3. Kuwe na ofisi za kudumu kwa mamlaka nilizozitaja. Hapa namaanisha NIDA na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili mtu anapofikisha umri wa miaka 18 anakwenda kujiandikisha sio mpaka asubiri zoezi lipite hali inayoleta usumbufu na watu kukosa haki zao za msingi.

4. Zoezi la vitambulisho vya uchaguzi lifanyke mapema ili kuepuka usumbufu dakika za mwishoni wakati tungeweza kufanya mapema.

5. Serikali iongeze vitendea kazi. Hasa mashine za kuprint kadi ngumu za plastiki (PVC cards). Hili linahusu mamlaka zote kuanzia NIDA, uhamiaji, TRA (TIN number na leseni) pamoja na tume ya taifa ya uchaguzi.

Mambo ya kuzingatia wakati wa usajili wa NIDA http://nida.go.tz/swahili/index.php/mambo-ya-kuzingatia-wakati-wa-usajili-2/


Mbali na hayo napendekeza taarifa zilizopo NIDA na tume ya uchaguzi (biometric informations) ziweze kufikiwa (accessed) na vyombo vya ulinzi na usalama, ili kusaidia kwenye uchunguzi wa matukio hasa yanayokua na uthibitisho mfano bunduki ikiokotwa wote walioishika wafahamike kupitia finger prints ambazo rekodi yake ipo tayari kwenye database ya taifa.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom