Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenza wa maisha

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
Ikiwa wale wanaokusudia kuoana hawataki kuwa na mashaka mengi wala kuwa na mambo kadha wa kadha ya kuwanyima furaha baada ya kufunga ndoa, imewalazimu kufikiria vyema na kwa moyo wote juu ya jambo hili na kwa wakati huu kabla ya kuoana.

Ikiwa hatua hii itafanywa kipumbavu, itakuwa mojawapo ya mambo makuu mno yawezayo kuharibu mafao ya mvulana ama msichana wawapo wamekwisha kuoana. Kwao maisha yataonekana kuwa kama mzigo wa laana.

Kaitka ulimwengu huu hakuna awezaye kumnyima mwanamke furaha, ama kumharibia maisha na kufanya yamuelemee na kumchoma moyo zaidi ya mumewe; na hali kadhalika hakuna mwenye uwezo wa kupooza matumaini na jitihada za mwanaume na kuposha nguvu zake, kuharibu mvuto wake na maendeleo yake zaidi ya mkewe. Mara nyingi ni tangu dakika ile baada ya harusi ambapo maisha huanza kuwaelemea wanawake na wanaume wengi. Ndoa ni jambo ambalo lina mvuto katika ulimwengu huu, na litakuwa na mvuto katika ulimwengu ujao pia.

Wengi hawaelewi vyema muungano huu wa ndoa. Wengi wao hudhani ya kwamba, muungano huu ni mojawapo ya njia ya kufikia upeo wa furaha; lakini laiti wangefahamu kiasi kidogo tu cha uchungu walionao wale waliounganishwa kwa kiapo cha ndoa ambacho kimewafunga kwa minyororo wasiyothubutu kuikata, hawangeshangaa kwa maelezo haya. Ndoa nyingi zinazofungwa huwa ni mkatale wa huzuni. Kuna maelfu ya watu waliounganishwa katika ndoa lakini hawapatani.

Wale wanaofikiria kuoa ama kuolewa ni lazima wajishauri vyema kuhusu hali na mwenendo wa ndoa wanayokusudia kuwa nayo. Ni lazima vijana wafanye uchunguzi wa kutosha katika mambo yanayohusu kuchagua mpenzi na kufanya uchumba. Ewe kijana mwenzangu, jihadhari ili kile unachodhania kuwa ni dhahabu ama lulu safi kisije kikawa takataka tu. Jambo hili halipaswi kufanywa haraka. Wakati ungali bado unaweza kupenda, jihadhari usije ukapenda kama kipofu.

Fikiria sana uone kama maisha yako na yule unayemchagua kuwa mwenzi wako wa maisha yatakuwa ya furaha ama ya kutopatana na kuhuzunisha baada ya harusi. Wanawake na wanaume wengi wameoana kana kwamba jambo la pekee lililowapasa kulijali ni kuwa wanapendana au la. Kuchagua mwenzi wa maisha kwafaa kufanywa kwa busara ili kuwawezesha wazazi na watoto pia, kuwa na hali nzuri kiroho, kiakili na kimwili.

Mambo ya kuzingatia katika kuchagua msichana wa maisha
Kijana wa kiume unapaswa uchague msichana ambaye atasiamama kando yake na ambaye ataweza kuchukua sehemu ya mzigo wa maisha yake, mke ambaye mvuto wake utamfanya mumewe na heshima na kumwezesha kuwa na mwenendo mwema, na ambaye kwa jili ya upendo wake, atamfanya kuwa na raha maishani mwake.

Ewe kijana wa kiume na mwanaume mwenzangu naomba ujishauri kwa uangalifu mkubwa kuhusu mambo haya yafuatayo na bila shaka kama yakizingatiwa kwa umakini yatakuwa msaada mkubwa kwako wewe mvulana mwenye nia ya dhati ya kuoa;
  • Je, huyo unayekusudia kumuoa atafanya nyumba yenu iwe ya furaha?
  • Je, yeye ni mwangalifu awezaye kutunza mali, ama akishaolewa hatapoteza mapato yenu tu bali pia atazitawanya mali zenu huku akionyesha upendo wa juu juu tu?
  • Je, huyo unayemtaka awe mwenzi wako ana hofu na kumcha Mungu?
  • Je, ana afya njema?
  • Je, ana bidii katika kazi?
  • Je, msafi wa kimwili na kiroho?
  • Je, ni mlevi?
  • Je, ni mtii, mnyenyekevu na mwenye adabu?
  • Je, anajiheshimu na kuvaa mavazi yenye heshima?
  • Je, ni mwaminifu?
  • Je, ni mtu anayetunza siri katika uhusiano wenu?
  • Je, ni mkristo, mpagani au mwislamu mwenzangu?
  • Je, mwenendo na tabia yake ikoje kwa wakati huu?
Nafahamu kwamba mvulana ambaye ametumbukia katika kisima cha mapenzi atayadharau maswali haya kana kwamba hayana maana wala manufaa yoyote, lakini hayana budi kufikiriwa kwa umakini na kwa ungalifu mkubwa zaidi.

Wakati wa kuchagua mke, tafakari na uelewe tabia na mwenendo wale, uone kama atakuwa mstahimilivu na mwenye bidii. Uone kama atachoka kuwatunza wazazi wako walo wazee wakati ule ambao watahitaji msaada wako. Uone kama atakushawishi utengane nao na kukushawishi umpende yeye peke yake na kusahau baba na mama ambao badala ya kupata binti watakuwa wamempoteza mwana.

Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mvulana wa maisha
Kabla msichana hajatoa mkono wake kwa mvulana na kuvishwa pete ya uchumba, kwanza na ajiulize kama yule mvulana wanayekaribia kuoana anafaa ama vipi. Mwenedo wake na tabia yake ya siku zilizopita ulikuwa wa namna gani? Je maisha yake ni masafi? Je upendo akuonyeshao unatoka moyoni na unaonyesha heshima na tabia njema ama ni upendo wa hivi hivi tu? Je anao mwendendo ambao utanifanya kuwa na furaha? Mimi kama mke nitaweza kuwa na furaha niwapo kwake? Je, ataniruhusu kudumisha tabia yangu na kunipa uhuru ama itanilazimu kutupilia mbali yote na kufuata matakwa yake? Maswali kama haya yakizingatiwa kwa busara yatakuwa na manufaa sana katika maisha yajayo ya msichana ambaye anatarajia kuolewa.

Kila msichana anayetamani kuwa na familia yenye furaha na amani, ambayo haitakuwa na udhaifu wala huzuni katika siku za baadae na ajiulize maswali haya kabla ya kutoa ukubali wake wa upendo.
  • Je, huyo unayemtaka awe mwenzi wako ana hofu na kumcha Mungu?
  • Je, ana afya njema?
  • Je, ana bidii katika kazi?
  • Je, msafi wa kimwili na kiroho?
  • Je, ni mlevi?
  • Je, ni mtii, mnyenyekevu na mwenye adabu?
  • Je, anajiheshimu na kuvaa mavazi yenye heshima?
  • Je, ni mwaminifu?
  • Je, ni mtu anayetunza siri katika uhusiano wenu?
  • Je, ni mkristo, mpagani au mwislamu mwenzangu?
  • Je, mpenzi wangu anaye mama?
  • Je, tabia ya mama yake ikoje?
  • Je, anatambua wajibu wake kwa mamaye?
  • Je, anajali upendo na furaha ya mama yake?
  • Ikiwa hajali wala hamheshimu mama yake, kweli ataweza kuonyesha heshima na upendo, wema na usikivu kwa mkewe?
  • Je, harusi itakapokwisha atakuwa na huruma kwa makosa yangu ama atakuwa ananikosoa mara kwa mara huku akiwa mgomvi na mkali?
Katika kuyajibu maswali haya shauklu nyingi yaweza kupishia mbali makosa na kasoro za mchumba wako, lakini upendo wa kweli hautaficha neno. Katika kuchagua mwenzi wa maisha, msichana na achague mvulana mwenye tabia na mwenendo safi wa kibinadamu, aliye na bidii, mwangalifu, mwenye heshima na aliye mwaminifu na mnyofu.

Ikiwa umefanya uchumba na mtu ambaye huelewi vyema tabia yake, usidhani kushika uchumba kutakulazimisha kuchukua kiapo cha ndoa na kuungana na mtu ambaye humpendi na ambaye wala hutamheshimu maishani mwako. Jihadhari sana unapofanya uchumba wenye masharti; lakini hata ukiwa ni uchumba wenye masharti, ni bora mara kumi kuuvunjilia mbali huo uchumba kabla ya kufunga ndoa kuliko kuja kuvunja ndoa baadae kama wengi wafanyavyo.


Nimeona niwadokezee vijana humu ndani namna ya kuchagua Mke Bora, ni dondoo tu ila uamuzi wa kuoa, kutooa unabakia kwako mwenyewe!!

Nimesukumwa kuandika hivi sababu nimegundua vijana wengi mtakuwa hamuoi; kazi yenu kuvizia vizia tu watoto wa wenzenu - siyo vizuri - tafuta wa kwako wa binafsi.

9b16ecfb472fc5f41bdd1b18ac1be835--african-braids-hairstyles-pretty-hairstyles.jpg




1. Mpenzi wako akija kwako na akakakuta unakula ugali na kachumbari na akaamua kula nawe..huyo muoe....

2.Ukimtangazia outing anakuja peke yake hakuji na marafiki zake kukuchuna.....na mkifika hotelini akaamua kuagiza ugali dagaa na maji tu...muoe anajua uchumi.

3.Mdada ambaye akimuona mkaka mwingine anaendesha Land cruiser na wewe una vitz yako Number A lakini akaamua kuja kwako...usimuache...

4.Mwanamke akikutembelea kwako akakuta nguo zako chafu akafua zote mpaka za wadogo zako, huyo mke usimuache!

5. Mwanamke unampa sh elfu tano akafanye shopping sokoni anakurudishia chenchi..huyo usimuache...anajua kubana bajeti na muaminifu.

6. Ukimpata mwanamke ambaye anakupigia simu na kukuuliza kama anaweza kukutumia credit au hela ya lunch, au anakupa pocket money saa nyingine, huyo tangaza ndoa fastaaa!

7.Mwanamke ambae anakupa password ya benki,laptop, simu na emails zake, huyo ni zaidi ya malaika.oa haraka..watamgombania wenzako!

8.Ukipata mwanamke ambaye mkipanda daldala analipa nauli au mkitoka out analipia bill ya chakula na vinywaji...huyo usimuache! anajua wajibu wa wana ndoa!

9.Ukimpata mwanamke ambae mnapokula, yeye anachagua mifupa tu na minofu anakuachia wewe, huyo usimuache...oa fastaaa... anajali afya yako!

10. Ukipata mwanamke ambae kila ukimuuliza angependa umletee nini ukirudi toka kazini, lakini yeye anakwambia hahitaji kitu ila anataka urudi salama, huyo ndio mke...sio kila siku unatumwa chips na kuku!



Je? Umesaumbuka kumpata yule atakayekuwa Baba/Mama wa watoto wako? Je? Ufunze mbinu kumi muhimu za kumchagua mchumba bora.Ukizifuata hizi hakika hutojutia.

Vijana wengi wamejikuta wakiitwa wahuni kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na makundi ya wanaume au wanawake. Hata hivyo wachunguzi wa masuala ya mapenzi wanasema idadi kubwa ya wapenzi si kigezo sahihi cha kupima tabia ya mtu na kumhusisha na uhuni.

Watalaam hao wanataja safari ya kupata chaguo halisi la mwanaume/mwanamke wa maisha ndiyo inayowaponza wengi kiasi cha kujikuta wameingia katika kashfa ya kuwa na uhusiano na dazeni ya wapenzi.

Wanasema msichana/mvulana anayeingia katika uwanja wa mapenzi kwa kuwa na hisia za kufanya ngono, hukosa umakini wa nani anafaa kuwa mpenzi wake kutokana na kukosa elimu ya uhusiano kutoka kwa wazazi wake.

Kwa mantiki hiyo, bila upembuzi wa kina, mtu asiye na elimu ya jinsi ya kumpata mpenzi wa kweli hujikuta ameangukia kwa mwanaume/mwanamke asiyemfaa, ambapo baadaye huamua kuachana na huyo na kwenda kwa mwingine kujaribu bahati tena ya kupata penzi la kweli.

Zinatajwa zawadi, hitaji la kusaidiwa kimaisha, mvuto wa kimahaba na mazoea kuwa ni vichocheo vinavyowaangusha wengi kwenye mapenzi na wasiowafaa.
Ukweli ni kwamba mtu aliyenaswa kwa ‘ujinga’, huwa hakatwi kiu ya penzi na mwanaume/mwanamke asiye chaguo sahihi la maisha yake.

Hivyo hufikia maamuzi ya kujiingiza katika uhusiano mpya mara 2,3,4,5 na kujikuta wakiambulia wanaume/wanawake wale wale wasio sahihi kwake.

Mwanamnke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Suzzy aliwahi kuniomba ushauri, akasema amechoka kuchezewa, maana kila mwanaume anayempata anakuwa si chaguo lake. Lakini kibaya zaidi kuachia ngazi au kutemwa huku akiwa tayari ameshafanya mapenzi na wanaume hao.

Nia ya swali lake ilikuwa ni kuniomba njia za kumtambua mwanaume mkweli bila kufanya naye mapenzi? Aliuliza hivyo huku akiwa na hoja kuwa wanaume wengi hawako tayari kuwa na uhusiano na msichana bila kufanya naye mapenzi na wakati huo huo huficha tabia zao chafu wakilenga kumnasa wamtakaye.

Binafsi nafahamu kuwa kuna wanawake/wanawake wengi ambao hujiingiza katika mapenzi kwa kutekwa na hadaa za mwili na kujikuta wanacheza mchezo wa kitoto wa pata potea.

Ni madhumuni ya somo hili kufundisha vigezo vya kumpata mwanaume/mwanamke halisi wa maisha, bila kufanya naye mapenzi. Njia hii ina faida kwa pande zote mbili yaani kwa mwanamke na mwanaume kwani kuacha au kuachwa bila kufanya mapenzi ni bora kuliko kuwa muonjaji, tabia ambayo huathiri kisaikolojia na ni hatari kwa afya.

Ifuatavyo ni njia ya kisaikolojia ambayo mwanamke anaweza kutumia kumpata mwanaume mwenye kumfaa bila kufanya naye mapenzi tena ni jibu sahihi la kuondokana na mchezo wa kubahatisha kwa wanaume wanaosaka wapenzi wa kweli na si taksi bubu ambazo mchana huweka namba za njano usiku nyeusi.
MCHUMBA.jpg

KWANZA- Ni ya mwanamke/mwanaume mwenyewe kujifahamu na kufahamu vigezo vya mpenzi anayemhitaji katika maisha yake. Ifahamike kuwa kila mwanaume ana wake na kila mwanamke anaye wake wa maisha pia. Hivyo asiyekufaa wewe anawafaa wengine, kinachotakiwa ni wewe kujitambua kwanza ili umtambue umtakaye.
Wanawake/wanaume wengi hawafahamu wanahitaji wapenzi wa aina gani, hivyo wanajikuta kama watu wanaoingia sokoni bila kujua wanataka kununua nini? Ndiyo maana wengi wameangukia kwa matapeli wa mapenzi, wakachezewe na kuumizwa moyo bure.

PILI- Ni kuketi chini na kuorodhesha vigezo stahili vya mwanaume/mwanamke unayemtaka. Baada ya hapo orodhesha tena kasoro za mwanaume/mwanamke unazoweza kuzivumilia na zile ambazo huwezi kuzivumilia kabisa. Hii inatokana na ukweli kwamba mwanadamu hajakamilika, ana upungufu wake.

TATU- Anza kumsaka kwa kutumia milango ya fahamu. Cha kufanya hapa ni kuruhusu macho yawaone wanaume/wanawake na kuwatathmini kwa maumbile yao ya nje na kisha kupata majibu kutoka moyoni juu ya kuvutia kwao ambako hutambulika kwa moyo kurithika na mwili kusisimka.

NNE - Kuanzisha safari ya kuchunguza tabia za nje na za ndani kivitendo. Hapa suala la ukaribu baina ya mwanaume na mwanamke linahitajika. Msingi unaotajwa hapa ni kujenga mazoea ya kawaida yasiyokuwa na masuala ya kimapenzi na ngono. Kutambuana, dini, viwango vya elimu, kabila na makundi ya marafiki ni mambo ya kuzingatia.
Katika uchunguzi huu mwanamke/mwanaume anayetafuta mpenzi hana budi kupitia na kumlinganisha huyo aliyempata na vigezo alivyojiwekea. Zoezi hili liendane na kuweka alama ya pata kila anapobaini kuwa mwanaume/mwanamke anayemchunguza amepata moja ya vigezo vyake. Lakini pia aweke alama ya kosa kwa kila kasoro anayoivumilia na ile asiyoivumilia.

TANO - Ajipe muda wa kutosha kati ya miezi sita na mwaka kumchunguza huyo mwanaume, kisha aketi chini na aanze kujumlisha alama za vigezo alivyovijiwekea na jinsi mwanaume huyo alivyopata au kukosa.
Ikibainika mwanaume aliyechaguliwa amepata zaidi ya nusu ya alama ya vigezo vilivyowekwa, basi ujue kuwa anafaa. Kuhusu alama chache alizikosa anaweza kusaidia kuzikamilisha polepole wakati wa maisha ya ndoa.
Lakini angalizo kubwa kabisa ni kwamba mwanaume/mwanamke akionekana kuanguka katika kasoro zisizoweza kuvumilia kwa zaidi ya alama tatu. Yaani kwa mfano ni mlevi, mwizi, muongo, mbishi na katika hizo kashindwa 3, huyu hafai, ni vema akawekwa kando kwani huwezi kubeba kero 3 kwa pamoja katika maisha.

SITA - Kusajili mapenzi yenye malengo yanayotekelezeka. Lazima baada ya kuchunguzana kwa kina wapenzi watengeneze muongozo wa mapenzi yao. Wasiwe kama wanyama, lazima mipango ya wapi wametoka walipo na wanapokwenda.
Hata hivyo watalaam wanasema lazima wapenzi wapime umakini wao kwa vitendo. Kama wamekubaliana kuoana, suala la mume kwenda kujitambulisha kwa wakwe na hatua ya kuiendea ndoa ionekane. Usiri usiwepo tena. Kila mmoja amuone mwenzake kama sehemu ya maisha yake na mara zote wasaidiane kwa ukaribu.

SABA - Ni vema ndugu wakashirikishwa ili kuwapa nafasi na wao ya kuamua kama mapenzi hayo ni budi yakaendelea au yakasitishwa. Ni ukweli ulio wazi kwamba licha ya wengi kupuuza maamuzi ya ndugu kwa madai ya kuwa hawana nafasi kwa wapenda nao, lakini uchunguzi unaonesha kuwa wapenzi wengi huacha kutokana na sumu za ndugu hasa pale wanapokuwa wameonesha kutounga mkono uhusiano wa wanaotaka kuoana

NANE - Hatua hii ni ya kuweza kuzungumzia ufanyaji mapenzi, hapa nina maana kama wapenzi wamejizuia kwa muda mrefu na wanahisi kuchoka wanaweza kujadiliana kuhusu hilo na kuamua ufanyaji huo wa mapenzi una lengo gani, kama ni kuburudisha miili basi suala la afya na uzazi salama litazamwe.

TISA - Kutimizwa kwa ahadi ya kuoana ni hatua ya tisa ambayo nayo si busara ikachukua muda mwingi kutekelezeka, kwani ucheleweshaji mwingi wa ndoa nao huvunja moyo na mara nyingine umewafanya wengi kutoaminiana.

KUMI - Kuamua kuwa mwili mmoja kwa kuvumilia na kuwa tayari kukabiliana na changamoto zote za maisha ukiwemo mkwamo na dhiki ambazo huchangia sana ndoa nyingi kuvunjika. Hapa pia ni wajibu wa wanandoa kuchukuliana udhaifu na kusaidia, kuwa tayari kujifunza na kujali zaidi upendo kuliko hisia za mwili ambazo wakati mwingine hudanganya na hivyo kumfanya mwanandoa asivutiwe na mwenzake.

Mwisho ni kwamba kanuni hizi huwafaa watu wazima mapenzi ya kitoto hayawezi kujenga misingi hii imara mara nyingi ni kudanganyana, kuharibiana maisha, kupeana mimba na maradhi.

Karibu tuendelee kuelimishana
 
Una miaka mingapi.umeoa? Na je umejifunza kutokana na 'makosa' au ndivyo ulivyoelimishwa kabla maana uzoefu wangu unaonyesha 'yaliowashinda' huwa wazuri saaana kushauri. Hehehe source kaka yangu
 
Young _ Master Mbona unapigana vita ambayo haipo?

Usirushe ngumi Hewani Hakuna adui huko

Sema tu Hakuna chanzo ila Nimeshushiwa na Mungu niwape wengine, Inatosha
 
Young _ Master Mbona unapigana vita ambayo haipo?

Usirushe ngumi Hewani Hakuna adui huko

Sema tu Hakuna chanzo ila Nimeshushiwa na Mungu niwape wengine, Inatosha

Ha ha haaaa!! Sawa sawa mkuu. Nimekupata.
 
Hongera kaka, watu wengine ni vilaza tu, wanachokijua wao ni kukosoa tu, kazi nzuri mkubwa!!
 
Back
Top Bottom