Uchaguzi 2020 Mambo ya kuzingatia ili usipate usumbufu siku ya kupiga kura

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
photo_2020-10-07_16-49-12.jpg

Ibara ya 5 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imempa haki kila raia aliyetimiza umri wa miaka kumi na minane kupiga kura.Kwa mujibu wa vifungu vya 13(1), 13 (2), 35C, 61 (3)(a) na 63(1) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 pamoja na kifungu cha 38 (1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani), Sura ya 292,Ili mtu aweze kupiga kura anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-

(i) Awe amejiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura:

(ii) Awe ana Kadi ya Mpiga Kura iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi;

(iii) Awe katika kituo alichojiandikisha kupiga kura

Sheria ya Taifa ya uchaguzi inamruhusu mtu kupiga kura kwa kufuata utaratibu ufautao:

(i) Mpiga Kura anatakiwa kwenda kwenye kituo cha kupigia kura alichojiandikisha akiwa na kadi yake ya kupigia kura.

(ii) Mpiga kura anatakiwa kupanga mstari akiwa kituo cha kupigia kura na kusubiri hadi zamu yake ya kupiga kura itakapowadia.

(iii) Mpiga kura anatakiwa afuate maelekezo yote atakayopewa na msimamizi wa kituo muda wote akiwa kituoni.

(iv) Baada ya kumaliza kupiga kura, mpiga kura anatakiwa kurudi nyumbani.
 
Swali mkuu, kama nikiwa safarini, nje ya jimbo na mkoa wangu, naweza kupiga kura ya Rais tu?!
 
(V) Mpiga kura anatakiwa abaki kituoni kulinda "bao la mkono" lisitokee.
 
Narusiwa kumpigia kura Lissu Mara nyingi zaidi nipendavyo
 
Kura ya Rais si inapigwa popote ukiwa na kitambulisho chako?.
Hapana Bosi,

Kwanza, huwezi kupiga kura kwa Rais peke yake, Sheria haiko hivyo, Sheria ya uchaguzi ni lazima upige kura kwa wote, kwa Rais, Mbunge na Diwani.

Pili, Sheria ya uchaguzi inasema, kila mpiga kura anatakiwa apige kura katika kituo alichojiandikisha, ,kwa mfano, Kama ulijiandikisha eneo la Kawe inabidi siku ya uchaguzi upige kura eneo la Kawe. kwasababu kadi yako ya mpiga kura umejiandikisha kawe.

Kwahiyo bosi. kama una mpango wa kupiga kura, usisafiri siku ya uchaguzi, vunja hizo ratiba za safari, baki kwenye eneo lako uliojiandikisha kupiga kura, ili uweze kupiga kura kwa wagombea wako.
 
Hapana Bosi,
Kwanza, huwezi kupiga kura kwa raisi peke yake, Sheria haiko hivyo, Sheria ya uchaguzi ni lazima upige kura kwa wote, kwa rais, kwa mbunge na kwa diwani.
Pili, Sheria ya uchaguzi inasema, kila mpiga kura anatakiwa apige kura katika kituo alichojiandikisha, ,kwa mfano, Kama ulijiandikisha eneo la kawe inabidi siku ya uchaguzi upige kura eneo la kawe. kwasababu kadi yako ya mpiga kura umejiandikisha kawe.
Kwahiyo bosi. kama una mpango wa kupiga kura, usisafiri siku ya uchaguzi, vunja hizo ratiba za safari, baki kwenye eneo lako uliojiandikisha kupiga kura, ili uweze kupiga kura kwa wagombea wako.
Kwa wengine haiwezekani kusafiri kwa ajili ya hilo tukio la siku moja.,

Mfano; ina maana mwaka huu Serikali nzima iliyohamia Dodoma wote hawatapiga kura?.itabidi kusafiri kurudi Dar ktk vituo vyao?.
Hili ni janga!!

Sijui kama Tume ama Serikali kwa ujumla wameliwaza hili.,
 
Bosi ndio sheria hizo, sasa kama ulijiandikisha Dar na umehamia Dodoma, hapo hamna namna lazima urudi Dar upige kura., kama huniamini subiri siku ya uchaguzi ukiwa huko huko Dodoma halafu nenda kituo chochote cha kupiga kura huko Dodoma halafu tuone kama wasimamizi watakuruhusu kupiga kura. cha kukushauri hapo, omba likizo kwa mwajiri, siku ya uchaguzi uende ukapige kura Dar kwenye kituo ulichojiandikisha kupiga kura.
 
Hapana Bosi,
Kwanza, huwezi kupiga kura kwa raisi peke yake, Sheria haiko hivyo, Sheria ya uchaguzi ni lazima upige kura kwa wote, kwa rais, kwa mbunge na kwa diwani.
Pili, Sheria ya uchaguzi inasema, kila mpiga kura anatakiwa apige kura katika kituo alichojiandikisha, ,kwa mfano, Kama ulijiandikisha eneo la kawe inabidi siku ya uchaguzi upige kura eneo la kawe. kwasababu kadi yako ya mpiga kura umejiandikisha kawe.
Kwahiyo bosi. kama una mpango wa kupiga kura, usisafiri siku ya uchaguzi, vunja hizo ratiba za safari, baki kwenye eneo lako uliojiandikisha kupiga kura, ili uweze kupiga kura kwa wagombea wako.
Mimi nilijiandikisha kwenye draft la wapiga kura 2015 nikiwa Moshi, ila 2019 kipindi cha ku-update draftari la wapiga kura sikujitokeza.

Je mm bado nina sifa za mpiga kura ?
 
Mimi nilijiandikisha kwenye draft la wapiga kura 2015 nikiwa Moshi, ila 2019 kipindi cha ku-update draftari la wapiga kura sikujitokeza.

Je mm bado nina sifa za mpiga kura ?
Dah mimi sio mfanyakazi wa tume, naona sasa kila mtu anataka kuniuliza swali, kwa hio ishu yako, nenda serikali ya mtaa , ulipojiandikisha kacheki hilo maana huko ndio daftari la kupiga kura lipo.
 
Mimi nilijiandikisha kwenye draft la wapiga kura 2015 nikiwa Moshi, ila 2019 kipindi cha ku-update draftari la wapiga kura sikujitokeza.

Je mm bado nina sifa za mpiga kura ?

Kwa sasa uko wapi?

Je siku ya uchaguzi utakuwa wapi?

Kama upo ulipojiandikisha Mwaka 2015 na kama siku ya uchaguzi 2020 utakuwa Moshi mahali ambapo ukijiandikisha uchaguzi Mkuu ulopita Mwaka 2015 , hata kama hukupata nafasi ya kuhakiki bado jina lako utalikuta lipo kwenye mbao za kituo chako cha kupigia kura ulichopigia Mwaka 2015.

Ilimradi uwe na Kado yako ya Mpiga kura.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom