Mambo ya kuzingati wakati wa kuweka Joto kwa vifaranga

farmersdesk

Senior Member
May 26, 2012
164
120
UTANGULIZI

Kwanza tuanze kwa kujiuliza ni kwa nini vifaranga huwa wanahitaji kuwekewa joto katika wiki za mwanzo?

Utaratibu bora wa ufugaji wa vifaranga unaelekeza kuwa katika wiki za mwanzo za ufugaji wa kuku wakiwa vifaranga inalazimu wawekewe vyanzo vya joto kwa kutumia taa za umeme au majiko ya mkaa au vyungu vya joto au taa special za umeme. Hii ni kwa sababu zifuatazo:

Kwa kawaida joto mwili la kuku huwa si chini ya nyuzijoto 40 na huenda hadi nyuzijoto 41 wakati huohuo joto la mazingira huwa linaanzia nyuzijoto 25 hadi 30/32. kwa kawaida joto husambaa kutoka sehemu lilipo jingi kwenda kule lilipo chache, kwa maana hiyo joto litatoka kwenye mwili wa kuku kwenda kwenye mazingira kupelekea kuku kupoteza joto.

Wakati huohuo kifaranga anakua hana idadi kubwa ya manyoya hivyo kupelekea joto kupotea kirahisi zaidi na madhara kuwa makubwa zaidi.

Si hivyo tu, bali ukaribu wa mapafu ya kuku na mazingira huchangia madhara zaidi. Mapafu ya kuku tofauti na binadamu yenyewe yapo mgongoni karibu kabisa na ngozi hivyo kupelekea kupoteza zaidi joto katika hali hiyo.

Vifaranga hawana uwezo madhubuti wa mfumo wa uzalisha wa joto hii ni kwa sababu bado hawajapevuka vya kutosha.

Sababu zote tajwa hapo juu zinapelekea kuku kudhulika zaidi pale ambapo mazingira yanayomzunguka yakiwa na baridi. Hivyo kwa wiki za mwanzo atahitaji kuongezewa joto ili asiweze kupoteza joto na kumpelekea kufa, kuzorota kwa ukuaji na kudumaa.

Joto linalohitajika kwa wiki ya kwanza ni nyuzijoto 35 na joto hili huenda llikipunguzwa kwa nyuzijoto 3 kwa wiki mpaka litakapofikia nyuzijoto 26 kufikia hapo basi vifaranga hawatakuwa wakihitaji tena joto la ziada.

Swali: je, niitajuaje kama hili joto nililoweka linatosha au halitoshi?

Jibu: kuna njia mbili za kujua kama joto linatosha au halijatosha.

Njia ya kwanza inahusisha kutumia kutumia kipimajoto (thermometer) na kupima joto centimeter tano kutoka chini ya brooder na katikati ya brooder.

Ungana na familia ya wafugaji kupitia
1.TELEGRAM tafuta neno "farmers desk" kisha jiunge
2.INSTAGRAM KAMA @farmersdesk_tanzania
 
Kama huna hayo makitu ya kizungu ya kupimia joto njia ya asili nayoijua

Ni kuangalia vifaranga wakikusanyika kwa pamoja ujue wanahitaji joto na joto likiwa kubwa utaona wanaikimbia ile source ya joto hivyo upunguze joto au ufungue mapazia madirishani
 
Back
Top Bottom