Mambo ya kukumbushana kabla hujatuma application ya kazi

Magari damu

JF-Expert Member
Apr 24, 2020
432
756
Habari zenu ndugu zangu.

Katika harakati za kujipambania kutafuta ajira na kulingana na kasi ya teknolojia ya dunia inavoenda, kuna mambo muhimu sana ya kuzingatia kabla ya kusubmit application yako ya kazi

1. ATS-CV

Huu ni mfumo wa uchakataji wagombea (Applicant Tracking System) ambao hutumika kuchakata na kudhibiti CV za waombaji wa kazi. Huu mfumo unachambua, unahifadhi na kupokea CV kwa ajili ya kazi husika.

Kinachofanyika, kunakuwa na maneno (keywords) yanayohusiana na nafasi ya kazi husika, na iwapo CV yako haina keywords hizo, unakuwa disqualified kwenye mfumo ma huwezi kuwa shortlisted.

- Tumia ATS-FRIENDLY CV kwenye applications zako za kazi.

- Update ATS CV yako kila unapotuma maombi ya kazi tofauti.

- Ubora na mvuto wa Content za CV yako, huficha udhaifu wako na kukupa nafasi nyingi zaidi.

2. COVER LETTER
- Usicopy na kupaste barua ya maombi ya kazi.

- Andika barua yenye uhusiano kati ya nafasi unayoiomba na Qualifications zako kwenye CV yako.

- Edit barua yako kila unapotuma maombi tofauti ya kazi

3. EMAIL na COVER LETTER

- Ni muhimu kwa kila maombi ya kazi unayotuma ku-support application zako kwa email.

- Usitume document kwenye Email bila kuandika chochote.

- Muajiri anataka kujua ni kwa namna gani unaweza kuwasiliana kupitia maandishi. Huu ni uwanja wako kujitangaza.

4. VIAMBATANISHO / DOCUMENTATION

- Zipe majina professionally docs zako zikutambulishe.

- Usi-merge docs kwenye document moja kama hujaambiwa kwenye maelezo ya tangazo la kazi.

- Hakikisha una-scan vizuri documents zako ziweze kuonekana vizuri.

- Usitume docs ambazo hujaambiwa utume kwenye maombi ya kazi.

NB! UKIWA SERIOUS KWENYE ATS- CV NA KUFUATA MAELEKEZO YA KUAPPLY, UNAKUWA NA UHAKIKA 100% WA KUPATA INTERVIEWS NA KAZI NDANI YA MUDA MFUPI
 
Eeeh kumbe tanganzo la BIASHARA...!!...nazan tujikite kujiajiri zaid...IN AFRICA THEY ASK U??.. WHO SEND U?....watu wamepata kaz bila hata kuonesha vyeti
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom