Elections 2010 Mambo Ya Kikwete: Shule ya Shilingi billion 4.3 yajengwa Bagamoyo

Sasa mimi sijaelewa kitu kimoja mtoa mada!je hiyo ni shule inayojengwa na serikali au ni yake binafsi?
 
sidhani tatizo la elimu ya tanzania ni juu ya majengo tu. Tunahitaji kuweka swala la majengo pembeni na kujiuliza juu ya mfumo wa elimu na aina ya elimu hitajika! swali la msingi ni je elimu ni mtaji ama biashara. Kama ni mtaji basi serikali inabidi kuwekeza ili kutoa ushiriki mpana wa vijana kupata elimu bora! kama ni biashara umasikini utatugonga mpaka kwenye ugoko!
 
ndio hiyo shule ya vipaji maalumu ya sayansi tu?? wameanza kuwatenga watoto wetu tena, niliisikia kwenye magazeti asubuhi, ndoto za kimweri
 
Samahani wachangiaji. Hii habari imekaa kushoto.

Kujenga shule ni nini?

Alichofanya Kikwete ni kujenga jengo au shule?

Shule ni muungano wa Majengo, Wanafunzi, waalimu na vitendea kazi kwa walimu na wanafunzi.........

Hiyo hela ni ndogo sana maana ni kama nyumba mbili za Gavana wa Bank.

Sasa kwa shule yenye nyumba za waalimu na madarasa/offisi ........... ni hela ndogo tu.
 
taarifa ya habari itv jana usiku....
mwantumu mahiza alikuwa akizindua majengo.....
mkandarasi ndiye aliyesema ni project ya more than 4billions tzs.

Shule inaitwa je vile? Is this a special school au ndo kama zile za zilizojengwa kijini kwetu.... hata mil 400 hazijatumika inakuwaje hii iwe 10x more????????????????
 
Mr. Prezident ameamua kufanya mambo kwa kujenga shule ya billion nne. .... kule bagamoyo
mmesema sana hoo shule za kata, sasa kaja na kali zaidi ya billion nne
twende kazi

kwani shule hiyo watasoma familia ya Rais pekee acha kumwaga upupu hapa ni ya watanzania wote ukiwemo wewe au ndugu yako, rafiki yako na jamaa. Kama ingejengwa wilayani kwako ungemsifu sana JK.
 
shule hiyo imejengwa kwa fedha za nani? inaweza pia kuwa imejengwa kwa fedha za wafadhiri kwa ombi maalum kujengwa bagamoyo, ubaya uko wapi? kwani bakamoyo haiko Tanzania? acha ubaguzi wa kimajimbo. si kila kinachofanyika bagamoyo kafanya Rais, je una maelezo ya ziada kuhusu hilo?
 
Ya kwake inaitwa Baobab kama sikosei,ipo unapoanza tu kuingia Bagamoyo ukitokea Dsm..
 
Mr. Prezident ameamua kufanya mambo kwa kujenga shule ya billion nne. .... kule bagamoyo
mmesema sana hoo shule za kata, sasa kaja na kali zaidi ya billion nne
twende kazi
Sio mara ya kwanza kusikia ngonjera hizo, Nilitembelea kanda ya ziwa 5yrs ago, mwezi huu nimeenda, nikakuta niliko acha barabara inajengwa haijasogea. Huo ni usanii wa kikwete. Hata hivyo majengo tumeona mengi, tunacho paswa kusikia sio majengo, bali waalimu watapatikana vipi na watalipwa vipi. HUO NI USANII WA SIKU ZOTE.
 
JK very shrewd unadhani akipigwa chini kwao watampokeaje si lazima aache some landmarks kama shule ili ata kama akishindwa atasema hamkunipigia kura
 
That is not a serious statement or It is a statement which comes from a person who is not serious. How could he build all those schools?
 
Back
Top Bottom