Mambo ya Dathalama- chuna buzi kwa kwenda mbele!!

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,257
353
Niko kwenye kijibaa kimoja mitaa ya uswahilini na scene ninayoishuhudia mbele yangu ni kama ndoto vile. Yupo dada mmoja amejipiga mkorogo wa kueleweka na kwa kumtazama taratibu umbo lake na sura- mashalaah- si haba, amekaa peke yake anakunywa coke na kama meza mbili toka hapo alipokaa kuna jamaa mmoja hivi, kwa kumcheki chapchap kwa jinsi alivyovaa- anaonekana 'wakuja', huyu jamaa anapiga 'kili' baridi na haishi kumkodolea huyo dada aliye pembeni yake.
"Vipi kaka? mbona unaniangalia sana? umenipenda?" anauliza mwanadada bila haya kwa sauti kubwa tu huku jicho akilizungusha. Jamaa anaonekana wazi amepatwa na mshtuko, hakutarajia swali kama hili. "Aah, mtoto kama wewe kila mwanaume lazime akupende", jamaa anajibu huku akitoa tabasamu la mashaka. "Njoo basi tukae wote hapa mezani kwangu" na bila kusita, jamaa anahama na 'kili' yake na kuungana na mwanadada huyo.Kutokana na accent ya jamaa na intro yake kwa mwanadada niliyoiskia nagundua kuwa ni mfanya biashara wa mifugo toka mkoa fulani wa kanda ya ziwa.
'Waiter' mwanadada anaita kwa sauti na mmoja wa wahudumu bila kuchelewa anakuja kumsikiliza "Niletee chupa kubwa ya amarula" ,sikumsikia mshkaji akikaribisha kinywaji nikadhani labda atalipa mwenyewe, mind you mwanzoni alikua ana mwendo wa coke! Huku maongezi yakiendelea na mshikaji, namuona mdada akipokea simu na kumueleza mtu mwingine mahali alipo, baada ya kama dakika ishirini hivi anakuja dada mwingine na alipokaa tu kwenye kiti bila hata kukaribishwa, akaagiza kamzinga kadogo ka konyagi na bitter lemon.Dada mwenyeji sasa aliniacha hoi alipokuwa akitoa intro "Shemeji yako huyu" Jamaa huku akitabasamu akasema "Hee, yamekuwa hayo tena?" Akaulizwa "Unashangaa nini? kwani wapenzi si huwa wanakutana sehemu kama hizi pia?" Baada ya masaa kadhaa nashtushwa na sauti kubwa ya mdada wa kwanza, " Jikooooni", mtu wa jikoni alipofika akatoa order " Tuletee kuku mzima wa kuchoma na ndizi nne, naomba ufunge kwa kuwa tunaondoka muda si mrefu"
"Sasa mpenzi niambie umefika hoteli gani ili nikishaonana na mama nikutafute jioni? au utakuwa hapa hapa?" Mshkaji anaulizwa na yule dada wa kwanza, namsikia akitaja jina la guest moja ya Sinza ambayo mwanadada anaonekana kuifahamu lakini kabla hajaondoka anamwambia kuwa hana dola na anaomba mshkaji amuwekee dola tano ili mawasiliano yawe rahisi, jamaa akaingia king. Mzinga wa mwisho kabisa niliousikia ni "Sasa niachie kabisa basi hela ya taxi,si unajua daladala za Sinza zilivyo tabu jioni?" aflu kumi ikatoka shwaa!
Jamaa alipoletewa bill jicho lilimtoka kichizi, nilidhani angeanguka pale, nilimsikia tu akiongea kilugha mwenyewe baada ya kulipa lakini nahisi ilimbidi aguse mtaji kulipa hilo deni."Ndio mkome kuparamia mashankupe ya mjini" alisikika akisema mhudumu mmoja wa kike wa baa hiyo.
 
Kabla ya kununua bidhaa ulizia bei.Hayo mambo siyo Dar tu hata viwanja watu wanapelekwa Red Lobster sana ukija kushtukia bill sawa na mshahara wa siku nzima kama sio zaidi.

Zaidi ya yote tahadhari na ngoma!
 
Haka ka story nimekaleta makusudi hapa kwa kuwa nakereka sana na kasumba ya wanawake wengi- haswa walioko bongo kutotaka kuchangia bills wanapokuwa na wanaume iwe kwenye baa au hoteli. Kuna mbunge mmoja wa kiume alisema tabia hii hata wabunge wa kike wanayo pia, wakienda mnadani kwenye bia na nyama, wanatataka wabunge wanaume ndio walipe.I can understand kama mwanamke hana, lakini most of the time hela zao ziko likizo...
 
Samahani kwa hili nitakalo sema nimetafuta njia nzuri zaidi ya kulisema ila hili ndio best zaidi;

Katika kutafiti kwangu nimegundua wanawake wa TZ wengi haijarishi na kipato chao wanatabia hii,sababu kubwa ikiwa.....-

Wanaume wengi Tuwavivu kwenye sita kwa sita (swala zima la kufanya mapenzi),unamwachia mwanamke ahangaike weee...!
Wewe unasubiri tu pale kileleni ukifika unaangukia pembeni haijarishi kama na yeye ameridhika au la... wewe ukifika ndio mwisho wa mchezo wenyewe.
Sasa hii ndio sababu wao wakata futa njia ya kujipa RAHA,kwanza watuchuneee....alafu tukifika kule anakuvumilia umalize uchukue time....

Mara nyingi kwenye tafiti,yangu wanaume wenye kuwalizisha wanawake wao huishia kwenye mapenzi ya ukweli(yaani muendeleze wa mahusiano hayo) ikiwa ni pamoja ku-share hizo BILLS na mamba ya ndani ya kila mmoja

kama unabisha jaribu
 
Sanda una hakika gani? Je una ushahidi gani? Umepata nafasi ya kufanya utafiti na kupata "first hand experience"?
 
Sidhani kama una ushahidi wa haya uyasemayo Sanda.
 
Sanda una hakika gani? Je una ushahidi gani? Umepata nafasi ya kufanya utafiti na kupata "first hand experience"?

Mkuu Pundit,
Jawabu ni NDIO.

Nadhani hapa sio swala la uhakika wa hilo,instead ni sisi WAOAJI (Ingawa silipendi hili neno) tu-devote muda kwenye sehemu ile na tuache kuifanya ile shuguli kama KUTENGENEZA WATOTO tu ila pia ni sehemu ya kupata RAHA na UTAMU wa maisha yenyewe.

Mwana mke mwenye kupata mwanaume anaye mlizisha,siku zote anakua tayari kwa kila kitu,Nieleweke hapa 'I mean every thing'

Lakini hii kwa muda mmrefu imeshindikana kwani Hii MALE EGO inatufanya tu-miss out kwenye maisha yenyewe.Angalia wewe na KNS mlivyo uliza kwa pamoja kama ni "kweli nina uhakika" Yes nin uhakika 101%kutokana na tafiti yangu na Swali lenu kwangu linathibitisha hilo,kwamab HAMJUI HATA SABABU YA SISI kugeuzwa MBUZI wa shughuli ili TUCHUNWE.
Tuchukue muda kufikili na kubadili maisha yetu ya MAPENZI badala ya kufika kileleni tu ,tuanagalie TUNAFIKAJE KULE JUU !

Hivi Hamjawahi jiuliza "kwanini kesi za wanawake(hasa mama wa nyumbani)hawaishi kutembea na Ma-HOUSE BOY wao!?
Nistasema sababu hapa,Sababu ni ile ile,Baba sikuzote yeye anataka kufika kule tu bila ya kumtayarisha mama LAKINI House boy anamaliza ufundi wote kwa mke matokeo yake mapenzi yanahamia kwa HOUSE BOY na wewe baba Unaishiwa kupewa UNYUMBA TU (this how they prefer to call it,because its the pay back of what you toil for her and the family) na mapenzi anapewa mwengine and not mapenzi peke yake...hata shoping anafanyiwa na pesa za kujiweka safi na hata ule utari wako mzuri anapewa ajipulizie atleast harufu ya jasho imtoke.

sasa if you guys think i am joking please take time to research for yor self and mind you ANZA NHYUMBANI KWAKO sio kwa kimada
 
I dont think its anything to do with mapenzi hapa, whether unamridhisha mpenzio or not, hili suala la wanawake kuwategea wanaume bill inapokuja mezani naona limekuwa kama cultural issue. Ukimlipia mwanake chakula na kinywaji chake- anaona ndio unampenda na kumjali, anakuona wewe ni gentleman na mbaya zaidi wanaume tunaenjoy kufanya hivyo, hata kama mtu huna kitu unataka ujitutumue mbele ya mademu ilimradi tu uonekane unacho.
 
MKUU,
hIVI USHAWAHI KUSIKIA NENO "MARIO"?

HIYO INA MAANA WALE WANAUME WANAO ISHI KWA KUTEGEMEA WANAWAKE WANA LIPIWA BILLS,MAVAZI,NA KILA KITU WAO WAPO KWA KUTOA MAPENZI TU(KUMLIDHISHA MAMA KWA MANENO MENGINE)

SASA HAWA NAO TUWAITAJE ?wana chuna buzi.....?
 
Aisee Sanda mimi napingana nawe kwa 100% hii kitu haina uhusiano kabisa na swala la mapenzi.

Hii ni swala la culture zaidi, wanawate kwenye society zetu wamekuwa tegemezi kwa wanaume. Unajua hata mwana mke kama anafanya kazi bado mwanaume ndie anachukuwa majukumu. Na hii kasumba imekuwa kuwa baba ni mtafutaji na mama ni kutake care familia hii inakuja hata ukiwa na marafiki wa kawaida tuu wa kike wanataka wewe ulipe hata kwenye Daladala nauli inabidi ulipe. Nakumbuka nilikuwa na demu nikiwa Mlimani yeye alikuwa anafanya kazi Sigara tulikuwa tukitoka out tukienda kama Rose Garden alikuwa ananipa pesa ili nifanya malipo.

Kwa jamii kama Jpn ukitoka na mwanamke kila mtu analipa. Na sio tuu hivyo Mtu akikwambia tutoke kwa lunch au dinner ni kuwa kila mtu anajilipia.

Ukupe wa wanawake wa kiafrica na wa Kibongo ni tabia tuu hauna uhusiano na mapenzi hata kidogo. Huku ugaibuni tuu ukikutana na mbongo mkienda bar utalipa wakati mwingine inabidi ule kona babake.
 
MKUU,
hIVI USHAWAHI KUSIKIA NENO "MARIO"?

HIYO INA MAANA WALE WANAUME WANAO ISHI KWA KUTEGEMEA WANAWAKE WANA LIPIWA BILLS,MAVAZI,NA KILA KITU WAO WAPO KWA KUTOA MAPENZI TU(KUMLIDHISHA MAMA KWA MANENO MENGINE)

SASA HAWA NAO TUWAITAJE ?wana chuna buzi.....?

Hao tutawaita ni Sex slaves. Hapo ni kutuiwa kuridhisana na unapata malipo. Ni sawa na kwenda kununua mdoli tuu wa kukufanya musterbation (Orgasm). Wewe unafikiri hao wanaume wange kuwa na uwezo wa kifedha wangekubali kuwekwa kinyumba na kulishwa ili watoe huduma?
 
Aisee Sada mimi napingana nawe kwa 100% hii kitu haina uhusiano kabisa na swala la mapenzi.

Hii ni swala la culture zaidi, wanawate kwenye society zetu wamekuwa tegemezi kwa wanaume. Unajua hata mwana mke kama anafanya kazi bado mwanaume ndie anachukuwa majukumu. Na hii kasumba imekuwa kuwa baba ni mtafutaji na mama ni kutake care familia hii inakuja hata ukiwa na marafiki wa kawaida tuu wa kike wanataka wewe ulipe hata kwenye Daladala nauli inabidi ulipe. Nakumbuka nilikuwa na demu nikiwa Mlimani yeye alikuwa anafanya kazi Sigara tulikuwa tukitoka out tukienda kama Rose Garden alikuwa ananipa pesa ili nifanya malipo.

Kwa jamii kama Jpn ukitoka na mwanamke kila mtu analipa. Na sio tuu hivyo Mtu akikwambia tutoke kwa lunch au dinner ni kuwa kila mtu anajilipia.

Ukupe wa wanawake wa kiafrica na wa Kibongo ni tabia tuu hauna uhusiano na mapenzi hata kidogo. Huku ugaibuni tuu ukikutana na mbongo mkienda bar utalipa wakati mwingine inabidi ule kona babake.

MKuu MTOTO WA MKULIMA,

Kwanza mimi siitwi Sada,Ni SANDA
Sikubariani na nakubariana na mawazo yako,Mimi sio naongea tu nime tafiti na hayo ndi majibu.
Unajua kwamba Culture hiyo hiyo ndio wewe inakufanya kukataa haya,Kama mwana ume wakiafrica unadhani kamba wewe ndio kila kitu na mwenye maamuzi yote at the expense ya mwanamke.

Dhana hii imekuwepo miaka mingi sana toka utawala wa Waarabu na hasa pwani ambako mwanamke alikua kama nichombo tu (Tamaduni na mila za kiarabu na sio Uisilamu)cha kukaa ndani na kungoja mume aamue kwa ajiri yake na hii ilichukuliwa kama ndio desituri yetu( watazania)
Baada ya watu kuanza kuamia mjini DASLAMU na kukuta wenyeji wakiishi namna hii.
Kama ujuavyo tamaduni inaendelea kizazi hadi kizazi mpaka ulipokuja kuvunjwa na utandawazi katika miaka ya hii ya karibuni.

Nakatika hili nadhani hiwezi kukataa yakua kuna wale ambao wamekua-left behind kutokana na elimu tu..!
Au kwao imeshakua desituri(mfano huyo Girl friend wako aliyekua ana kupa pesa ulipe bills) na wengine kutokana na maisha magumu wanaamua "kuchuna buzi" kwani wanaume ndio watafutaji.
na wengine kwa ajiri ya uvivu wao tu amabo hata wa Afrika wanume tunao nawameamua kuwa tegemezi.

Inategemea Bwana KNS na wewe mmeangukia kwenye kundi la wanawake wapi?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom