Mambo ya ajabu uliyowahi kufanya ukiwa shule ya msingi

Muzine

JF-Expert Member
May 4, 2017
32,366
60,399
Habari zenu wana Jf

Nakumbuka nikiwa shule ya msingi nilikuwa na tabia ya kuwapiga watoto wa walimu endapo huyo Mwalimu alinipiga lazima nimvizie mtoto wake nimpe ngumi ya nguvu.

Nikitumwa kuchota maji kwa Mwalimu ambaye simpendi lazima nitemee mate .

Naombeni mnisamehe natubu dhambi zangu .Msema kweli mpnz wa mungu walimu kuweni makini na wanafunzi jaman.

Mapovu ruksa kesho nina kazi ya udobi.
 
Nakumbuka ilikuwa mwaka mpya tuliiba kengere ya shule tukaipeleka bondeni kwenye chaka...
Ilikuja kupatikana baada ya mwezi.

Tabia ya kurusha mawe juu ya bati kwa walimu wakorofi.

Ilikamatwa barua namwandikia demu kumtongoza darasa la tatu
 
Mimi nilikuwa nawaibiaga mifagio wenzangu nikakusanya mifagio ya chelewa takriban 60. Nikaiunganisha nikaifungasha pamoja kuna dada mmoja anaitwa SINA alikuwa pande la mtu likaja kijiweni kwetu likanipiga kikumbo kimoja tuu mie huyo chini likachukua lile bunda la mifagio yoote likasepa shule nzima wakawa wananizomea mimi
 
Mimi nilipokuwa darasa la 3 nilikwenda shuleni na ulanzi au ulasi watu wa iringa mnaujua nilipokamatwa nao niliadhibiwa waliponiacha nikakimbilia nyumbani ile kurudi na gobore la babu begani mbona shule ilifungwa kwa muda hapa ni ukweli mtupu sitanii nilimsababishia babu matatizo makubwa sana japo alikuwa colonel mstaafu ila alisumbuka sana
 
Habari zenu wana Jf

Nakumbuka nikiwa shule ya msingi nilikuwa na tabia ya kuwapiga watoto wa walimu endapo huyo Mwalimu alinipiga lazima nimvizie mtoto wake nimpe ngumi ya nguvu.

Nikitumwa kuchota maji kwa Mwalimu ambaye simpendi lazima nitemee mate .

Naombeni mnisamehe natubu dhambi zangu .Msema kweli mpnz wa mungu walimu kuweni makini na wanafunzi jaman.

Mapovu ruksa kesho nina kazi ya udobi.
Umesoma boarding?
 
Machimbo wenzangu tupo wale wa kutoingia class na kujisahihishia na peni nyekundu.Tulikuwa tunakutuna kwa bikob*ro mtaalam wa kupika mihogo hapo ndio machimbo(majonzi) hatukosekani kizinga Primary Xul
 
Back
Top Bottom