mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,701
Nimebahatika kujumuika na wadau (wananzengo) kwenye fukwe za Ukerewe kipindi flani kimepita, hizi ni tofauti kabisa na fukwe nyingi duniani kama sio Tanzania.
1:Kule tunaogelea uchi wa mnyama, hakuna mbwembwe za kuvaa vivazi vya ujanjaujanja.
2:Kule wanawake wanasehemu yao na wanaume wanasehemu yao, ingawa wote wanakuwa uchi wa mnyama japo mnaonana kwa mbali.
3:Kule ukiogelea au kuoga vyovyote vile utakavyo ila ili zoezi likamilike lazima ujisugue mwili kwa mtego (dodoki maalumu), na kama umefanikiwa kuwa na machacha/magaga utakuta jiwe natural saafi pembeni kwa ajili ya kusugua hayo majamaa.
4Pamoja na shughuli zote, ukirudi nyumbani lazima uende na kakitu umeshika mfano labda ndoo ya maji, au samaki kutoka kwa wakokozi, au kigusu (jiwe maalumu la kusugulia ukoko wa ugali kwenye sufuria wakati wa kuosha vyombo), au chochote ingawa hii ni kwa wanawake zaidi.
5:Kule beach ni kilugha tu, hata kama mtu hakujui.Pia sabuni mnaazimana, hata iwe kicherema kiasi gani itawatosha wote na mtafurahi.
6Pamoja na anasa hiyo ya kuogelea ziwa la maji baridi, tishio la kuviziwa na mamba kutafunwa na kuchambuliwa kama karanga kinywani mwake liko palepale. kwa ufupi "Swim at your own risk".
Kweli tembea uone.