Mambo Unayotakiwa kufanya linapotokea tetemeko la ardhi

ze future

JF-Expert Member
Jan 2, 2020
204
295
Kwa mujibu wa tafiti za jiolojia tetemeko hutokea mara kwa mara, lakini mara nyingi ni hafifu mno, haisikiki na binadamu ila tu inapimwa na mitambo ya wataalamu.
Mara nyingine huweza kusababisha madhara kama uharibifu wa makazi na mali.

Tetemeko likitokea katika eneo la bahari, basi huweza kusababisha mawimbi makubwa ambayo huweza kuleta athari yanapopiga pwani na hujulikana kama Tsunami.

Majanga kama haya hayaepukiki lakini suala la msingi ni kujiandaa na ni muhimu kuwa na elimu ya jinsi gani ya kujilinda, ufanye nini wakati wa tukio ama baada ya tukio la tetemeko la ardhi.

MAMBO YA KUFANYA WAKATI WA TETEMEKO LA ARDHI

Shuka chini kisha ingia kwenye sehemu iliyofunikwa mfano chini ya meza, kisha shikilia ili isihame na eneo ulipo. Kama huna meza basi kaa eneo la ukuta ambalo halina dirisha, kama hakuna vyote basi weka mikono yako kichwani uzibe kichwa chako. Subiri hapo hapo hadi tetemeko litakapokwisha.

Kama upo kwenye jengo imara, baki hapo hapo

Kama upo ndani ya jengo lililochakaa basi tafuta njia salama ya kutoka nje.

Usitumie lifti kutoka kwenye jengo.

Tumia ngazi kufika nje ya jengo

Kama upo mbali na mlango wa kutokea ama kwenye jengo refu basi tulia na fanya mambo yenye ulazima tuu.

Usiharikishe kutoka nje, toka taratibu na kwa usalama.

Kaa mbali na vitu vya vioo ama vinavyoweza kuvunjika.

Kaa mbali na majengo yaliyozungushiwa vioo.

Kaa mbali na maeneo ya mteremko ili kuepuka kuangukiwa na mawe.

Kama unaendesha gari basi ingia pembeni ya barabara na usimame.

Usijaribu kupita kwenye madaraja
ambayo huenda yameharibika.

Mambo ya kufanya baada ya tetemeko la Ardhi,

Angalia kama kuna moto umetokea, kisha anza kuzima.

Angalia laini za umeme pamoja na maji kama zimeharibiwa.

Safisha kemikali zozote ambazo zinaweza kusababisha majanga mengine.

Fuata ushauri wa wataalamu ambao umetolewa kwa jamii.

Toa taarifa ya utakapoenda kama una mpango wa kuhama eneo lako la makazi.

MAMBO YA KUTOKUFANYA BAADA YA TETEMEKO LA ARDHI

Usiingie kwenye majengo ambao yameharibika kidogo, yanaweza kuanguka na kusababisha maafa zaidi.

Usitumie simu yako kupigia ndugu na jamaa, badala yake piga simu kupata msaada wa kiafya kwanza.

Usiendeshe chombo cha moto kwenye maeneo yaliyopata uharibifu.

Haya ni baadhi ya mambo ya kuzingatia katika tukio la tetemeko la ardhi, lakini suala la msingi linalosisitizwa na wataalamu ni kutulia. Unapaswa kutuliza akili na kuhakikisha unafanya maamuzi ambao hayatasababisha madhara zaidi kwako ama kwa familia au watu wa karibu wakati wa tukio.

Wakati wa tetemeko hupaswi kukimbia, ni rahisi kuanguka na kupata majeraha zaidi ukiwa unakimbia, upaswa kutulia ama kutoka eneo moja kwenda lingine kwa utaratibu.

Source; BBC News
 
Back
Top Bottom