Mambo tatanishi uamuzi wa kesi ya mauaji ya Abdalah Zombe na wenzie...

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,468
911,181
Nitafupisha hii hukumu na kuichambua siku zijazo.

UAMUZI HUU HAPA


http://www.judiciary.go.tz/wp-content/uploads/2016/09/CRIMINAL-APPEAL-NO.-358-OF-2013-ZOMBE0001.pdf

Kizungumkuti ni hiki hapa:-

Kama hukuwepo wakati wa mauaji basi hukuua!

Ni askari mmoja tu aliwaua marehemu naye hajulikani alipo hadi leo!

Ni ballistic tests zipi zilithibitisha marehemu waliuawa na bunduki mmoja tena ya polisi mmoja ambaye sasa katoweka?

Hivi polisi mtoro Mara ya mwisho ilikuwa ni lini alionekana hai na kwa nini hakutiwa nguvuni mapema?

Hivi inawezekana askari mmoja tu afyatue risasi na kuua bila ya wenzie kufyatua?

Marehemu waliuawa na risasi za kisogoni wakiwa wamefungwa Kamba. Yawezakana polisi mmoja kuyafanya haya yote dhidi ya marehemu bila msaada Wa mapolisi wengineo?



Tukio la wizi kwenye benki kutumika kama gheresha ya kuwakamata na kuwaua marehemu likanikumbusha jinsi general kombe alivyouawa na polisi

General Kombe ilidaiwa gari liliibwa Dar na walikuwa wakilifuatilia. Hivi magari mangapi huibwa yakafuatiliwa kwa umakini wa gari ya aina alilokuwa akiliendesha general Kombe hata wezi Wa gari kuuawa kinyama hivyo?


Taxi driver alikuwa shahidi muhimu lakini hakuchunguzwa ipasavyo.

Mfano polisi ni nani aliwatonya hadi kukamatwa marehemu


Ni polisi yupi aliyeruhusu marehemu watoke kituo cha polisi na kwenda kuuawa?

Fedha na Mali za marehemu polisi walizozikamata Leo ziko wapi?


Siku za usoni nitajaribu kuyapatia majibu maswali haya kulingana na nionavyo....
 
Wizi Wa benki ulitumika kama kisingizio cha kuwakamata marehemu na kuwapora fedha na madini yao lakini ni nani aliwatonya polisi nyendo za marehemu ni swala nyeti lakini halikujibiwa na hukumu tajwa
 
Aliyewatonya polisi alikuwa karibu sana na marehemu hivyo nyendo za dereva teksi zilipaswa kumulikwa vilivyo lakini hazikumulikwa
 
Ni wazi aliyewasaliti marehemu alikuwa anawasiliana na polisi kwa simu lakini so rekodi za simu za dereva teksi, mapolisi husika, marehemu au waliowauzia madini hazikuchunguzwa na hivyo kukosa ufahamu Wa mtandao Wa ujambazi unaowahusisha polisi, waendesha teksi, wamiliki au wahudumu Wa magesti na mabaa na wauza madini.
 
Back
Top Bottom