Mambo Saba (7) Unayotakiwa Kufanya Ili Kuongeza Kipato Chako Mara Mbili Kwa Kuwekeza Kwenye Viwanja Na Nyumba

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Haiwezekani kila anayewekeza kwenye viwanja na nyumba apate mafanikio makubwa. Hii inasababishwa na sababu mbalimbali.

Kwenye ukurasa huu nimekuandalia mambo saba ambayo yatakufanya kipato kiongezeke mara mbili kilivyo sasa.

Mambo 7 Ya Kuzingatia Ili Uongeze Kipato Mara Mbili.

MOJA.

Mtazamo chanya na nidhamu.

Unahitaji nidhamu ya kusimamia muda wako kuhusu uwekezaji kwenye viwanja na nyumba.

Unahitaji kujifunza tofauti kati ya mtazamo chanya na mtazamo hasi. Ili uweze kufikia malengo makubwa zaidi unahitaji mtazamo chanya.

Unahitaji nidhamu ya kufanya kile unachoamini na unachokifahamu kuhusu uwekezaji kwenye viwanja na nyumba.

Kama hauna sifa hii ya mtazamo chanya na nidhamu huwezi kunufaika na mambo sita (6) yanayofuata hapa chini.

Unahitaji mtazamo wa kujitoa mhanga.

Haiwezekani kujenga mafanikio makubwa kupitia uwekezaji huu endapo hauwezi kujitoa ipasavyo.

Kila siku utakuwa na sababu za kughairisha mipango yako ya kuwekeza kwenye viwanja na nyumba.

Usichukue kila mbinu kutoka kwa wawekezaji wanaokuzunguka. Tumia mbinu za uwekezaji unazozifahamu vizuri.

Mbinu ambazo zinakupa matokeo mazuri unatakiwa kuzitumia zaidi na zaidi.

MBILI.

Ukuaji binafsi (self-development).

Kila siku zinaibuka mbinu mpya za kuwekeza kwenye viwanja na nyumba. Kwa sasa kuna uwekezaji kwenye viwanja na nyumba zisizo halisi (virtual real estate investment).

Kuna vitabu vipya na vichache vilivyoeleza kwa undani zaidi kuhusu mbinu ya nyumba za kupangisha iitwayo B-R-R-R-R Rental Property Investment strategy.

Kwa kujifunza bila kukoma utaweza kufikia malengo makubwa zaidi ya kipato chako ndani ya muda mfupi kuliko kawaida.

Ili akaunti yako iwe na kiasi kikubwa cha fedha unahitaji kujifunza kila mara bila kukoma.

Ukiacha kujifunza kipato kinaanza kupungua hadi kufilisika kabisa. Ni sana kuendelea kujifunza maarifa sahihi.

Usiwe mwekezaji wa kutumia taarifa sahihi bila kutumia maarifa sahihi. Maarifa sahihi hukuonyesha jinsi ya kufikia malengo makubwa uliyojiwekea.

Taarifa hukuonyesha matokeo mazuri yaliyopatikana kwa kuwekeza kwenye viwanja na nyumba bila kuonyesha jinsi matokeo hayo yalivyopatikana.

TATU.

Kukuza mtandao wa wateja.

Hapa unatakiwa kuendelea kukuza wateja watarajiwa na kulinda wateja wa zamani. Hii inatakiwa kuwa ni kazi endelevu haijalishi umefikia hatua gani ya mafanikio.

Mitandao ya kijamii inaweza kukusaidia kukuza mtandao wako kwa haraka zaidi.

Mitandao ya kijamii ni kwa ajili ya kukusanya wateja watarajiwa na kuwakusanya kwenye kundi moja la Telegramu au WhatsApp.

Wakiwa kwenye kundi kwa muda mrefu watajenga imani kubwa kwako na litakuwa kundi sahihi kwako kuwekeza nguvu nyingi, muda mwingi na maarifa.

Njia ya mdomo ni njia bora kabisa ya kukuletea wateja waaminifu na watakaonunua tena na tena.

NNE.

Kuwafanya Wafuatiliaji Kuwa Wateja Halisi.

Kundi la WhatsApp au Telegramu ambalo wanachama wake hujifunza kuhusu uwekezaji wa viwanja na nyumba kutoka kwako.

Sio lazima utumie makundi ya WhatsApp na Telegram, barua pepe (email list) ni njia nyingine unayoweza kuitumia kuwafanya watu wajenge imani kwako kabla hawajawa wateja halisi.

Hapa unaweza kuendelea kuwashirikisha taarifa na maarifa mbalimbali kuhusu uwekezaji kwenye ardhi na nyumba.

Maarifa na taarifa unazotoa kwa kundi kubwa la wafuatiliaji yanakupa thamani kubwa zaidi ukilinganisha na kutoa taarifa na maarifa kwa mtu mmoja mmoja.

Wafuatiliaji wa huduma zako wanapokuwa wengi zaidi huchochea ukuaji wa thamani ya huduma zako. Hii itapelekea kipato chako kiongezeke mara mbili au zaidi ya mara mbili.

TANO.

Kupima matokeo ya mchakato.

Unatakiwa kupima kila mchakato unaokuwa ukipitia. Chochote ambacho hakipimwi, hufa kirahisi sana.

Hutakiwi kuendelea kuwekeza kwenye viwanja na nyumba bila kuwa njia za kujipima.

Kama unatoa huduma za udalali wa viwanja na nyumba unahitaji kujipima kila mwezi na kila wiki.

Kama unawekeza kwenye majengo ya kupangisha, unahitaji kupima ukuaji wa uwekezaji wako.

Kama unawekeza kwenye nyumba za kuhamishika, unahitaji kupima maendeleo ya uwekezaji wako.

Unatakiwa kupima matokeo ya njia unazotumia kuwafikia wapangaji wa nyumba yako. Unatakiwa kupima matokeo ya njia unazotumia kuwafikia wanunuzi wa nyumba yako.

Kwa kupima michakato unayopitia ya kuwekeza kwenye viwanja na nyumba, utaweza kuwekeza nguvu na muda kwenye michakato inayokupa mafanikio makubwa.

Unahitaji kuandaa ripoti za ukaguzi wa nyumba kabla hujanunua nyumba husika. Unahitaji kuandaa ripoti ya ukaguzi wa kiwanja kabla hujanunua kiwanja husika.

Unahitaji kuandaa ripoti ya makadirio ya mapato na matumizi kutoka kwenye nyumba unayotaka kumiliki. Ripoti hizi zitaisaidia timu yako kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati sahihi.

SITA.

Kuchagua Kazi Za Thamani Kubwa.

Kuna kazi kubwa ukifanya zinaongeza thamani yako na timu yako. Kazi za aina hizi ndizo unatakiwa kuwekeza nguvu na maarifa mengi kuliko kazi za aina nyingine.

Unatakiwa kutumia muda mwingi na nguvu nyingi kwenye kundi lako la wafuatiliaji wengi kuliko kutumia muda na mteja mmoja.

Kazi zinazoweza kuongeza thamani kubwa ni kama ifuatavyo;-

✓ Kutafuta wateja watarajiwa.

✓ Kufanya mazungumzo ya mikataba ya kuuza nyumba.

✓ Kutembelea projekti mbalimbali za uwekezaji kwenye viwanja na nyumba.

✓ Kuongeza mtandao wa wafuatiliaji wako.

✓ Kuandaa ripoti za ukaguzi wa nyumba, ripoti za ukarabati wa nyumba, ripoti za ujenzi wa nyumba mpya, mikataba ya upangishaji na kadhalika.

SABA.

Mamlaka na ushawishi.

Unahitaji kuwa na mamlaka juu ya muda wako, fedha zako, akili yako na mtandao wako.

Chagua aina ya watu wanaotakiwa kukuzunguka. Chagua muda mzuri wa kufanya mambo ya msingi ya uwekezaji kwenye viwanja na nyumba.

Chagua jinsi utakavyoamua kutumia fedha zako na sio kuendeshwa na maoni ya watu wanaokuzunguka.

Fanya na ongea kile ambacho akili yako huamini. Usifanye na kuongea mambo yahusuyo viwanja na nyumba ambayo huyaamini.

Pia, unahitaji kujifunza jinsi ya kuwashawishi wafuatiliaji wako ili waweze kulipia huduma zako za viwanja na nyumba.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

WhatsApp; +255 752 413 711
 
Back
Top Bottom