Mambo nisiyokubaliana nayo katika Serikali ya Magufuli

Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,745
5,446
Wadau wa JF, Vyamavingi sio mwanachama wa Chama chochote cha Siasa nchini ila ni muumini wa mfumo wa siasa wa demokrasia ya vyamavingi.

Uzi huu unaweza kuwasaidia watawala kujua mtazamo wa baadhi ya Watanzania wanaoingia humu Jamii Forum.

Binafsi namuunga mkono Rais wetu Dk. John Pombe Joseph Magufuli ktk mambo mengi sana kwenye utawala wake. Lakini hii hainizuii kuona kasoro zilizopo katika utawala wake wa Awamu ya Tano.

Yafuatayo ni mambo nisiyomuunga mkono JPM na Serikali yake:-
1. Kubana uhuru wa Vyama vya siasa na wanasiasa wa upinzani kuendeleza au kufanya kazi zao za kisiasa. Siasa nayo ni kazi kwa wanasiasa na Katiba inatoa uhuru wanasiasa kufanya harakati zao za kisiasa mradi tu harakati zao haisabaishi uvunjifu wa amani. Ikumbukwe kuwa Wapinzani wamekuwa na mchango mkubwa sana kwa Serikali ya CCM kupitia siasa zao za ukosoaji dhidi ya watawala.

2. Kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya Bunge kupitia TV na Radio. Katiba inatoa uhuru kwa wananchi kutafuta na kupokea habari. Ifahamike kuwa Watanzania tunayo haki ya kufuatilia mijadala inauoendelea Bungeni. Binafsi sifuatilii tena Bunge na wala sioni umuhimu wake baada ya kuzuiwa matangazo ya moja kwa moja.

Wadau wengine kuelezea mambo ambayo tunadhani Serikali ya JPM ina kasoro ili watendaji wake waweze kurekebisha.

Vv
 
Daahh uzandiki tuu hamna jema mmejaa roho ya kwanini na mtabaki hivohivo
Baadhi ya wafanyakazi kuondolewa kwenye malipo na kuwafanya waishi bila mishahara Tangu mwezi wa 4 wakati Wapo kazini ajabu wakurugenzi waliofanya Makosawamepewa ukuub wa wilaya
 
Kama mkuu ndiye anayeyataka utayakubali tu, Utawala huu ni wa Magufuli sio wa CCM wala Ukawa.

Watu walimchagua Magufuli sio CCM. Lazima utii hata ikiwa haukubaliani
 
Ni kweli, na kama kweli rais wetu anataka kukonga nyonyo za watanazania walio wengi, tunamuomba arekebishe kasoro tajwa
 
Kila siku tunasema humu, mtu akishasimama upande wa kile chama siku zote anakuwa hatari sana kwa mstakabari wa taifa hili. Watu wa chama kile wako mbali sana na maslahi ya taifa hili. Wanakipenda sana chama chao na wako tayari kuiangamiza nchi ili chama chao kiendelee kutawala. Hilo ndilo tatizo pekee. Sijasema chama gani.... kwa hiyo msinitafute kwa uchochezi!
 
Daahh uzandiki tuu hamna jema mmejaa roho ya kwanini na mtabaki hivohivo
Duh, mkuu, ukereketwa wa itikadi na ufuasi wa vyama usikufanye upoteze uwezo wako wa kufikiria na kuchambua mambo.

Anyway, una uhuru wa kufikiria chochote na kusema chochote, huo ni uhuru wa asili ambao ndio wengine tunautetea.

Vv
 
Maisha ndivyo yalivyo.Haiwezi kupata kila ukitakacho kwa kiwango kile ukitakacho kwa kila jambo.Kuchagua kunaenda sambamba na kuacha baadhi ya mambo bila kuyashughulikia.Rasimali ni chache, hatuwezi kufanya miujiza kurıdhisha kila mwanajamıı kwenye jamii ıliyochanganyika (heterogeneous).
 
Kama mkuu ndiye anayeyataka utayakubali tu, Utawala huu ni wa Magufuli sio wa CCM wala Ukawa.

Watu walimchagua Magufuli sio CCM. Lazima utii hata ikiwa haukubaliani

Wengi hawakumpa kura rais wa sasa, aliingizwa na system. Kukurukakara anazofanya ni kwamba Mr.president is being haunted by the truth - that he is in the state house not by the will of people! Do you think he is getting peaceful sleep? Ah wapi...
 
Kama mkuu ndiye anayeyataka utayakubali tu, Utawala huu ni wa Magufuli sio wa CCM wala Ukawa.

Watu walimchagua Magufuli sio CCM. Lazima utii hata ikiwa haukubalianiu
Wengi hawakumpa kura rais wa sasa, aliingizwa na system. Kukurukakara anazofanya ni kwamba Mr.president is being haunted by the truth - that he is in the state house not by the will of people! Do you think he is getting peaceful sleep? Ah wapi...

Umejuaje kwamba hapati usingizi wa amani mkuu Wambandwa!!! Thubutu, jamaa analala usingizi wa nguvu.

Inawezekana alichaguliwa na wachache ama wengi, hilo halina uthibitisho, ila usichukulia tu wewe na rafiki zako kumnyima kula basi ndio watu wengi walimnyima kura. wewe sio kipimo/kielelezo cha kwamba upande unaosimama au kuuamini ndio upande wa wengi. Elewa kuwa ukiwauliza pia wale wa upande wake nao watakupatia jibu hilo hilo kama la kwako, namaanisha ya kwamba raisi aliyepo madarakani alichaguliwa na wengi.

Mkuu ni nini cha kufanya....

Ni kuchapa kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo binafsi, hili la kuchaguliwa na wengi au wachache ishabaki historia na wala haitakusaidia. Kuhusu usingizi wa amani hilo linamhusu yeye, sidhani ikiwa lina tija yoyote kwako.
 
Sisi tuliomchagua tunakubaliana nae.

Nyumbu ni bora mngejikita kutafakari jinsi ya kupata mwenyekiti mpya maana huyu wa gia za angani mhh.

Mtasubiri miaka 200
 
Baadhi ya wafanyakazi kuondolewa kwenye malipo na kuwafanya waishi bila mishahara Tangu mwezi wa 4 wakati Wapo kazini ajabu wakurugenzi waliofanya Makosawamepewa ukuub wa wilaya
Daah inakuuma eee sasa uendelee kukaa nyumbani chuo hurudi tena kwa divisheni foo yako
 
Back
Top Bottom