Vyamavingi
JF-Expert Member
- Oct 3, 2014
- 5,794
- 5,507
Wadau wa JF, Vyamavingi sio mwanachama wa Chama chochote cha Siasa nchini ila ni muumini wa mfumo wa siasa wa demokrasia ya vyamavingi.
Uzi huu unaweza kuwasaidia watawala kujua mtazamo wa baadhi ya Watanzania wanaoingia humu Jamii Forum.
Binafsi namuunga mkono Rais wetu Dk. John Pombe Joseph Magufuli ktk mambo mengi sana kwenye utawala wake. Lakini hii hainizuii kuona kasoro zilizopo katika utawala wake wa Awamu ya Tano.
Yafuatayo ni mambo nisiyomuunga mkono JPM na Serikali yake:-
1. Kubana uhuru wa Vyama vya siasa na wanasiasa wa upinzani kuendeleza au kufanya kazi zao za kisiasa. Siasa nayo ni kazi kwa wanasiasa na Katiba inatoa uhuru wanasiasa kufanya harakati zao za kisiasa mradi tu harakati zao haisabaishi uvunjifu wa amani. Ikumbukwe kuwa Wapinzani wamekuwa na mchango mkubwa sana kwa Serikali ya CCM kupitia siasa zao za ukosoaji dhidi ya watawala.
2. Kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya Bunge kupitia TV na Radio. Katiba inatoa uhuru kwa wananchi kutafuta na kupokea habari. Ifahamike kuwa Watanzania tunayo haki ya kufuatilia mijadala inauoendelea Bungeni. Binafsi sifuatilii tena Bunge na wala sioni umuhimu wake baada ya kuzuiwa matangazo ya moja kwa moja.
Wadau wengine kuelezea mambo ambayo tunadhani Serikali ya JPM ina kasoro ili watendaji wake waweze kurekebisha.
Vv