Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,226
- 26,048
1. Nikiwa kiongozi wa nchi hii nitajikita sana kujenga sekta binafsi imara. Nitawawekea mazingira mazuri ya kukua na kustawi maana hawa hawajinufaishi peke yao. Kwa walivyojitoa kutoa mapesa kedekede ni dhahiri kuwa hawa ndo engine ya Taifa wakati wa amani na wakati wa vita. Sitaruhusu vyovyote sekta binafsi kubughudhiwa
2. Nitawaheshimu na kuwalinda wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji/ Matajiri. Kwa jinsi Rostam alivyotoa misaada amedhihirisha kuwa ni muhimu kuwalinda na kuwathamini wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji/ Matajiri. Dunia nzima umeona ni kwa jinsi gani watu hawa wamesaidia masikini na serikali zao kwenye janga hili.
3. Nitahakikisha tunaweka hifadhi kubwa ya Chakula kuwezesha kuwahudumia watu Milioni 20 kwa kipindi cha miezi kuanzia 10 mpaka 12. Ni dhahiri hatukuweka akiba cha chakula na Ndo mana hata tumeshindwa kuweka Lockdown kwenye kipindi hiki.
4.Uhusiano wa kimataifa ndo nguzo kuu kwenye maendeleo ya nchi na watu. Ukiwa kiongozi hakikisha unadumisha na kutengeneza sana mahusiano ya kimataifa maana wakati wa shida ni lazima utahitaji msaada.
5. Huduma ya afya ni jambo kuu kwenye Taifa. Ni bora kuweka huduma bora za vifaa mahospitalini kuliko kuanza kujenga mareli. Watu wanahitaji sana huduma bora za afya kuliko reli na ndege.
6. Kwenye kupanga matumizi lazima bajeti ya dharula iwe ina fedha za kutosha na ni kwa muda wote.
Asanteni