Mambo ni moto: Hotuba ya Upinzani (Mambo ya Ndani) kusambazwa mitandaoni

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,600
218,004
Hii ni kwa mujibu wa Waziri kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi Mh Godbless Lema alipoongea na waandishi wa habari .

Ikumbukwe kwamba Kambi rasmi ya upinzani imeamua kuachana na kusoma hotuba zake ndani ya bunge la Tanzania kutokana na hujuma za wazi zinazofanywa na Spika na Naibu wake .

Wito - Ukitaka kutatua utata kuhusu Mauaji ya Raia , Utekaji na watu kupotea ,ikiwa ni pamoja na wizi wa masanduku ya kura hutakiwi kukosa hotuba hii.

Mungu ibariki UKAWA
 
ni jambo jema. ila kwa mtazamo wangu wabunge wote wa upinzani waandae nondo kuhusu mapungufu ya jeshi la polis katika kulinda usalama wa raia na mali zao kwa ubaguzi. ikiwezekana wapeane semina kidogo namna ya kuweka wazi maovu ya jeshi la polis.
 
Tunakoelekea tunamhitaji Mungu kuliko wakati wowte kama taifa. Mambo mengi yana utata mwingi na majibu hayapatikani. Tatizo ni kuwa kadiri mwanadamu anapokuwa na maswali nengi yasiyo na majibu uwezekano wa yy kufanya maamuzi yasiyo na muelekeo ambayo yanaweza kuwa mazuri au mabaya. Kwa msingi huu ni budi Mungu aingilie kati hatima yetu cc kama taifa. Kama taifa tukiomba kwa bidii Mungu anaweza kutuvusha tukafika mahali pazuri tofauti nawengi wanavyodhani na kuanini kuwa hali c shwari tena. i
 
Back
Top Bottom