Mambo muhimu yakuzingatia baada ya kuachana na mpenzi wako

adamWaEden

New Member
Nov 24, 2020
2
1
Je? Wewe ni mmoja kati ya wanaosema maumivu ya kuachwa ni makali kushinda maumivu ya viungo vya mwili? Mbona ni kama unajaribu kuwashauri madaktari waanze kufanya oparesheni bila ganzi hivi? Enewei! Tuachane na hilo! Jambo la msingi ni kuwa kuna maisha baada ya Brekapu 💔!
Yafuatayo ni mambo flan hivi ya kipuuzi ya kuzingatia ili uweze ku'move on

Kwanza kabisa inabidi ukubali matokeo🙌🏾Ukiwa ruba ni sawa na kujiambia 1+1=11❌ huku ikifahamika wazi 1+1=2☑️. Ukiwaze sana mambo ya michezo ya Selina kuchezeana nywele🔞 kwani kila binadamu ana maajabu yake! Utashindwa kumsahau! Na kwa nini uendelee kung'ang'ania kwani huyo uliyeachana nae ulimuumba wewe!!!?😡 Kaa kwa kutulia.

Punguza ukaribu, weka umbali kwa Muda ikiwezekana wa mawasiliano📵 yasiyokuwa ya lazima! Ikibidi salam tu, mpe gwala🤛🏿 yaani ile "hi" hiyo ndo saizi yake! Isije ikasababisha mambo ya kupasha kiporo♨️(ON n'Off) ambayo utajikuta unarudi enzi za kina Vansco Dagama(kataa kuwa mtumwa). Kuwa bize na mambo yako maana kujaribu kumfuatilia pasipo yeye kujua yaani zile mambo za kumchungulia kwenye mitandao ya kijamii kuhusu nini anaposti ni sawa tu na kutaka kujua anaendeleaje. Usiwe spy(ghost follower)ni kujitekenya kisha unacheka mwenyewe. Hapa ndio malijendi wengine wanaamua ku'mblock mtu kabisa! mambo ya #hashtag kikono👋🏾 inakuwa pwetelea pwete!

Samehe ndio utasahau! Kama umeamua kuanza upya huna sababu ya kumkunjia kunji! Usimuombee mabaya wala kufurahia matatizo yake haitofanya mambo yako yawe mazuri! Maana unapoweka chuki automatikale utakuwa unaumia kila utakaposikia anapiga hatua kimaendeleo ila ukisamehe utakuwa na amani mpaka kumoyo

Usilazimishe Mahusiano mapya kwa kuwa tu unaogopa kupitia alichowahi kupitia Bwana Akon (usiogope upweke).Vita vya panzi ni furaha ya kunguru ndo hapa watu wa back bencha(wanaokufukuzia) wanapoteleza na teza..! Oh sorry nmechapia! Wanapoteleza na fursa ndo itabaki kama opsheni pekee ya kujiliwaza! Wakati duniani bado umebaki na vitu vingi tu vya kujiliwaza kwa mfano muvi,baga,selfie na mazagazaga kibao! usikae kinyonge! Acha vitu vifloo vyenyewe automatikale.Hayana mwenyewe hayo yalimshinda shahrukh khan.

#sindanoZamasaa💉
#streetmasterMind
 
Mtoa mada inaonekana bado unakosa raha sababu ya Ex wako kwahiyo umeona uje utulishe na sisi pumba! Sisi ma legendar hatunaga kabisa kitu kinachoitwa Ex tukipita sehemu hatuachi hata ushaidi
 
Kumsahau x ni rahisi, ila kuna siku utakumbuka ile sex mlikuwa mnafanya hapo ndipo noyo unaanza kujirudisha 😂😂😂
 
KWA KUONGEZEA VITU VINGINE MUHIMU VYA KUZINGATIA

1.UKIACHWA USIPENDE KUONYESHA SURA YA HURUMA ILI ALIYEKUACHA AKUONE HURUMA

2.UKIACHWA EPUKA KUMWOMBEA MABAYA MCHUMBA WAKO KWA KUFANYA HIVYO UTAZIDI KUUMIA

3.UKIACHWA FUNGUA UKURASA MPYA WA MAISHA KISHA

4.UKIACHWA TAFUTA MTU MWINGINE AMBAYE UNAMUONA NI BORA ZAIDI YA HUYO ALIYEKUACHA
 
Back
Top Bottom