Mambo muhimu ya kuzingatia katika maisha.Hasa kwa wanaume

Youngblood

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
18,919
54,990
Mambo muhimu ya kuzingatia katika maisha.

1. Usifikirie hata siku moja kwamba changamoto au matatizo katika maisha yako zitaisha.Watu wengi wanadhani kwamba wakifanya vitu flani au wakimiliki pesa nyingi au gari flani au wakipata kazi nzuri ,wakifanya kazi kwa bidii ipo siku watapumzika na kuenjoy maisha!,Maisha hayako hivyo, maisha yenyewe jinsi yalivyo ni msululu wa changamoto, furaha ambayo tunaipata ni baada kutatua matatizo tuliyonayo,mfano ukiwa na pesa,pesa zako zitakutesa, ukiwa huna pesa utateseka sababu huna pesa,ukiwa na boyfriend or girlfriend utateseka sababu upo kwenye mahusiano ,ukiwa single utateseka sababu upo single.Kwa kifupi ni kwamba chochote utakachokifanya lazima kitakuletea changamoto,hivyo usidhani ipo siku utaishi maisha ambayo ni problem free,hakuna kitu kama hicho, matatizo hayawezi kuisha ila yanaongezeka au yanapungua ukubwa jinsi siku zinavyokwenda,kitu cha msingi unatakiwa ufurahie kusolve matatizo uliyonayo,kama kipato chako ni kidogo jitahidi kufurahia hivyo hivyo au kama upo kwenye ndoa furahia ndoa yako hivyo hivyo na matatizo yenu na mwenzako,usisubiri wala usidhani ipo siku utaishi maisha ambayo hayana changamoto zitakazo kusumbua akili,mana hamna kitu kama hicho.

2. Mwanaume usiache kutafuta maisha ya ndoto zako kisa mwanamke.Kuna baadhi ya wanaume wako dhaifu kiasi kwamba anaweza kuacha kufanya kazi,au kwenda mbali kutafuta pesa sababu ya mwanamke, mwanaume halisi anajali ndoto zake kuliko mapenzi, furaha ambayo utaipata baada ya kupotezea ndoto zako sababu ya mwanamke itadumu tu kwa muda mfupi,ila baada ya hapo itapotea na hata huyo mwanamke ambayo alikufanya upotezee ndoto zako ataanza kukushangaa, kudharau,na hatimaye mahusiano au ndoa kuvurugika,ni kwamba hakuna mwanamke atakayekubali kuishi na mwanaume ambaye hawezi kujisimamia katika mambo ya maana,wanawake wanataka wanaume wapambanaji.

3. Usitumie familia kama kisingizio cha kutofanikiwa katika.Watu wengine wanashindwa kutoka na kwenda kutafuta maisha ya ndoto zao sababu tu anaogopa kukaa mbali na mke au watoto,ni heri kukaa mbali na familia au kututana nayo siku tatu ukiwa unaisapoti vizuri kuliko kulala ndani mwaka mzima huku huna mchongo wowote wa maana matokeo yake ni dharau kutoka kwa watoto na mama yao na mbaya zaidi hata mke utapigiwa na wenzako sababu unaonekana hujielewi.

.............................................................................
Youngblood
 
Matako ni muhimu kuliko maisha.banaweee ukisha kula kalimbwata ka Moshi ndo kabisaaa. Hata akikiuacha si umefaidi. Tafuta nyingine. Umeachwa si mara kibao tuu. kwani mtu akudharau na ukambagua na ukampotezea kuna shida?
 
Duh
Matako ni muhimu kuliko maisha.banaweee ukisha kula kalimbwata ka Moshi ndo kabisaaa. Hata akikiuacha si umefaidi. Tafuta nyingine. Umeachwa si mara kibao tuu. kwani mtu akudharau na ukambagua na ukampotezea kuna shida?
 
namba 2 = 50/50..... "Beyond the success of a man there is a woman behind...beyond the failure of a man look for a woman behind" mwisho wa kunukuu
 
Kila la kheri Mkuu,amini nakwambia ijapokuwa unaweza ukawa umemuacha mke na watoto kwenye huzuni lakini ukweli ni kwamba kwa upande mwingine wanafurahia kuwa na baba mtafutaji,baba ambaye yupo tayari kuiacha familia kwa muda mfupi ili kwenda kutafuta furaha ya familia ya muda mrefu.
Nasoma uzi huu nikiwa kwenye usafiri nimeiacha familia yangu naenda kutafuta hopefuly nitafanikiwa.
 
Back
Top Bottom