Mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kufanya uamuzi wa kubadili windows yako..

sijui nini

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
2,553
1,277
Baada ya kuona watu wengi wakipaa matatizo mbalimbali kutokana na jambo hili leo nimeona tupeane somo kidogo juu ya jambo hili. Ni mara nyingi utasikia mtu akisema nataka kubadilisha operating system(wengi wao wakiwa waumiaji wa windows) na baada ya hapo unakuta mtu huyohuyo anajuta kwa nini alibadilisha na anaanza kuhangaika tena na matatizo tena pengine zaidi ya yale yaliyokuwepo mwanzo. Sasa basi embu tuone mambo ya msingi/muhimu kabisa mtu anapaswa kuzingatia pale anapoamua kubadili OS ya pc yake. ..na nitaongelea kwa undani zaidi kuhusu kwa wale wanaotaka kubadili windows..

  1. KWA NINI UNABADILI WINDOWS?
Hili ni swali la kwanza kabisa mtu yoyote mwenye mpango huu anapaswa kujiuliza…kwa nini nabadilishe hii windows ninayotumia? Ina tatizo gani na limeanzaje? je ni kweli kubadili windows tu ndo suluhisho lililobaki? Kwa nini basi usitafute suluhisho la hayo matatizo kwanza kabla ya kuamua kuhama! Unauhakika gani ukibadili windows hayo matatizo hayatarudi tena? Kwa nini usi install fresh copy ya windows iliyokuwepo mpaka unaamua kubadili? Asilimia kubwa ya watu huwa wanabadili windows kwa sababu tu wamekutana na tatizo flani sasa bila kutafuta chanzo hasa cha tatizo hilo anakimbilia tu kubadil window na matokeo yake yanakuwa ni matatizo zaidi ya yale ya kwanza.Ni vyema basi kuhakikisha unatafuta utatuzi wa kudumu wa tatizo kabla hujaamua kubadili windows au angalau basi ujue kwa kina tatizo ni nini hasa..hii itakusaidia hata unapoamua kubadili windows na tatizo likijitokeza tena una solve kwa urahisi.

  1. FANYA UCHUNGUZI.
OK, umegundua ni kweli kuna tatizo na umejitahidi weee kutafuta suluhisho umekosa..umeamua ku install windows upya, jiulize hiyo PC yako ipo compatible na hiyo window unayotaka kuweka? Ili kujua hili ni rahisi tu..tafuta sehemu ya RUN kwenye PC yako (kwa windows xp click start>run>type “dxdiag” then enter, na kwa windows vista na seven click start kishakwenye sehem ya ku search type run utaona imekuja ya kwanza kwenye result ifungue kisha type “dxdiag” then enter ikija message yoyote click yes) hapo utapata maelezo ya kutosha kuhusu aina na model number ya pc yako. Kwa kutumia hizo data nenda kwenye web ya model ya pc yako tafuta model yako(unaweza pia ku search google kwa kuandika hiyo brand na model number yako moja kwa moja) kisha angalia aina ya windows inayoweza support. Brand nyingi za computer huwa wanatoa maelezo ya kila pcna model zao inaweza kuchukua window gani katika website zao. Ni vizuri uchunguze kwanza ujue kama pc yako inaweza beba hiyo window unayotaka kuweka na hii itakutibitishia uwezekano wa kupatikana kwa drivers zake kwa urahisi. Wakati mwingine unaweza ukaweka window kwenye pc afu ishu ikawa drivers…ukapata drivers na zikakubali ila ndo zikawa chanzo cha matatizo yako yoote bila wewe kujua. Si kila drivers inayokubali kwenye pc yako inafaa na ndo maana ckuizi kuna universal drivers kibao( unakuta sound ina universal driver zaidi ya moja) si kwamba zote zinafanya kazi vizuri kwa kila pc! Usipende kufanya mambo kwa kubahatisha, ipo siku utakuja lia…
Kitu kingine cha muhimu sana ni kujua software unazozitumia sana zinafanya kazi kwa window hiyo unayotaka kuweka? Mfano, ulikuwa unatumia xp na unapenda kutumia (au kazi zako zinahitaji sana ) software flani sasa unachange window labda kwenda vista au win 7bila kujua software yako kubwa sio compatible na win vista au seven na hawajatoa version inayokubali window hiyo matokeo yake unalazimisha wee na kusababisha matatizo mengine! Tabu yote ya nini…!?
  1. BACKUP…BACKUP…BACKUP…BACKUP….ALWAYS!!!
Najua wengi wanajua umuhimu wa hili ila wengi wetu huwa hatuna tabia ya kufanya backup ila tu mpaka pale unapopatwa na tatizo na unahitaji kuformatt ndo unaanza kufikiria ku backup…(ni ujinga)…weka tabia ya kubackup kila wakati na njia nzuri ni kuwa na either external drive au hata kufanya tu partirion ya hard disk yako na kuweka vitu muhimu vyote kwenye partition! Na wengi pia hawajui jinsi ya ku backup drivers zao wanapohitaji kufanya installation ya windows (haswa kwa wale wanaokuwa na haja ya kufanya installation ya fresh copy ya window ile ile) na hata wale ambao wanahitajikunadili windows… kuna baadhi ya model(haswa dell na Toshiba kidogo ) huwa drivers zake unaweza kuzi backup kwa urahisi tu sababu wakati wa installation ziantengeneza folders ambazo ni rahisi kuzitambua kwenye c drive unakuta kama dell ukifungu c drive unakuta folder kabisa limeandikwa dell/drivers ila kuna zingine drivers zinaenda moja kwa moja kwenye system files na kuzibackup hivihivi tu ni ngumu. Njia rahisi ni kutafuta driver detective software yoyote uinstall kisha kuna kuwa na sehemu ya kufanya backup kwa drivers zilizokuwa installed moja kwa moja, so una backup tu then unazitunza kama kwenye flash au ujuavyo na wakati wa kurudishia unainstall tena hiyo software then una fanyarestoring ya driver zako kama zilivyokuwa mwanzo…(yaani unabackup kabla yak u format then una restore baada ya kuformatt na driver zote zinarudi normal)…wengi hawajui hili!! Kwa kukusaidia kama huna hii driver detective chukua hapa full version :
DRIVER DETECTIVE FULL VERSION
chukua hiyo itakusaidia.

  1. FANYA UAMUZI SAHIHI..
Haya, baada ya kuyaona haya bado uamuzi upo kwako…bado unahitaji kubadili windows au?? Kama bado upo ulazima wa kubadili then CHUKUA HATUA..ila zingatia hayo niliyokueleza na hakika yatakusadia sana..usipende kushawishiwa..

  1. NYONGEZA..
Kumbuka ku set restoration point mara tu baada yak u install windows kabla hujaweka kitu chochote kingine kile! IPO SIKU UTAJUA UMUHIMU WAKE..

Kwa leo yangu ni hayo tu, kumbuka mambo haya nimeyatoa mwenyewe kwa kulingana na uzoefu wangu na inawezekana kabisa kukawa na mengine zaidi ya haya…kuwa huru kutoa maoni yako ili tuelimishane zaidi!!
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom