Mambo muhimu kuhusu uchaguzi wa Zanzibar

Tulime

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
248
104
MAMBO MUHIMU KUHUSU UCHAGUZI WA MARUDIO ZANZIBAR

1. Ulishirikisha wagombea wote 14 walioshiriki uchaguzi wa #Oktoba25 ambao ulifutwa baada ya kugubikwa na dosari kama vile mgombea urais wa CUF Maalim Seif Shariff Hamad kupoka mamlaka ya tume ya Taifa ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kwa kujitangazia ushindi ili hali chombo pekee chenye mamlaka ya kutangaza matokeo ni tume. Kosa hili ni la jinai. Ifahamike maamuzi ya ZEC hayaingiliwi wala kuhojiwa na chombo kingine chochote hii ni kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 Ibara ya 119 Kifungu cha (12&13)

2. Baadhi ya wagombea walidai kuiandikia tume barua lakini hazikukidhi matakwa ya sheria ya uchaguzi namba 11 ya mwaka 1984 ya ZEC chini ya kanuni za uchaguzi kwa mujibu wa Kifungu cha 130(1) ya sheria hii. Kanuni ya 28 Kifungu kidogo cha 1-3 ambavyo vinasisitiza barua ya mgombea iambatane na kiapo cha Jaji wa mahakama kuu Kwa mgombea urais. Kwa mantiki hii mbali na wagombea kuijua sheria na kanuni bado waliamua kufanya mazingaombwe ya kuitikisa tume ambayo ilisimama imara.

3. Vyama vyote vya siasa vina hadhi sawa katika chaguzi kwani vimesajiliwa Kwa mujibu wa sheria namba 5 ambayo inaviruhusu kufanya shughuli zake ambapo moja ya malengo yake ya msingi ni kushika dola. Katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar njia pekee ya kushika dola ni uchaguzi huru na haki unaozingatia misingi ya demokrasia. Lakini ni hiyari kwa chama cha siasa kuamua kushiriki au kutokushiriki katika uchaguzi.

4. Upatikanaji wa makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar utazingatia katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 Ibara ya 39 Kifungu 3 (i&ii) ambapo sifa ni mbili;Moja mgombea urais atakayekuwa wa pili lakini asiwe amepata chini ya 10% ya kura za Rais, Pili akikosekana Rais atamteua kutoka Chama kilichoshika nafasi ya pili kwa idadi ya wajumbe wa baraza la wawakilishi. Ndiyo sifa pekee za kumpata.
5. Idadi ya wapiga kura wote waliokuwa wameandikishwa na tume ya Taifa ya uchaguzi Zanzibar ZEC ni 503,580 idadi hii haijabadilika na iliyoshiriki uchaguzi wa #Oktoba25. Katika uchaguzi wa marudio wa #Machi20 waliojitokeza kupiga kura ni 341,865 sawa na 67.9% ya wapiga kura wote. Kura halali zilikuwa 328,327 sawa na 65.19% ya wapiga kura wote. Dkt Ali Mohamed Shein (CCM) alitangazwa kuwa mshindi Kwa kupata kura 299,982 sawa na 59.57% ya kura na ni 91.4% ya waliojitokeza kupiga kura ambao ni 341,865. Hivyo basi hata kama Maalim Seif Shariff Hamad angeshiriki uchaguzi huu asingebadili ushindi wa Dkt. Shein. Kwa mantiki hiyo maamuzi ya wazanzibar yaheshimiwe.

Anayewaza kufanya vurugu ili mazungumzo ya maridhiano au muafaka yawepo basi ajue nafasi hiyo haipo. Vyombo vyetu vya ulinzi vipo makini mno asivijaribu ataumia. Zaidi washirikiane na waliopewa dhamana kuijenga Zanzibar.
#MapinduziDaima #MuunganoUdumu #WazanzibariWameamua #MunguIbarikiZanzibar #MunguIbarikiTanzana.
 
kwa sifa izo mshindi wa pili ambae ni ADC hana ata moja sasa kipi kitafanyika ili apatikane makam wa kwanza
 
Ccm kazi munayo
Hapa nahisi katiba wataivunja mama wazee wa magamba roho zao ni kama wanyama vile
 
Usidanganyike au kujiimanisha kwa takwimu za upande mmoja tuu
Nani nje ya ccm na Jecha wake amethibitisha takwimu hizo?
 
Mimi imenikosha pale nilipofanya hesabu za kura zilizopigwa na zile za wagombea nikagundua kuwa kura za wagombea walizopata zimezidi. Yaani hesabu kamili ni zaidi ya 100%. ukipiga hesabu utakuta jumla ni 104.3%.
Jecha bwana hadi uchaguzi huu anadanganya wakati wananchi wote waliompigia Maalim hawajenda kupiga kura
 
Yaani awa mwisho, kura wamepiga wenyewe, mawakala wao wenyewe, walinzi wao wenyewe, walohesabu kura wao wenyewe, kila kitu wamefanya wao wenyewe machizi kweli kupoteza izo pesa tu kisiwa chenyewe maskini
 
MAMBO MUHIMU KUHUSU UCHAGUZI WA MARUDIO ZANZIBAR


4. Upatikanaji wa makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar utazingatia katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 Ibara ya 39 Kifungu 3 (i&ii) ambapo sifa ni mbili;Moja mgombea urais atakayekuwa wa pili lakini asiwe amepata chini ya 10% ya kura za Rais, Pili akikosekana Rais atamteua kutoka Chama kilichoshika nafasi ya pili kwa idadi ya wajumbe wa baraza la wawakilishi. Ndiyo sifa pekee za kumpata.

nadhani unakosea.

39.(1) Kutakuwana Makamo Wawili wa Rais ambao watajuulikana kama Makamo wa Kwanza wa Rais na Makamo wa Pili wa Rais.

(2) Ndani ya siku saba mara baada ya Rais kushika madaraka, atateua Makamo wa Kwanza wa Rais na Makamo wa Pili wa Rais.

(3) Makamo wa Kwanza wa Rais atatakiwa awe na sifa za kumuwezesha kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na atateuliwa na Rais baada ya kushauriana na chama kilichotokea nafasi ya pili katika matokeo ya kura ya Uchaguzi wa Rais.
Isipokuwa kwamba:-

(i) iwapo chama kilichotokea nafasi ya pili katika matokeo ya kura ya Uchaguzi wa Rais kimepata chini ya asilimia kumi (10%) ya kura zote za Uchaguzi wa Rais, au;

(ii) endapo Rais atakuwa hana mpinzani,
basi nafasi ya Makamo wa Kwanza wa Rais itapewa chama chochote cha upinzani kilichotokea cha pili kwa wingi wa viti vya Majimbo katika Baraza la Wawakilishi.
zanzibar.jpg
 
Back
Top Bottom