Mambo mengi tunayoona ni matokeo ya mambo mengi yasiyoonekana

GazProm, (GAZovaya PROMyshlennost) au Gas Industry ndio kampuni kubwa kuliko zote duniani katika uzalishaji na uuzaji wa mafuta na gesi. Utajiri wa gazprom unakadiriwa kuwa Dola billion 106, sawa na bajeti ya Tanzania ya karibu miaka 20. M/kiti wa GazProm ni moja kati ya watu watatu wenye Nguvu kubwa kisiasa huko urusi. wengine ni Rais na w/mkuu.
GazProm inamilikiwa na serikali ya Urusi na inasambaza asilimia 38 ya mafuta yanayotumia katika jumuia ya ulaya, na asilimia 32 ya gesi. Kwa mujibu wa takwimu, GazProm ina uwezo wa kusambaza mafuta na gesi katika nchi ya china kwa muda wa miaka 300. Zaidi ya hapo, GazProm inamiliki jeshi lake lenyewe.
Huo ndio ukuu wa Kampuni ya kufanya tafiti, kuzalisha na kuuza mafuta na gesi. Taarifa zinaonesha kuwa GazProm wanapowekeza katika kuzalisha bidhaa zake, huzilipa serikali za mataifa inamowekeza vizuri sana kuliko makampuni ya magharibi. Hulipa karibu asilimia 30.

Watanzania, baada ya ugunduzi wa kiwango kikubwa cha mafuta na gesi huko Mtwara, tumeshuhudia ugeni mkubwa kutoka mataifa Makubwa duniani.
Xi Jimping, Rais wa China mara tu ya kuchaguliwa alikuja Tanzania na kusoma hotuba yake ya kwanza kwa taifa lake la china na Dunia nzima mnamo tarehe 12 Aprili 2013. Kisha alisaini mikataba ya siri akaondoka.

Barack Obama, Rais wa marekani alidhuru Tanzania tarehe 01 julai 2013. Naye alipelekwa kukagua mitambo ya kuzalisha umeme iliyopo Ubungo, ambayo tunaambiwa ililetwa kifisadi na kashfa hiyo inamuandama Mh. Edward Lowasa hadi leo, lakini Rais wetu alimpeleka Barack Obama kuikagua.
Vilevile, Rais Obama alisaini mikataba ya siri akaishia.

Taarifa zinaeleza kuwa Obama alishauriwa na 'The Congress' kuacha kutembelea Tanzania kwa sababu ya ripoti mbaya ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na serikali ya Tanzania. Mauaji ya raia kwenye shughuri za kisiasa na utekwaji, uteswaji na mauaji ya wanaharakati. Dr. Ulimboka na Mr. Mwandosi ni mifano. Lakini kwa utashi wake Obama hakukemea ukiukwaji huo wa haki za binadamu, bali aliona kuna faida kubwa zaidi ya kutembelea Tz kwa Kaka yake wa hiari Mr. Jakaya Kikwete.

Vladimir Putin, The classic Putin, Rais wa Urusi alitarajiwa kutembelea Tanzania mnamo February 2015. Hakufika bali aliishia Misri. Tanzania haikusaini mkataba na GazProm, kampuni inayojali zaidi maslahi ya nchi inayoshirikiana nayo kulinganisha na makampuni ya magharibi, Stateoil, Puma energy nk.
Bernard Membe, waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa alimtembelea waziri mwenzake wa urusi, Sergei Lavlov January 2015, huko walizungumza kuhusu kuimarisha mahusiano ya kiuchumi na ulinzi wa kijeshi na usalama, Elimu na Pengine kuandaa mazingira ya ziara ya Rais Putin nchini Tanzania mwezi mmoja baadae, yaani Feb. 2015. La ziara ile haikufanikiwa!.

MASWALI.
1.Kwa kuwa GazProm wanashiriki katika tafiti za mafuta na gesi Tanzania, na sasa wapo huko ziwa Tanganyika na tafiti zao, na kwa kuwa wanatoa faida kubwa sana kulinganisha makampuni ya ulaya na Marekani, Je! Ni nini kilichopelekea serikali ya Tanzania kuitosa GazPron na kukumbatia wenye maslahi machache?

2. Je! Ikiwa kuna Nguvu iliyotumika kuzuia ziara ya Putin, ambayo ingeweza kupelekea serikali ya Tanzania kusaini mikataba na GazProm, je nguvu hiyo haionekani katika harakati za kuingiza mrithi wa mikataba ya siri Ikulu katika kipindi hiki cha uchaguzi?

Mwisho, tukumbuke maneno ya Prof. Kabudi Paramaganda, alioyasema katika ukumbi wa Ubungo plaza wakati wa kongamano la katiba mpya, "Tanzania ndio kiuno cha Africa, wanaoimezea mate Afrika wanaanzia Tanzania. Profesa alitaka kuonesha namna Geografia na historia ya Tanzania ilivyo rafiki kwa kuitumia kuidhurumu Africa. Kiuno ndio mahali nyeti zilipo. Kwa hiyo nyeti za Africa zipo Tanzania, ukiiweza Tanzania umeiweza Africa.

Mungu ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania sasa na baada ya uchaguzi.
Happy ndo kigugumiz
 
Back
Top Bottom