Mambo Mengi muda mchache, kijana aende wapi kati ya diploma ya CLINICAL MEDICINE NA PHARMACY

Binafsi naona kijana aende pharmacy kwanini kwa sababu
pharmacy ni kozi yenye mwanya mpana sana katika kujiajiri mfano unaweza kufungua duka la dawa baridi kwa ganzi ya diploma pia ukiwa na degree utapiga pesa sana hasa ukifungua pharmacy au hata labaratory pharmacy kam ile ya laicent medical industry katika ushalishaji dawa na vifaa tiba lakin pia diploma kwenda Bpharm ni rahisi zaidi kuliko CO to MD kwa sababu ya ushindani pia kama ukiajiriwa kwenye vituo vya afya mafamasia wanaitajika sana kuliko hata ma clinical unaweza uka kuta zahanati ya kijiji ma co wako wawili lakin mafamasi ni zaidi ya +
yote kwa yote good luck.
Unaongelea kinyume au hayo unayoyasema kwenye pharmacy au lab kama huna mtaji ni bure.
 
Unaongelea kinyume au hayo unayoyasema kwenye pharmacy au lab kama huna mtaji ni bure.
Jitahidi kuelewa unilichokiandika chanzo cha mafanikio ya kujiajiri yatategemeana na pesa uliyonayo kama kianzio cha pesa katika mtaji kwa sababu ukitaka kujiajiri lazima uwe na maarifa ama ujuzi/ pia hata kipaji fulani pili uwe na pesa kama kianzio tatu resonable areas au market for investment.
 
Jambo lingine hospital inaweza isiwe na Mfamasia,mtu wa maabara na nesi ila daktari akafanya yote tena kwa usahihi mkubwa ila haiwezekani hata siku moja daktari asiwepo afu kazi zikaenda.
Acheni kupotosha watu kwenye afya huwa wanategemeana na yaani hospital iwe na daktari tu? Hapana na msichojua katika hospital mtu wa mwisho kuhakiki makosa ya daktari ni mfamasia musichukulie poa
 
Elewa kwanza comment yangu kabla hujaniambia napotosha pia ni vyema ungelisoma moja moja tangu huko juu.
Acheni kupotosha watu kwenye afya huwa wanategemeana na yaani hospital iwe na daktari tu? Hapana na msichojua katika hospital mtu wa mwisho kuhakiki makosa ya daktari ni mfamasia musichukulie poa
 
Sijakukatalia..ila hayo unayosema sisi tumesoma japo sio deep tumesoma makundi,zinavyofanya kazi,madhara na drug interaction nk...wewe utatibu Malaria ila ni tofauti na mimi tabibu nitakavyotibu mimi nitazingatia kila kitu kuanzia severity ya ugonjwa na madhara mengine yatasababishwa na huo ugonjwa...mfano Mtu akiwa na Malaria kali wewe utafikiria tu Alu,Duo,Atequick na aina zingine ya vidonge ila mimi nitaangalia mbele zaidi labda nitaangalia Injection zaidi kutokana na hali yake...wewe utatibu matibabu mazuri mimi nitampa matibabu sahihi zaidi.

Yote kwa yote nawaheshimu pia.
Sasa ni Mfamasia gani atashindwa kujua kuwa huyu mtu ana Severe Malaria?..Watu wanasoma haya mambo na wanajua dalili za severe Malaria mkuu na wanajua kuwa kwa case hii inabidi mtu apate injection ya Artesunate..

Watu hawapo shallow kama unavyotaka kusema hapa..Watu wanasoma Clinical pharmacy 1,2,3..na huko ni magonjwa,pathophysiology yake ,aetiology yake na Pharmacological & non-pharmacological Management yake.

Hospital zetu bado ni local tu ndo maana hata kazi za Mfamasia hazionekani..mfano hospitali kali inabidi iwe na kitengo cha Therapeutic drug Monitoring..sasa kuna magonjwa yanatibiwa kiholele holela tu wakati ilibidi Therapeutic Monitoring ifanyike,mfano mtu ana Kidney Failure ila hata individualization ya dose haifanyiki,kuna dawa ukimeza lazima plasma concentration yake iwe monitored ili kusitokee toxicity yenye madhara lakini hili halifanyiki coz setting hizo hamna mahospitalini huku kwenye nchi zisizoendele..na mambo mengine mengi..hapa sasa ndo utakapojua Mfamasia ni nani hasa kwa upande huu wa hospitali.

Though daktari ni daktari na mfamasia ni mfamasia...Lakini tusijaribu kudharau shule waliyonayo wafamasia..sio ndogo.
 
Ukisoma Comment zangu hakuna mahala nimedharau taaluma ya mtu soma vizuri mkuu.

Kozi za afya zipo kama mwili wa binadamu kila kiungo kina kazi na maana yake...hata kwenye afya hivyo hivyo tunategemeana japo kuna ambao wanaweza kufanya kazi zaidi ya moja kwa usahihi.
Sasa ni Mfamasia gani atashindwa kujua kuwa huyu mtu ana Severe Malaria?..Tunasoma haya mambo na tunajua dalili za severe Malaria mkuu na tunajua kuwa kwa case hii inabidi mtu apate injection ya Artesunate..

Hatupo shallow kama unavyotaka kusema hapa..Tunasoma Clinical pharmacy 1,2,3..na huko ni magonjwa,pathophysiology,aetiology na Management.

Though daktari ni daktari na mfamasia ni mfamasia...Lakini tusijaribu kudharau shule waliyonayo wafamasia..sio ndogo.
 
The applicable figures can be available but time of application can make all prior features to be disqualified,all in all mama wa afya anaupiga mwingi.
 
C/O hana market kumshinda mtu wa maabara na mfamasia kwa kipindi hiki,kigezo au vigezo tunavyo vingi sana,hata wewe jiulize mtaani kwenu kuna maabara ngapi za afya ambazo ndani yake lazima kutakua na lab technician?na maisha ya watanzania wengi hawana muda wa kwenda hospitali kwasababu ukifika hospitali unaambiwa ufungue faili buku 5,kumuona dokta buku 5,ukiandikiwa vipimo ukatoe tena hela,bado dawa ukanunue,ukibisha bisha tu kwasababu tayari ulishaingia chaka,mfamasia ana soko tena kwa kipindi hiki ambacho sio wengi ndio kabisa.
 
Inasemekana na ina aminika kwamba,mfamasia anaheshimika sawa na Tabibu kwasababu anapaswa kusoma mambo mengi kama tabibu,kama jicho lako lina ukungu huwezi kuona hili.
 
Back
Top Bottom