Mambo matatu tu muhimu kwa Acacia/Barrick gold

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,605
8,744
Mimi kwa kukaa US kwa miaka mingi sasa na kusoma Finance huku na kufanya kazi kama consultant ninajua culture ya huku ya kampuni na ninajua Tanzania kwasababu mimi ni Mtanzania na nimekulia TZ kwa miaka 21 ya kwanza ya maisha yangu. Kuna mambo machache sana sana kwenye majadiliano ya TZ ambayo hizi kampuni zinaangalia

1. Kuhakikisha jina la Barrick haliharibiwi na hii skendo: Kuonyesha kwamba jina la Barrick haliaribiwi maana hii itasababisha (a) Share za kampuni kushuka (b) sehemu watakazo wekeza baadae kuwa ogopa mfano machimbo mapya hasa Africa na south america (c) uhusiano wao na serikali ya canada ambayo inajali sana kuonekana wako fair
2. Je pesa watakao lipa ni zaidi au pungufu ya pesa watakayopata kwa maisha yaliyobaki ya migodi. Kwa mfano kama serikali inataka walipe $700M wakati kwa maisha yote ya mgodi watapata $500M basi hawawezi kukubali maana ni hasara kubwa kwao. Lakini watakuwa tayari ku break even na kutokupata hasara kama serikali inasema $400 na wenyewe wanategemea kupata $500. Hivyo ni muhimu kwa serikali kujua kwamba je mpaka mgodi ufungwe ni thamani gani hawa jamaa watatengeneza kuanzia sasa ukitoa gharama zote. Lakini ki kubwa watajaribu kuondoka kana haitalipa bila kuharibu jina au kupigwa fine na serikali ya canada hilo ni muhimu. Vilevile tuelewe hawataweza kulipa zaidi ya $700 M na vilevile wataomba malipo kwa miaka mingi sio kwa mara moja ili wawe na cash-flow. Hivyo kama tunategemea pesa nyingi kwa mkupo haitatokea. Serikali inaweza ku switch issue ya pesa mfano wanaweza kuchukua ndege canada halafu Barrick wakalipa ile kampuni mfano ndege mbili kwa $400M halafu barric waka lipa polepole kampuni badala ya serikali kutoa pesa zote.
3. Watataka pesa na makubaliano yawe na mabaraka ya serikali ya canada ili kama wakitoa pesa na ikitumika vibaya lawama ziwe kwa serikali sio kwao hivyo wataweka serikali ya canada kama wasimamizi huru.

Ukweli ni kwamba hawatalipa pesa za ajabu ambazo tunataka maana si za kweli Acacia value ni around $2B na Barrick $18B tusitegemee watupe kwa mara moja $1B ni ndoto
 
Nitashangaa kama Barrick na serikali hawatatoa statement ya kuhusu majadiliano over the weekend!
 
Nchi hii haitakuja kuacha mikataka na mazungumzo ya siri ndiyo maana huwa tunafikia makubaliano ya hovyo kabisa
 
Barrick wanajali jina kwanza na wasipate hasara basi. Mambo mengine yote ni bla bla wenzetu wako strategic sana na wana weka mambo kirahisi zaidi
 
IMG-20170818-WA0023.jpg

Hivi huyo Mruma si anaendelea na MAZUNGUMZO au hayumo kwenye kamati.

Huu uteuzi si unaweza kumvuruga akili asiwe makini na mazungumzo au?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nime overestimate value ya Acacia ni only around $940 M kwa dollar. Hivyo hatutaweza kulipwa zaidi ya thamani nzima ya kampuni .....

In pound
Mkt cap 741.47M
MARKET CAP (M GBP) 768.090
 
Naomba kuuliza lakini. Je kama wataamua ku-file kesi MIGA mfano kwa sababu IPO katika mkataba iwapo mazungumzo hayatatoa majibu chanya tutafanyeje??
 
Mimi kwa kukaa US kwa miaka mingi sasa na kusoma Finance huku na kufanya kazi kama consultant ninajua culture ya huku ya kampuni na ninajua Tanzania kwasababu mimi ni Mtanzania na nimekulia TZ kwa miaka 21 ya kwanza ya maisha yangu. Kuna mambo machache sana sana kwenye majadiliano ya TZ ambayo hizi kampuni zinaangalia

1. Kuhakikisha jina la Barrick haliharibiwi na hii skendo: Kuonyesha kwamba jina la Barrick haliaribiwi maana hii itasababisha (a) Share za kampuni kushuka (b) sehemu watakazo wekeza baadae kuwa ogopa mfano machimbo mapya hasa Africa na south america (c) uhusiano wao na serikali ya canada ambayo inajali sana kuonekana wako fair
2. Je pesa watakao lipa ni zaidi au pungufu ya pesa watakayopata kwa maisha yaliyobaki ya migodi. Kwa mfano kama serikali inataka walipe $700M wakati kwa maisha yote ya mgodi watapata $500M basi hawawezi kukubali maana ni hasara kubwa kwao. Lakini watakuwa tayari ku break even na kutokupata hasara kama serikali inasema $400 na wenyewe wanategemea kupata $500. Hivyo ni muhimu kwa serikali kujua kwamba je mpaka mgodi ufungwe ni thamani gani hawa jamaa watatengeneza kuanzia sasa ukitoa gharama zote. Lakini ki kubwa watajaribu kuondoka kana haitalipa bila kuharibu jina au kupigwa fine na serikali ya canada hilo ni muhimu. Vilevile tuelewe hawataweza kulipa zaidi ya $700 M na vilevile wataomba malipo kwa miaka mingi sio kwa mara moja ili wawe na cash-flow. Hivyo kama tunategemea pesa nyingi kwa mkupo haitatokea. Serikali inaweza ku switch issue ya pesa mfano wanaweza kuchukua ndege canada halafu Barrick wakalipa ile kampuni mfano ndege mbili kwa $400M halafu barric waka lipa polepole kampuni badala ya serikali kutoa pesa zote.
3. Watataka pesa na makubaliano yawe na mabaraka ya serikali ya canada ili kama wakitoa pesa na ikitumika vibaya lawama ziwe kwa serikali sio kwao hivyo wataweka serikali ya canada kama wasimamizi huru.

Ukweli ni kwamba hawatalipa pesa za ajabu ambazo tunataka maana si za kweli Acacia value ni around $2B na Barrick $18B tusitegemee watupe kwa mara moja $1B ni ndoto
Bottomline ni kuwa kama wanadaiwa watalipa, kama hawadaiwi hawatalipa kamwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli ni kwamba hawatalipa pesa za ajabu ambazo tunataka maana si za kweli Acacia value ni around $2B na Barrick $18B tusitegemee watupe kwa mara moja $1B ni ndoto
Chakukushangaza hujawahi kukagua vitabu vyao halisi vya mapato zaidi ya geresha ya takwimu waonyeshazo kwa wanahisa....! Lakini una'shupaa' kuonyesha unajua in na out ya kile wanapata hao...! Naona, mbinu zinawaishia. Nawasifu waliofikiria mazungumzo haya kuwa siri. Kumbuka acacia hatambuliki huku kwa taratibu za tanzania mpaka sasa.
 
Nime overestimate value ya Acacia ni only around $940 M kwa dollar. Hivyo hatutaweza kulipwa zaidi ya thamani nzima ya kampuni .....

In pound
Mkt cap 741.47M
MARKET CAP (M GBP) 768.090
I bet these are 'pikwadi' data. However, the so called acacia is not in our balance equation! Upo?
 
Eti amesema US huyo halafu anajifanya kuelekeza Barrick cha kufanya watupige bao
 
Nasikia majadiliano hayaendi vizuri kwa serikali maana hawako realistic na namba zao. Vilevile kama livyosema mwanzo kama wanajua itakuwa hasara anyway wako tayari kurefusha maongezi hata kwa miaka... maana value kubwa ni jina na kuhakikisha stock zao hazishuki. Wakati huohuo watatumia muda huu kama wanajua watakataa offer ya serikali kutafufuta jinsi ya kuuza hiyo asset ya TZ
 
Back
Top Bottom