Mambo matatu muhimu katika maisha

Makonyeza

Member
Feb 2, 2020
69
252
Hello,
Kwenye maisha yetu kuna mambo matatu hutakiwi kuruhusu yakupite, ni haya yafuatayo:

1. Mazoezi:

Hatufanyi mazoezi ili tusajiliwe timu fulani, au tukashiriki mashindano kugombania zawadi, lah, ni kwa afya zetu tu.
Katika siku tano za wiki unahitaji kati ya dakika thelathini mpaka masaa matatu ya kufanya mazoezi katika siku mbili za mwisho wa wiki.

Kama mkimbiaji kimbia kilometa zako mbili, Tatu au zaidi kama ukiweza. Au ukiweza cheza soka ya wazee(veterans) kama sisi.

Itakusaidia kutoa jasho la mwili na kubadili mapigo ya moyo wako huku ukipasha moto misuli na mifupa, jambo lenye Tija kubwa kiafya.

Usinidanganye kwamba eti unashindwa kutenga nusu saa ya mazoezi kwa wiki mzima.

2. Elimu(kujifunza):

Elimu ni zaidi ya uijuavyo, ninmaanisha elimu ni zaidi ya kukaa darasani ukizitafuta Shahada na Stashahada.

Kila usichokijua na unayo fursa ya kujifunza ukakijua bila kujali aina ya mafunzo unayo Pata, hiyo ndo elimu.

Ukiwa na spirit ya kujifunza kila kinachowezekana kukijua kwako, nakuhakikishia utaelimika na hiyo elimu itakupa maarifa mengi na hatimaye utaweza kubadilisha maisha yako.

Kwa kifupi soma na ujifunze kila iitwayo leo Kadri unavyoweza, yaani kila leo usikubali kuwa yule yule kama wa Jana.

3. Ibada:

Hili ndilo kubwa kuliko yote.
Hukijiumba, wala hukuomba kuumbwa na wala hujui hatima yako, yaani hujui utakufaje wala lini utakufa.

YUPO anayejua majibu ya maswali yote hayo, KWANINI, kwa nini usirudishe shukrani kwake??

Ebu tazama, kwa wakristo ni masaa machache sana katika wiki, kwa waislamu ni dakika chache sana zisizozidi ishirini na tano kwa siku.

Mfano katika IBADA ya funga; hii tunaifanya ndani ya mWezi mmoja ndani ya mwaka mzima. Yaani miezi yote kumi na miwili unakula, unakunywa na kustarehe utakavyo.

Sasa kwa kuwa Kuna wengine hawapati chakula kama unavyo kipata wewe, maisha Yao ni dhiki kila leo.

MUNGU alitaka tujifunze kujua nini maana ya mtu akisema ana NJAA, ili iwe rahisi kwako kumuelewa na kumsaidia.

Ebu jaribu, amua kuanza leo, unaweza
 
Nakubaliana nawe kila hoja.

Naomba kujua kidogo hapo kwenye mazoezi, kwa wale hard worker ambao daily wanatoka jasho nao wana haja ya mazoezi
 
Soma vizuri sijaacha kitu hapo, ni uelewa wako tu. Angalia jambo la pili Elimu itakupa maarifa yatakayobadilisha maisha yako
 
Back
Top Bottom