Aliko Musa
Senior Member
- Aug 25, 2018
- 156
- 240
Kama ulinunua kwa makosa ardhi au nyumba zako, unahitaji kusoma makala hii. Kama una mpango wa kununua ardhi au nyumba, unahitaji kusoma makala hii.
Kama hujui ni nini hasa cha kuandaa kabla ya kununua ardhi au nyumba, unahitaji kusoma makala hii. Kama una nyumba yoyote ya kukuingizia kipato, unahitaji kusoma makala hii.
Kama una kiwanja au shamba, unahitaji kusoma makala hii. Kama una nyumba iliyokamilika na hakuingizii kipato endelevu, unahitaji kusoma makala hii.
Lakini nitaongelea zaidi kwa yule anayeanza kuwekeza katika ardhi na nyumba.
Karibu sana tujifunze mambo matatu (03) muhimu sana ya kuzingatia ili ununue nyumba au kipande cha ardhi:
Moja.
Usichukue Mkopo.
Huu ni ujumbe wa pekee kwako rafiki yangu. Hata kama una kila sababu ya kuona kwamba mkopo unaweza kukunufaisha. Kama ndio unaanza kuwekeza usichukue mkopo. Mazingira yatabadilika na kuifanya njia yako kuwa ndefu mno.
Kanuni niliipata kutoka kwa mwanauchumi G.Timothy Haight inasema kuwa "tawanya utajiri wako katika mlinganyo wa theluthi, theluthi moja weka kwenye ardhi na majengo, theluthi nyingine iweke kwenye biashara utakazokuwa na udhibiti ya moja kwa moja na theluthi ya mwisho iweke kwenye hisa na mitaji".
Kutoka na mlinganyo huu unatakiwa kuchukua jumla ya mkopo wa 30% ya utajiri wako wote. Kanuni hii unaweza kuisoma zaidi kwenye kitabu chake kiitwacho The Real Estate Investment Handbook (Kijtabu cha uwekezaji kwenye ardhi na majengo).
Kwa kanuni hii, asilimia 30 ya fedha zangu zote ninawekeza katika ardhi na majengo. Asilimia 30 ya fedha zangu zote ninapanga kuchukua mkopo. Asilimia 30 ya fedha zangu zote nawekeza katika aseti za nyingine.
Asilimia 10 ya pesa yote ina baki benki kwa ajili ya kushughulikia dharura za biashara zote. Huu mlinganyo wa 30%, 30%, 30% na 10% umeandaliwa na mimi mwenyewe kama maboresho ya kanuni ya Bwana G.Timothy Haight.
Sasa unahitaji mfumo kabla haujaanza kuwekeza katika ardhi na nyumba. Mfano, una tumia mfano wa mgawanyo wa hapo juu. Wewe ndio unaanza hivyo kwenye mkopo utakuwa na kiasi sifuri kabisa. Huhitaji kuchukua mkopo rafiki.
Sababu nyingine ya kutochukua mkopo pale unapoanza kuwekeza katika ardhi na nyumba ni kuwa unapokopa unaongeza kiwango cha kipato kitachokuwa kinaingia kila wiki au mwezi.
Pia mkopo huongeza hatari za kupoteza mtaji fedha hata ambao umetoka au kwa wanahisa wa kampuni lako. Sasa chagua uongeze hatari ya kuanguka au usubiri mfumo ambao utakuwezehsa kupiga hatua kubwa japo kwa kuwa subira.
Mbili.
Tathmini Gharama Za Uendeshaji.
Gharama za ukarabati wa nyumba unayotegemea kumiliki. Gharama ya kodi ya pango la ardhi au kodi ya majengo. Gharama ya usafiri yako wewe mwenyewe.
Gharama za kutafuta wapangaji. Gharama za matangazo ya kuuza au kununua ardhi utakayonunua kama utaiuza baada ya muda mfupi.
Gharama za chakula chako wewe mwenyewe. Hakikisha unatumia nguvu zako sana kuliko kutumia pesa nyingi kwa mambo ambayo unaweza kufanya wewe mwenyewe.
Kwa dunia ya sasa ni rahisi sana kupata mtaji kama utatumia nguvu na ukawa na subira. Hii ni kwa sababu ya teknolojia na maendeleo tuliyonayo ya kuwafikia watu wengi kwa muda mfupi kuliko miaka 200 iliyopita.
Usikubali kuajiri mtaalamu labda kama kitendo hicho kitaboresha sana ufanisi wa uwekezaji wako. Kama unajua kusoma na kuandika unaweza kupiga mahesabu wewe mwenyewe na kupata tathmini kamili. Kumbuka kuwa naongelea zaidi anayeanza kuwekeza katika ardhi na majengo.
Tatu.
Tathmini Asilimia Ya Kipato.
Katika uwekezaji kwenye hisa asilimia 7.5 kwa mwaka inaweza kuwa kipato kizuri tu. Katika hatifungani asilimia 4.5 kwa mwaka inaweza kuwa kipato cha kawaida.
Lakini kama ndio unaanza kuwa mmiliki wa nyumba, asilimia 10 ya kipato ya mtaji fedha inatosha kukufanya uendelee na uwekezaji wako.
Kadri miaka inavyoendelea ndivyo asilimia za kipato zinaongezeka zaidi na zaidi. Usikubali kumiliki nyumba ambayo inaingiza kipato endelevu chini ya 10% ya thamani ya nyumba yako ya kwa mwaka.
Wengi humiliki nyumba za kupangisha ambazo hazina manufaa yoyote. Chanagamoto za nyumba za kupangisha zimewachosha.
Wamiliki hao wanakuwa hawana tena mbinu bora za kuwasaidia kuongeza kipato kupitia nyumba zao za kupangisha.
Jambo hili linakuwa ni tishio zaidi pale ambapo mtu humiliki nyumba ya kwanza ambayo haina manufaa ya moja kwa moja.
Nyumba ya kwanza ambayo haingizi kipato endelevu na kipato chanya inakuwa ni mwiba kwa mmiliki husika.
Nyumba hiyo badala ya kuwa daraja la kukuza uwekezaji wake, inakuwa ni kikwazo cha kumrudisha nyuma.
Hatua tano (5) za kumiliki nyumba ya kipato endelevu na kipato chanya ni kama ifuatavyo;-
✓ Kuwa na mawazo na maarifa sahihi.
✓ Jifunze kutoka kwenye vyanzo sahihi vya maarifa ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo.
✓ Chagua na andika mpango sahihi kwako.
✓ Miliki nyumba sahihi ya kupangisha kwako.
✓ Simamia nyumba yako kwa namba sahihi za uwekezaji kwenye nyumba za kupangisha.
Nifanye niwe mmoja wa wanatimu wako wa uwekezaji kwenye ardhi na majengo. Unaweza kunifanya kuwa mmoja wa wanatimu wako kwa kulipia ada ya kundi la UWEKEZAJI MAJENGO.
Ukiwa mwanachama wa kundi hili, nitashirikiana na wewe kwenye kila kitu kuhusu uwekezaji kwenye ardhi na majengo.
Rafiki yako,
Aliko Musa.
WhatsApp/Calls: +255 752 413 711