KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,600
Ikiwa imebaki miezi miwili tuingie katika uchaguzi za serikali za mitaa na mwaka mmoja tuingie kwenye uchaguzi mkuu, mtazamo wa wananchi juu ya siasa umebadilika sana. Vyama vya upinzani vimeingiwa na hisia za kushindwa katika chaguzi mpaka kuwa na mtazamo wa kuhisi kushindwa kwao kunatokana au kutatokana na CCM. Hizo ni dalili za mwanzo kabisa za kuonyesha ushindi wa kishindo kwa CCM katika chaguzi zilizopo mbeleni ni Dhahiri na kama hali ya CCM kukubalika hivi itaendelea tuna uhakika wa 98% ya ushindi katika chaguzi hizo.
Kwa tathmini ndogo niliyoifanya, nimegundua kuwa CCM itapata ushindi wa kishindo katika chaguzi zijazo kutokana na mambo haya matano:
Kwa tathmini ndogo niliyoifanya, nimegundua kuwa CCM itapata ushindi wa kishindo katika chaguzi zijazo kutokana na mambo haya matano:
- Uongozi thabiti wa viongozi wetu wakuu wa chama
- Wapinzani kuwa wanaharakati
- Maendeleo yasiyo na chama.
- Ahadi zinazotekelezeka
- CCM kuendelea kuwa chama cha ukombozi