mambo matano yanayokera sana wanaume toka kwa wachumba zao

Bernard bakari

JF-Expert Member
Mar 30, 2016
407
781
Mapenzi ni furaha, upendo, amani na maelewano mema kwa wapendanao. Lakini wakati mwingine upendo hutoka kwenye hali ya kuwa ya furaha na kuwa kero na maudhi. Mambo yafuatayo hukera sana wanaume pale wanapofanyiwa na wachumba zao.

1. Kuja na rafiki yake pale unapomwalika au kumwita nyumbani. Ipo tabia ya wadada kuja na marafiki zao pale unapo mpa ofa, wengi hufanya hivyo kwa sababu kuu mbili, yawezekana anataka kuringa kwa rafiki yake au anaogopa mwanaume asije mng'ang'ania kwenye mambo yao yale. Hali hii ni kero kubwa inatuboa sana wanaume hatuipendi hata tone.

2. Kuwa busy na simu mwanamke anapokuwa na mpenzi wake. Hii smart phone za siku hizi na vifurushi vya chuo vimeharibu kabisa vijana wa leo, unakutana na mchumba wako mnakaa masaa matatu lakini ukija kupiga hesabu unakuta masaa 2:25 ametumia kujishughurisha na simu. Yaan hali hii inatuuzi sana yaan nyie acheni tu.

3. Kupenda kupiga mizinga ya pesa mara kwa mara. Wako wadada yaan asijue unafanya kazi wapi yaan bora ujishushe cv ili ubaki salama yaan mtu anaomba pesa leo kesho kutwa anaomba tena baada ya siku tatu anaomba tena. Watu hawana hata aibu kuwa huyu mtu ana matumizi yake, ana malengo yake, ana ndugu zake wanamtegemea. Jaman mjue nasi tuna matumizi yetu.


4. Kuchelewa kurudi nyumbani. Mabinti wengi wa kileo hawaoni umuhimu tena wa kuwahi nyumbani, Raha ya mke umkute nyumbani akupokee na kanga moja si unakuja nyumbani unaoga unakimbizana na tv mkeo bado hajulikani aliko inakera sana hii.

5. Kutoa adhabu ya kumnyima mpenzi unyumba. Wapo wanawake ukimkosea tu kifuatacho mzungu wanne. Jamana adhabu hii ni kero kubwa kwa wanaume.
 
Wanadai kuwa eti wewe ni kinara wa hiyo namba 3!!........Kuna ukweli wowote kwenye hilo jamani?
mm nipo single huyo wakumpiga mizinga namtoa wapi?? Si kweli ila wengi wanaamini hivyo kutokana na michango yangu kwenye mada km hizo, istoshe kuna uzi niliwahi kuandika
So wengi watanihisi hivyo but nipo tofauti kidogo
 
Hahahahaha! Hahahahaha! Na nyie baadhi yenu hamtabiriki kabisa mbona wapo mabinti wanaojielewa na wametulia mnoooo lakini mnawaacha tu.
 
Mkuu naunga mkono hoja, ila nasisitizia namba 2, kati ya zoootee ulizozitaja namba 2 ndio huwa inanikera kupita maelezo
 
Nimerejea mkuu..mbishembishe zilibana hii wiki moja nilikuwa offline
Pamoja mkuu.
Karibu sana.

Nusura nianzishe thread ya operesheni ya kukutafuta maana sijakuona siku kadhaa kama kawaida yako Font ferd, in Mkulu's voice
 
Back
Top Bottom