Mambo matano ambayo ukiolewa ni lazima uachane nayo;

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
(1) Kuchat Na Kuwasiliana Na X Wako;
Huyu hana nia nzuri na wewe, mlishaachana hata kama ni ile kuachana kwa wema lakini kuna mawili, ukimchekea sana atakugonga lakini mumeo akijua anakutimua. Hata mimi nakutimua, siwezi kumaucha mtu ATM Card yangu wakati najua ana password, labda kama huko Benki hamna kitu.

Nikiamini kuwa labda kama mumeo hakupendi ndiyo atakucha ujichekeshe chekeshe na X wako, ila kama anakupenda kakutimua, hawezi vumilia, hivyo achana naye usimfuatilie wala usiwasiliane naye, and yes msiwe marafiki. Vile viofa ofa anavyokupa hembua chana navyo kwani siku ukiachika basi nayeye humuoni tena.

(2) Kumuelezea Mama Yako Kila Kitu Kinachokutokea;
Mwanzoni ulikua unamuelezea siri zako, sasa hivi una mume, kila unachomuambia kinawahusu nyie wawili, kwanza unamvua nguo mumeo na pili akijua kua kila kitu ni kwa Mama, kila maamuzi ni mpaka Mama akubali atajiona kama hajakuoa wewe kamuoa Mama yako.

(3) Kuelezea Utamu Wa Mume Wako Kwa Rafiki Zako;
Hawa watakuibia na sisi wanaume kwakua hatujivungi, ukikaribishwa chakula cha bure unakula tu, hivyo acha kabisa ushakua mtu mzima kufikishwa kileleni ndiyo nini! Unafikiri wao hawataki? Mnaharibu ndoa zenu kwakua hamuishi kuwasifia hao waume zenu, tena wengine hata kwa sifa za uongo. Sasa wanaume wazuri wanaojali ni washida hivyo shoga yako akisikia unaye atasema hata mimi nilikua namtafuta huyo huyo na atamchukua bila hata kupepesa macho.

(4) Acha Kwenda Kulia Shida Kwenu;
Kila shida unayopata kwenu, kumuambia Mama, yaani mume hata hajasema siwezi, hajakutuma au ni kitu cha kununua kakuambia hana hela umeshaenda kulia lia kwenu kwakua wana uwezo. Hapo utamfanya mumeo asijihisi kama mwanaume na atatafuta tu mwanamke wa kumfanya ajihisi mwanaume.

Acha huo ujinga, muache mume wako ajaribu kutatua mpaka ikishindikana na yeye akakuambia mke wangu hapa hili ni kubwa sana tukaombe msaada. Lakini kama kila kitu kidogo ni kwenda kwenu atakuchoka na kukukimbia kwani ataona kama yeye hana maamuzi, unamuona kama hawezi kutunza familia mpaka asaidiwe na wakwe.

(5) Kutumia Muda Mwingi Sana Na Marafiki Zako;
Umeolewa lakini kuna wale rafiki zako ambao bado wana danga unataka uendelee kutoka nao kila siku, kuwakaribisha nyumbani kwakua hawana kazi wanakuja na kukaa tu, asubuhi jioni mume akirudi anawakuta.

Jingine huwaingiza mpaka chumbani, mnavaliana na nguo, yaani mke wa mtu unavaliana nguo na mwanamke mwingine! Wewe moja kwa moja hujajua maana ya ndoa ni nini? Umeolewa ni lazima ujiheshimu, sisemi uwatenge hapana, mbakie marafiki lakini kuwe na mipaka, wewe waendekeze tu kuna mawili, mume atawagonga au atachoka tabia zao atawachukia na kukuchukia na wewe.

Rafiki zako wanapaswa kuishi sebuleni kwako na kamwe wasikanyage chumbani!
 
Poooovu hili njoeni mchote mkafulie hizo tabia zenu zitakate mkawe wasafi kwa waume zenu.
 
Shosti hiyo ya Pili nadhani mimi nna niko tofauti, Mama yangu ni rafiki yangu ndio msiri wangu,siwezi kumwambia kua nimefanya mapenzi na mumewangu leo ila jengine lolote langu atalijua, mfano account yangu,mali zangu tumenunua nini na mumewangu kumbuka yule ni mume na huyu ni mama,kwangu Mama daraja yake nyengine Baba yangu atayasikia kwa mama ila mama nilazima ajue chochote changu,ivi mfano ningetangulia mimi kufariki mali zangu unadhani mume angesema sijui mwanao amewacha nyumba yake hati zake hizi hapa? lakini kama anajua inakua sio tabu kwake na kwa wanangu pia..
 
Iko Powa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulitafuta ukiwa mwenyewe au kwenye ndoa tayari?? Iweje kama ulitafuta hizo mali ukiwa kwenye ndoa useme ni vyako na si vyenu na mumeo?? Mali ni zako au za familia kwamba ukiondoka/fariki hazistahili kutumiwa na mumeo au wanao??
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom