Mambo manne ambayo lazima yatakutokea maishani mwako

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
3,186
8,212
Binadamu ni mwingi wa lawama sana kwa watu wengine ambao anaona wamekosea lakini ni vigumu sana kwa mtu kujua wapi anapowakoseaa wengine.

Kwa kulitambua hilo katika saikolojia kuna neno Fundamental attribution of error ambapo ni kanuni inaelezea kuwa watu wakitukosea huwa tunawalaumu,kuwachukia.

Lakini makosa hayo hayo tukifanya sisi huwa tunasema tumekosa kwa sababu mbalimbali kama vile Bahati mbaya, ajali,sababu zilizopo nje ya uwezo n.k.

Ukimkosea mtu utakuwa na kisingizio cha kumkosea ila watu wakikukosea huamini visingizio vyao.

Utamchukia mtu yeyote yule kama utamsema vibaya sana kwa dosari za maumbile yake na kutaja tabia zake mbaya ambazo huzipendi.

Kila mtu unaemchukia ni kwa sababu 2 ya kwanza umeanza kumsema kwa ubaya wa sura,rangi, muonekano, lafudhi,kabila sababu ya pili unamchukia kwa sababu ya ubaya wa tabia zake aambazo tabia ni mjumuisho wa mawazo,matendo,fikra zake,hisia zake na imani yake.

Endapo hautamchukia mtu kwa muonekano wake au tabia zake utakuwa umeondoka kwenye mtego ambao watu wengi wamefungwa.

Ili ujichukie wewe mwenyewe ni pale utakapochukia muonekano wako na maisha yako.

Ambapo maisha yako ni pamoja na matendo ya watu wengine juu yako, matokeo unayopata katika harakati za maisha yako,kufeli, kukataliwa,watu kukusema tofauti na kukosolewa.

Vitu vinne ambavyo usipojua kuvikabili utaishi kwa huzuni kama watu wengi ni.

1.KUFELI HUWEZI KUEPUKA
Unaweza kufaulu shule mitihani yote na utasifika kuwa genius LAKINI katika maisha yako kufeli lazima tu.
Kila aliyefanikiwa amefeli sana katika mipango yake.

Ili usifeli acha kujaribu chochote,haya ni maisha sio movie hivyo maisha huwa yanakuja tofauti na matarajio yako.

Kubali matokeo ya maisha hata kama hujayapenda kwa sababu kujichukia kwa sababu mipango yako imefeli ni adhabu unajipa kwa kosa hujafanya.

Chochote utakacho fanya kipo ndani ya uwezo wako mwanzo ila ukishafanya matokeo yanakuwa nje ya uwezo wako.

2.WATU WATAKUSEMA TOFAUTI
Haijalishi utakuwa mnyenyekevu kiasi gani huwezi kuzuia watu kuwa na mtazamo hasi juu yako

Hao wanaokusema vibaya hata wao pia husema vibaya,hao wanaokukosoa pia hukosolewa,hao wanaokulaumu pia hulaumiwa,hao wanaoziona dosari zako pia watu wengine huziona dosari zao.

Haijalishi utakuwa bingwa kiasi gani huwezi kufanya kila mtu akutazame kwa jicho sawa.

Wapo watakuona mchamungu hata kama wewe ni muovu pia wapo watakuona muovu hata ukiwa mchamungu

Mtu kama hakuamini haijalishi utajitetea kiasi gani hawezi kukuamini bali atatafuta dosari za utetezi wako ili kukutoa dosari.

Kila mmoja anazo sehemu 2 za tabia zipo sehemu ya tabia nzuri na tabia mbaya

Hata kama mtu atasifika kwa tabia nzuri zipo sehemu za tabia mbaya hata kama huzijui

Hakuna mtu mzuri kwa 100% wala hakuna mtu mbaya kwa 100%

Haijalishi upo na tabia nzuri sana lakini ipo sehemu unatambulika kwa tabia mbaya

Kila mmoja wetu anazo tabia mbaya kwa baadhi ya watu .

Hata kama utakuwa mwema kiasi gani bado kuna mtu atakutambua kwa mabaya yako tu.

Wapo huona mabaya yako tu hata ufanye mazuri kiasi gani pia wapo huona mazuri yako hata ukifanya mabaya kiasi gani

Utamchukia mtu endapo utafikiria sana mabaya yake na utampenda mtu sana kama utafikiria mazuri yake lakini hakuna mtu duniani mwenye mazuri pekee

Ukiona mtu anakusifia kwa kila tendo huyo anakupoteza kwa sababu kama binadamu lazima utakuwa unakosea tu kwa kujua au kutokujua

3.HUWEZI KUZUIA KUKATALIWA
Kuna mtu utakuwa umemuomba msaada lakini amekukatalia.

Kisaikolojia mtu unaempenda akikukatalia huwa unapata maumivu sawa na kupigwa na kitu mwilini.

Ndio sababu watu wenye upendo wa dhati huwa wanasema mapenzi yanauma.

Unaumia kwenye mahusiano kwa sababu ya upendo wako na matarajio yako makubwa kwa mwenzio unayoweka

Ukweli ni kuwa hakuna binadamu anaweza KUKUTIMIZIA matarajio yako yote kwa 100% hivyo kama unatarajia mtu akupe furaha hawezi kukupa furaha kwa

"No expectations no disappointment"

Hao wanaokukatalia pia hukataliwa,hao wasiojibu sms zako pia sms zao huwa hazijibiwi kwa wengine

Utakataliwa tu na hakuna kinga ya kuzuia hilo labda usiombe chochote kutoka kwa mtu yeyote.

4.KUKOSOLEWA NI KAWAIDA
Kila mtu ni bingwa wa kuona tabia mbaya za mwengine ambazo hazifai lakini hakuna ambaye anaona ubaya wa tabia zake kwa wengine

80% ya mazungumzo ya watu huwa ni kulalamika sana juu ya ubaya wa matendo ya wengine na kulaumu matokeo ambayo hayakuwa chagua lao

Kila mtu anatafuta mwenza sahihi wa maisha lakini hakuna anaethubutu kuwa mwenza sahihi kwa .wengine

Kila mmoja anajua tabia za mwengine ambazo hazifai lakini hakuna anayejua tabia zake mbaya ambazo hazifai

Ukiona mtu ni bingwa wa kutaja mabaya ya wengine hivyohivyo ndiyo hutaka mabaya yako kwa wengine pale unapoondoka

Wapo huona ubaya kwenye uzuri na pia wapo huona uzuri kwenye ubaya .

Wapo huwa mabingwa wa kukuonyesha nini hakipo sawa lakini hawana uwezo wa kukwambia nini kipo sawa.

Kama hutafinza namna ya kupokea maoni mabaya ya watu juu yako au katika kazi zako lazima utakata tamaa.

Mtu mwenye hasira hawezi kukosoa kazi zako kwa lugha nzuri hivyo elewa watu vile walivyo sio vile unavyowaona.

Mtu atakusema kwa mabaya kwa sababu anajisikia vibaya wakati huo na mtu atakusema kwa mazuri akiwa anajisikia vizuri kwa wakati huo

Usitarajie maoni mazuri kwa mtu ambaye amechanganyikiwa,mtu mwenye wivu,mtu mwenye kukuchukia,mtu asiejipenda,mtu mwenye lawama sana.

Watu watakusifia wakiwa na furaha na watakulaumu wakiwaa na huzuni

Ndio sababu watu watasema binadamu hafadhiliki lakini ukweli ni kuwa binadamu huongozwa kwa hisia hivyo hisia zake zikibadilika na maoni yake hubadilika

Unaweza kupost picha leo rafiki yako atakusifia sana kwa picha hiyo ipost picha hiyohiyo kila kila siku kwa mwezi mmoja utaona hasifii tena ile picha bali atasema huna picha nyingine upost
Tatizo sio picha bali hisia zake juu ya picha zimebadilika

Mtu anaweza leo kukusifia kesho atakukosoa na kukashifu sana kazi zako usipojua kuwa kilichofanya akosoe kazi zako ni hisia zake utaanza kusema binadamu vigeugeu

Ukweli ni kuwa hakuna binadamu anaeweza kukusifia kila siku saa zote kwa nyakati zote kwa sababu hisia za binadamu hubadilika vilevile tarajia maoni yao kubadilika
 
Ahsante sana ..nimejifunza kitu kikubwa mno ndugu yangu
 
Back
Top Bottom