Mambo machungu muhimu unayotakiwa kuyajua na kuyahimili ili uiweze ndoa

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
11,161
15,836
Kabla ya yote zingatia haya mambo machache

Hakikisha unachagua mwanamke aliye na maradhi yako(unavyovipenda)kwa maana yule mwenye umbile unalopenda wewe.

Kama unapenda chura tafute mwenye chura na rangi uipendayo wewe, huyu akiwa ndani naam hata mkigombana utataka muyamalize ili usijemkosa.

Angalia sana usije kuoa mwanamke ambaye tayari anampenda mtu mwingine, kubali kuwa FBI kwa muda ili usijekuwa wewe ni kaka wa mkeo na mume wa mkeo yupo nje. Chunguza

Hakikisha unaoa mwanamke wa style yako, kama dini muendane, ama laa basi kila mmoja wenu akubali kujifunza kioya cha mwenzie.

Baada ya hayo tuangalie baadhi ya mambo machungu kwenye ndoa hata kama ukampata mwanamke wa type yako

1. Ndoa ni tamu mno mwanzoni mwake kama utamu wa mlo unapouanza ukiwa na njaa kali.

Unapozidi kukila chakula hicho unaona kawaida na hatimae unaanza kuona kumbe chumvi haikutokea vizuri na chakula ni cha kawaida tu.

2. Kadri siku zinavyozidi lazima hisia za mapenzi baina yenu zitapungua mpaka mkae muda mwingi au muongezeane vichochezi vya hamasa.
Hili tambua

3. Mwanzo mkioana mnakuwa wanandoa ila kadri mnavyozidi kuishi na kuzoeana mnakuwa marafiki ambao mnaweza pita hata wiki nzima hamjafanya sex.

4. Mumeo au mkeo anaweza kuwa ni mtu ambaye hawezi kuomba tendo mpaka uanze wewe, hapa watu wanahisi mwenza hana hamu ya tendo la ndoa au ana mtu nje.

Hapa anza wewe kuomba na hili ulijue fika.

5. KUNA NYAKATI MWANAMKE ATAFANYA TENDO KUKURIDHISHA WEWE LAKINI YEYE HANA MOOD.

Kuna wakati atakupa wewe ili utoe hamu lakini yeye hajiskii so chukulia poa zipo siku anakuwa na mood.

6. Mkeo au mumeo lazima awe na katabia fulani kabaya usikokapenda ambako kana ugumu kurekebisha. Usimuache kwa hiyo sababu endelea nae.

7.bNdoa inataka uvumilivu kwa wote.kama sio mvumilivu huwezi ndoa, na uvumilivu unatakiwa wakati wa shida, kwenye raha hakuna uvumilivu ambao mtu utamshinda.

8. Kubali tu kuwa kuna wakati hautakuwa na hamu ya tendo na mkeo kwa sababu upo naye muda mwingi sana, usitafute mchepuko kwa sababu na huo utauchoka.

Kula sana karanga, korosho, pweza, maji mengi, juisi ya tende usikose japo kimoja wako kuongeza mavitu.

9. Kubali kuwa mkeo au mumeo ana privacy zake ambazo hapendi uzijue (mbali na kuchepuka) so usimdukue dukue kuepusha migongano.

10. Kubali tu kuwa lazima utawaona wenye kuvutia zaidi ya mumeo au mkeo huko nje.

Hii isiwe sababu ya kumsahau na kumsaliti mwenza wako kwa sababu wazuri hawaishi. Kubali wapite rudi kwa mwenza wako maisha yasonge.

We oa mwanamke mzuri kiasi gani, olewa na HB namna gani ila bado utawaona zaidi yake.

11. Kubali tu kuwa mmoja wenu atatangulia kufa au wote mtakufa, so akifa mwenzako isijitie hasira na kusema hutooa tena no. Tulia tafuta mwingine maisha yaendelee.

12. Watoto wanapunguza concentration ya mke kwa mumewe, usitake akutreat akiwa nanunu iwe sawa na kukutreat enzi zile take easy.

Kwa machache tusikate tamaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom