Mambo machache tu kati ya mengi yaliyoipelekea ccm kuwa chama cha upinzani karatu.

Gwallo

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
3,200
3,761
Mambo machache tu kati ya mengi yaliyoipelekeaa ccm kuwa chama cha upinzani karatu.

1.Mwaka 1995-2000 kipindi cha kwanza cha Dr.Slaa alifanya kazi yake katika mazingira magumu kwani viongozi wote wa vijiji walikuwa wameonywa kutoshirikiana naye.

2.Dr.Slaa bila kukosea alitumia mwanya huo wa chuki ya serikali ya ccm dhidi yake kuwafungua ufahamu wananchi kuwa wanaweza kupata maendeleo ktk maeneo yao bila ccm.Mpango ukaanza mara mora moja kuchimba mitaro ya kuweka bomba.

3.Dr.Slaa alianza kampeni yake ya kupunguza kodi ya kichwa cha mtu kutoka 5000 hadi 2500.Jambo ambalo lilipingwa na serikali ya ccm na kodi iliposhushwa na kuwa 2500 Halmashauri ya Wilaya Karatu ikapata mapato makubwa ambayo hayajawahi kufikiwa hapo kwanza ktk kipindi chote cha Mbuge wa ccm.Kulikuwapo na kodi za ajabu sana ng'ombe,Mbuzi, Kondoo na baiskeli zikafutwa zote hizo.

4.Dr. Slaa pia alianza kupanga mbinu ya namna gani ataweza kupata madiwani wa kutosha kuunda Halmashauri ya Wilaya,katika mikutano yake yote aliwasisitizia wananchi wake kutofanya makosa ktk uchaguzi wa mwaka 2000 na kumpatia madiwa wa kutosha na kweli wananchi wa karatu waliweka usikivu mkubwa na kumuunga mkono Mbuge wao ktk harakati zake hizo ambazo alianza kuona wananchi wameitikia wito wake na kuchagua viongozi wa Chadema katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi september 1999.Mfano huo ni kijiji changu mwenyekiti na serikali yake ni chadema isipokuwa mtu moja kati yao ni ccm.

Jambo ambalo sintasahau lilitokea ktk mkutano wa Dr. Slaa na wanakijiji.

Mwaka 2000 June ikiwa imebakia miezi minne kabla ya kufanya uchaguzi mkuu. Dr.Slaa alifika ktk Kjiji cha Bassodawish akiwa na lengo la kuwafahamsha wananchi namna ya kupata msaada wa mahindi maana mwaka huo watu hawakupata mazao kabisa,kama kawaida ya ccm ikampangia afanye mkutano wake karibu na Jengo kubwa Ghala la kuhifadhia mazao ambayo liko mita 25 toka mashine ya kusaga inayotumia diesel. Aliposimama tu Dr.Slaa kutoa maelekezo mara mashine ikawashwa ikawa imepunguza usikivu kwa kuwa eneo limetawaliwa na kelele za mashine, mara akasimama mtu moja na kumtaka Dr.Slaa na wananchi waende kufanyia kikao kwenye miti iliyokuwa mbelel ya ofisi ya ccm ambayo iko umbali wa kama mita 100 toka mashine ya kusaga ilipo. Tukahama na meza na viti vya mheshimiwa Mbuge. Kikao kilipoanza tu akatokea katibu mwenezi wa ccm wa kijiji na kuvuruga mkutano, akidai nani aliyewaruhusu mfanyie mkutano hapa n.k Huwezi amini alivyosogelea ile meza baada ya dakika moja tukashindwa kutambua kati ya yeye na vumbi huku fimbo za kutosha zikiwa zimemwangukia sehemu mbalimbali za mwili wake na Dr.Slaa aliingilia kati na kuamua ule ugomvi huku akisisitiza kuwa huyu katibu mwenezi ni mtu mdogo sana lakini ujasiri huu ameupata wapi akalinagnisha wale wote waliokuwa wanamwadhibisha katibu yule na stoy hii.

wewe unaogo mtoni umevua nguo zako mara akatokea kichaa na akaondoka na nguo zako,wewe ukaanza kumkimbiza!! Je Mtu wa kwanza kuwaona mkikimbizana atamdhania nani kati yenu kuwa ndiye kichaa??????

Kikao kikaisha watu wakaelewa namna ya kupata msaada wa mahindi na ccm kikaendelea kulaaniwa pale kijijini kwa tukio hilo lakipumabvu la katibu mwenezi. Miezi mitatu baadaye Dr.Slaa akarudi lakini yaliyotokea tena afadhali ya hayo niliyosimulia hapo ju. Mkasa huu nitakuletea siku nyingine!!!!!!!!!!!!

Kwa hiyo hakuna namna ya kuilezea ccm kijijini kwangu watu wakakuelewa kwa hiyo basi ni jukumu letu sisi kulitokomeza hiki chama (ccm)na inawezekana. Wana JF mnaokithamini CHADEMA HAYA YANAWEZEKANA na iko siku tutaondoka nalo ila tuanze mkakati sasa hivi tusisubiri 2015.

Sorry for the very long story!!!!!!!! I apologize.
 
Back
Top Bottom