"Mambo kwa soksi"

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
88,516
2,000
Hakika kifo cha mkongwe wa muziki nchini Dkt. Remmy Ongara kitakuwa kimewashtua watu wengi.

Leo hapa nimekuwa nikisikiliza nyimbo zake nyingi tu. Na katika pekua pekua yangu nikakutana na mkanda wa kaseti wenye wimbo wa "mambo kwa soksi" uliokuwa ukizungumzia matumizi ya kinga ya mipira ya kiume wakati wa kufanya mapenzi.

Wimbo huu ulipingwa sana hadi kufikia redio Tanzania kukataa kuupiga na kanda zake zikawa zinauzwa kinyemela kwenye soko la giza.

Sasa hivi matangazo ya kinga ya mipira yako kila sehemu. Iwe mabango, magazetini, redioni, kwenye tv, na sehemu nyingine nyingi.

Kwa maono yangu Dkt.Remmy aliona mbali sana kuliko hata watawala wetu wa wakati huo. Alichopingiwa enzi hizo ndicho kinachofanyika hivi sasa. Kweli mtu huhitaji shahada kuwa na busara.
 

SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,244
2,000
Huwa najiuliza ni kwa nini alinyimwa uraia wa Tz?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom