Nanyaro Ephata
JF-Expert Member
- Jan 22, 2011
- 1,221
- 1,788
Kwaheri 2020 karibu 2021
Awali ya yote tuna kila sababu ya Kumshukuru Mwenyenzi Mungu mwingi wa neema na Rehema.Mwaka 2020 umekuwa na changamoto lukuki,katika sekta zote,Kiuchumi,kiafya,kijamii na kisiasa.Lakini bado Mungu wetu ni mkuu sana!
Tunafahamu kuwa tuna ndugu,jamaa,marafiki ambao tulianza nao mwaka ila kwa sasa hawapo nasi.Sisi tulio baki tumebaki kwa kusudi la Mwenyenzi Mungu.Sharti tuishi kwa kusudi hilo,mwaka 2021 ukautazame kwa matumaini makubwa huku ukitenda matendo ya huruma,utu na yenye kumpendeza Mwenyenzi Mungu
Tunapoanza mwaka mpya 2021,ninakutakia Baraka za Mwenyenzi Mungu!usonge mbele kwa matumaini na imani kubwa ! lakini pia zingatia mambo haya 10 ambayo yatabadili maisha yako kabisa,yawe maisha ya furaha,upendo,amani,shukurani na ufanisi
Hizi kanuni 10 zitabadili maisha yako kabisa! Zipitie kisha uwe unazifanyia kazi kila siku kama vile ulivojizoesha ku brush meno/kinywa kila siku asubuhi baadae zitakuwa sehemu ya .maisha yako!
1.Orodhesha malengo.Hakikisha unakuwa na malengo yaliyoorodheshwa katika mpangilio unaotekelezeka! Usibuni orodhesha kile tu kinachotekelezeka!
2.Pangilia mapema.Kumbuka kila dakika unayotumia kupangilia itaokoa muda mwingi ambao ungeutumia kutekeleza kisichotekelezeka,hakikisha kila lengo linakuwa kwenye karatasi,fanya kazi kwa karatasi na kalamu daima
3.80/20 .Hakikisha unazingatia kanuni hii kuwa 20% ilete matokeo ya 80%.Yaani nguvu kubwa weka kwenye 20% ambayo italeta matokeo ya 80%
4.Fanya uchaguzi sahihi! Kwa kuwa huwezi kufanya kila kitu kwa wakati mmoja,jifunze kuweka malengo na vipaumbele,sharti vipaumbele viwe kwenye shughuli zinazoleta matokeo bora na sio bora matokeo
5.Kanuni ya Utatu.Tumia hii kanuni kwenye maisha yako yote,itakufanya uwe na muda wa kila jambo.Kanuni hii inataka 1.Fanya Uwezacho,kwa kutumia kile ulicho nacho,kwenye mahali ulipo!(usianze kulaaani kwa nini umezaliwa Tz au kwenye familia fulani au kwenye mjini fulani)
6.Tekeleza moja kwa 100%.Mshika mawili moja humponyoka,jitahidi kuhakikisha kuwa unatekeleza jambo moja kwa ukamilifu ili likupe changamoto ya kusonga mbele kwa ujasiri mkubwa
7.Fanya uchambuzi sahihi.Ukianza utekelezaji wa malengo yako chagua moja ambalo wewe ni mtaalamu wake,au moja ambalo umelitekeleza kwa umakini na weledi wa hali ya juu,kisha hili ndio liwe msingi wa kusonga mbele
8.Jipe motisha.Hakikisha unajimotisha wewe binafsi,tumia 80% ya muda wako kwenye mambo mazuri na 20% au pungufu kwenye matatizo,usiache matatizo yawe kansa kwako!
9.Usiwe mtumwa wa teknolojia. Teknolojia ni nzuri sana ila ifanye iwe mtumwa wako,wewe usiwe mtumwa wa teknolojia.Jifunze muda wa kufanya simu/laptop/tv etc na muda wa kufanya mengine(kuna watu wanaangalia TV anafuatilia tamthilia ya kifilipino hadi analala kwenye kiti)kila jambo lifanyike kwa kiasi,wengine simu hata akienda ibadani yupo busy na simu,huu ni utumwa,fanya ziwe vitendea kazi vyako na wewe uwe juu!
10. Tengeneza jedwali la Maksi.Hakikisha unakuwa na jedwali la maksi ili uzipe maksi kazi/malengo na jinsi ambavo umetekeleza kwa kila lengo na mpango wake.Hili jedwali litakusaidia kujua wapi una nguvu na wapi ni dhaifu,wapi uboreshe,wapi uongezee bidi……………..
Nawatakia nyote Baraka za Mwenyenzi Mungu mwaka huu 2021
Nanyaro EJ