Mambo kumi usiyoyajua kuhusu dr. Slaa........... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo kumi usiyoyajua kuhusu dr. Slaa...........

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by RONALD URASSA, Oct 12, 2010.

 1. R

  RONALD URASSA Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mambo Kumi Muhimu Kuhusu Dk Willibrod
  Peter Slaa
  2
  Dk Willibrod Peter SLAA
  1. Anachokisimamia
   Dk Slaa anasimamia maadili, uadilifu, uamakini na uwajibikaji katika
  uongozi wa nchi na utendaji serikalini.
   Dk. Slaa anaamini kuwa Watanzania wanaweza kuleta mabadiliko
  wanayoyataka wakipata uongozi bora na thabiti.
  2. Kuzaliwa, elimu ya msingi na sekondari
  Dk Slaa alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1948 katika Wilaya ya Karatu. Alipata elimu ya
  msingi katika shule za Karatu na Kwermusi (Mbulu) kati ya mwaka 1958 na 1965.
  Alisoma elimu ya sekondari katika Shule za Dung’unyi Seminari na Itega Seminari
  kati ya mwaka 1966 na 1971.
  3. Mafanikio ya Dk Slaa Kielimu na Kitaaluma
  Dk Slaa ana shahada na stashahada zifuatazo
   Shahada ya Uzamivu (PhD ) katika Sheria ya kanisa kutoka Chuo Kikuu cha
  St. Urban, Rome
   Stashahada ya Theolojia kutoka Kipalapala Seminari
   Stashahada ya falsafa kutoka Kibosho Seminari
   Stashahada ya Afya ya Macho kutoka Kituo cha Kimataifa cha Macho
  4. Mafanikio ya Dk Slaa Kikazi na Kitaalamu
  Dk Slaa amefanya kazi katika maeneo na sehemu mbalimbali. Baadhi ya nyadhifa
  alizoshika na kazi alizofanya ni hizi zifuatazo:
   Mkurugenzi Mtendaji, Chama cha Wasioona Tanzania, 1992-1998
   Katibu Mkuu, Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), 1985-1991
   Mkurugenzi wa Maendeleo (Jimbo Katoliki la Mbulu), 1977-1979 na 1982-
  1985.
   Padri wa Kanisa ikatoliki kuanzia 1977 hadi 1991.
  5. Vitabu alivyoandika
   Utimilifu wa Msichana (1977)
   Utimilifu wa Mvulana (1977)
   Expediency and exigency Liturgical Legislation (1981)
  3
  6. Ufasaha katika lugha nane (8)

  Dk Slaa anajua kuzungumza na kuandika lugha nane za kimataifa zifuatazo:
  Kiswahili, Kiingereza, Kilatini, Kiitaliano, Kijerumani, Kihispania, Kireno na Kifaransa.
  7. Uzoefu wa Dk Slaa Kisiasa
  Dk Slaa ana uzoefu wa muda mrefu katika shughuli za kisiasa. Baadhi ya nyadhifa
  alizoshika ni hizi zifuatazo:
   Mbunge wa Karatu kwa miaka 15, kutoka 1995 hadi 2010
   Katibu Mkuu wa CHADEMA, 2002 hadi sasa
   Makamu Mwenyekiti Taifa wa CHADEMA, 1998-2002
   Mjumbe wa Kamati Kuu na Baraza Kuu wa CHADEMA kutoka 1995 hadi sasa
  8. Uzoefu wa Dk Slaa Kitaifa na Kimataifa
  Dk Slaa ana uzoefu mbalimbali kitaifa na kimataifa kama ifuatavyo
   Mjumbe wa kuwakilisha Bunge la Tanzania katika Bunge la Afrika, Carribean
  na Pacific-EU (ACP-EUC Joint Assembly), 1996-2000
   Mjumbe Kamati ya Uongozi (ACP-EU Joint Assembly)
   Mjumbe katika Bunge la SADC kutoka 1998 hadi 2010
   Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la SADC (Inter Parliamentary
  Cooperation and Capacity Building Committee) kutoka 1998 hadi 2010
   Naibu Kiongozi wa Kamati ya Upinzani Bungeni, 2006-2010
   Mwenyekiti, Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Bunge la Tanzania,
  2008-2010
  9. Mafanikio kisiasa na kiutendaji
   Dk Slaa amekuwa mbunge wa Karatu kwa miaka 15 mfululizo. Karatu ni moja ya
  wilaya hapa nchini zenye mafanikio makubwa ikiwemo miundo mbinu bora, maji
  na huduma nyingine za kijamii. Dr. Slaa anataka kutumia uzoefu wake wa miaka
  15 ya ubunge wa Karatu kwa ajili ya taifa zima.
   Ndiye Katibu Mkuu aliyefanikiwa zaidi kuijenga CHADEMA. Kwa kushirikiana na
  viongozi wengine ameweza kuipitisha CHADEMA katika changamoto mbalimbali
  na kukifanya kuwa chama kilicho tayari kushika uongozi wa taifa.
   Bila kujali vitisho vya watawala aliibua rasmi kashfa za ufisadi mbaya kuliko zote
  zilizowahi kutokea hapa nchini zikihusisha wizi wa fedha za umma katika Benki
  Kuu. Madai yake mazito Bungeni yalimlazimisha aliyekuwa Gavana wa Benki
  Kuu nchini kutoroka nchini.
  4
  10. Baadhi ya vipaumbele vya Serikali itakayoundwa na Dk Slaa

   Kuanzisha mchakato wa kuandika upya Katiba ndani ya siku 100 baada
  ya kuunda serikali
   Kupambana na kuwashughulia mafisadi katika nafasi zote, ikiwa ni
  pamoja na kuhakikisha fedha zote zilizoibwa zinarejeshwa na wahusika
  wanashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
   Kuhakikisha kuwa kilimo chetu kiwe bora na cha kisasa, chenye faida
  na kinachofikia viwango vya kimataifa katika kuvuna, kuhifadhi, kusafirisha
  na kuuza mazao mbalimbali.
   Kuhakikisha kuwa kila mtoto wa kitanzania anapata elimu bora katika
  ngazi zote.
   Kuanzisha utaratibu wa kuwalipa pensheni wazee wote wenye umri wa
  miaka 60 na kuendelea nchi nzima na kurekebisha mfumo wa malipo ya
  pensheni kwa wastaafu
   Kuanzisha utaratibu mpya wa upandaji mishahara kwa watumishi wa
  umma na wa sekta binafsi utakaohakikisha kuwa mishahara inapanda
  kadri gharama za maisha na mfumuko wa bei unavyopanda.
  Chagua Mabadiliko,
  Mchague Dk Slaa ili arudishe tunu za taifa letu:
  Uzalendo, Maadili, Uadilifu na Umakini.
   
 2. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  sifa toshelezii kwa kiongozii wa kuikomboaa tanzaniaa kuondokana na umaskini wa kulazimishwaa..hongera dr slaa kwa uzoefu na maadili bora.
   
 3. NAWAPASULIA

  NAWAPASULIA Member

  #3
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaelekea hujui kuwa Dr slaa alipata phd ya canon laws(sheria za kanisa)?.........hujui kuwa anapaswa kuwa hakimu wa mahakama za kanisa?.................yaelekea hujui kuwa alisoma na askofu Gorg Muller wa Norway ambaye amejiuzulu kwa kulawiti watoto na walisoma wote pale Trust Tutorial College London mwaka 1985 na walikaa chumba kimoja?..........vilevile hujui kuwa Dr slaa ana mtoto anayesoma chuo kikuu cha Dodoma ambaye ni matokeo ya padre huyo kumpachika mimba mpishi wa Mbulu seminari mwaka 1987 wakati akiwa padre?..........pia yaelekea hujui kuwa Dr slaa amedhulumu milioni 800 kati ya bilioni mbili na nusu ambazo chama cha conservative cha uingereza walitoa kama msaada kwa CHADEMA?...........................NAFIKIRI UNAPASWA KUYAONGEZEA NA HAYA ILI WATANZANIA WAMJUE VIZURI DK SLAA ILI WAWEZE KUFANYA UAMUZI SAHIHI PALE OKTOBA 31
   
 4. M

  MathewMssw Member

  #4
  Oct 12, 2010
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Karibu Rais Dr Slaa!
   
 5. p

  pierre JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  DR.SLAA nimekukubali,watanzania wenzangu tusisubiri Mungu ashuke kutoka juu ndio tukubali,hii kweli ni tunu ya Taifa ni zawadi Mungu aliyotuandalia Watanzania baada ya kilio chetu cha muda mrefu.

  TUMPENI KURA ZETU DR. SLAA KUWA RAIS 2010.
   
 6. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Anafaa. Atakuwa hakimu kwa mafisadi maana atadiriki kufanya maamuzi magumu kuhusu mikataba mibovu ya madini, Ufisadi na mipango mibovu ya kudhoofisha elimu nchini tanzania kuhakikisha kila mtoto wa kitanzania anasoma kwa kadiri ya uwezo wake bila kikwazo cha ada
   
 7. M

  MathewMssw Member

  #7
  Oct 12, 2010
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakufananisha na Fisadi nanihii vile!
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,819
  Trophy Points: 280
   
 9. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  peeeeopleeeeeeeeeeeeezzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz........!!
   
 10. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #10
  Oct 12, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwa nini aliacha upadre?
   
 11. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  aliamua kubadili kazi. period
   
 12. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Sasa kusoma chuo na kukaa chumba kimoja vina uhusiano gani? kwani wewe ukisoma na mtoto wa fisadi nawe ni fisadi? sasa kwa kuwa baadhi ya Watanzania wenzetu ni mafisadi na sisi wote ni mafisadi? naona wewe unahasira na wachukia ufisadi. Sasa tukiamua kuweka wazi Kesi ya Babu Seya mtapona? Ingekuwa ulichokiandika ni kweli jamaa zako wa CCM wangekwishaeleza siku nyingi. Nyerere alishasema "Ukiona kajamaa kanatumia vijipesapesa kwenda ikulu ni ka kuogopa kama UKOMA" Hivi wewe ni MTanzania gani usiye na uchungu na wenzako? Labda wewe ni kipofu huoni wananchi wanavyotaabika.
   
 13. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  Ntakupa kura yangu slaa
   
 14. D

  Dawa ya Mjinga JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 382
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ni ukweli kuwa kama mimi na wewe tulivyo na hiari ya kubadilisha kazi padre naye kadhalika. Kuna makala naiambatanisha hapa chini ikieleza zadi kuhusu upandre.

  ========================================================
  [FONT=&quot]Kwa nini hofu ya upadre wa Dk. Slaa haina msingi[/FONT]
  [FONT=&quot][​IMG][/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Lula wa Ndali-Mwananzela[/FONT]
  [FONT=&quot]Septemba 1, 2010[/FONT]
  [FONT=&quot][​IMG][/FONT][FONT=&quot][/FONT]​
  [FONT=&quot]KWA muda mrefu sasa vyombo kadhaa mbalimbali vya habari na watu binafsi vimekuwa vikieneza habari kuwa Dk. Wilibroad Slaa ni Padre wa Kanisa Katoliki na kuwa kwa vile aliwahi kuwa Padre (kuhani) ndani ya Kanisa hilo ina maana kuwa hadi leo hii yeye ni padre kama walivyo mapadre wengine. [/FONT]
  [FONT=&quot]Kutokana na madai hayo ya kuwa Dk. Slaa bado ni padre hivyo hastahili kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wengi wanaosema mambo haya wanaonyesha kutokujua mafundisho ya Kanisa Katoliki juu ya upadre na jinsi gani mtu anaweza kuwa padre na akauacha na kuwa mlei kama walei wengine. [/FONT]
  [FONT=&quot]Kanisa Katoliki linazo Sakramenti saba ambazo ni Ubatizo, Kipaimara, Komunio (Ekaristia), Upatanisho (Maungamo), Ndoa, Upadrisho (Ukuhani) na Mpako wa Wagonjwa. [/FONT]
  [FONT=&quot]Sakramenti hizo saba zipo ambazo zinatolewa mara moja tu kwa mtu na nyingine ambazo zaweza kurudiwa. Tunaposema "kutolewa mara moja" maana yake ni kuwa mtu anapopatiwa uwezo na nguvu za kuanza kupokea neema za sakramenti hizo hilo hufanywa mara moja tu na hairudiwi tena (isipokuwa kama hakuna uhakika kuwa alishapokea mara hiyo ya kwanza). Hizi ni Ubatizo, Kipaimara na Upadrisho. [/FONT]
  [FONT=&quot]Nyingine ni zile ambazo mtu anapokea mara ya kwanza lakini katika maisha yake ya kila siku anarudia kupokea mara kwa mara kwa kadiri inavyohitajika. Hizi ni Ekaristia na Maungamamo japo nazo huanza kupewa mara moja tu na kutoka hapo ni kuendelea kuchota neema zake kwa taribu zinazotakiwa. Na zipo ambazo hufanywa upya kabisa kama vile hazijawahi kufanywa kabisa; hizi ni ndoa na mpako wa wagonjwa.

  Si kusudio langu kuelezea theolojia ya sakramenti hizo ila nataka kuzungumzia hili ambalo linaonekana kuwashinda watu kuelewa. Jambo hili kwa wengine wanalipa ugumu usiostahili kwani unahitaji kukaa chini kwa sekunde chache tu kuelewesha na wewe mwenyewe ukajikuta unapata ule wasaa wa kusema “aha! Nimekuelewa”. Hata hivyo, natarajia kutokueleweka kwa baadhi ya watu kwa sababu aidha ni wagumu mno kuelewa au wana wepesi wa kusahau.[/FONT]

  [FONT=&quot]Ni kweli Dk. Slaa alipewa Sakramenti ya Upadrisho ndani ya Kanisa Katoliki baada ya kumaliza maandalizi yake ya kazi hiyo. Upadre si kama kazi nyingine ambazo mtu "anasomea"; si sawa na udaktari, uwakili au uhasibu. Upadre ni Sakramenti ya Ukuhani ambayo mtu anaandaliwa kuiingia na kuitumikia. Ndiyo maana kimsingi kabisa, hata mtu ambaye hajasomea kabisa mambo ya theolojia na falsafa anaweza akapewa Upadrisho endapo haja kama hiyo inatokea. [/FONT]
  [FONT=&quot]Lakini kwa miaka mia nyingi Makanisa (Mashariki na Magharibi) yamekuwa yakiwaandaa wale wanaotaka kuingia katika "Daraja Takatifu" kwa mafunzo maalumu ya mambo ya dini, falsafa, utawala n.k Ukiondoa mafunzo ya Theolojia ya Katoliki mafunzo mengine ya falsafa, utawala, au elimu nyingine yoyote ni sawa kabisa na mafunzo yanayotolewa katika vyuo vikuu vingine.

  Mtu akishapata daraja ya Ushemasi wa Mpito (hatua ya kwanza kabla ya upadre) na baadaye Upadre basi anakuwa ni "Kuhani Milele kwa mfano wa Melkizedeki" na hakuna kitu chochote ambacho kinaweza kufanywa kuondoa daraja hilo. Hii huitwa "alama isiyofutika". Ni alama ile ile ambayo inapatikana katika Sakramenti ya Ubatizo na Kipaimara ambapo mtu akishabatizwa ubatizo wake hauwezi kurudiwa tena kwani alama hiyo ya neema haifutiki. Kama vile wakristo wote waliobatizwa nao wanayo alama ya kudumu ya ukristo wao. Hata Mkatoliki anapoacha dini, kuhamia dhehebu jingine au kuhamia dini nyingine alama hii ya ubatizo haifutiki. [/FONT]

  [FONT=&quot]Kutokana na hilo Mkatoliki huyo akiamua kurudi kwenye Imani Katoliki basi habatizwi tena zaidi ya kuungamishwa Imani ya Mitume. Alama hii ya ubatizo si kwa Wakatoliki tu, Kanisa Katoliki linatambua kama ni halali ubatizo unaofanywa na madhehebu mengine ya kikristu (japo si yote) kama vile Waanglikana na Walutheri. [/FONT]
  [FONT=&quot]Ndiyo maana Wakatoliki, kwa mfano, wakimpokea Mkristu anayetoka Ulutheri au Anglikana ambaye amebatizwa huko hatobatizwa tena kwenye Ukatoliki atapokelea tu baada ya kukiri imani Katoliki.[/FONT]
  [FONT=&quot]Hili nalo ni kweli kwa mtu analiyepadrishwa. Alama yake ya upadrisho wake ni ya kudumu na hakuna kitu ambacho yeye au mtu mwingine anaweza kufanya kuifuta milele. Hata yeye mwenyewe hawezi kuifuta kwa kutoamini au kukana uwepo wa Mungu. Ni kwa sababu hiyo mtu ambaye ameshawahi kupata upadrisho ataendelea kuwa na alama hiyo milele. Hili ni fundisho ambalo ni msingi wa kuelewa padre ambaye bado anahudumu na padre ambaye ana alama ya kudumu. Mapadre wote wanayo alama hii ya kudumu lakini si wote wanaweza kuhudumu kama mapadre. [/FONT]
  [FONT=&quot]Kwa maana hiyo, Padre wa Kikatoliki anaweza kuacha, kufukuzwa, kuachishwa kazi za kila siku za kutoa huduma ya Upadre lakini bado anabakia kuwa ni padre moyoni. Hivyo, mtu huyo aliyeacha hastahili kuitwa "Padre X" kwa maana ya mapadre ambao bado wako kwenye huduma. Ni sawa na daktari aliyeacha kazi ya udaktari au kufukuzwa udaktari au uwakili lakini bado mafunzo na uwezo wa kutoa huduma hiyo akawa bado anao japo haruhusiwi tena kufanya hivyo. Wapo watu ambao kutokana na mazoea wataendelea kumuita "daktari" japo hafanyi tena huduma hiyo.[/FONT]
  [FONT=&quot]Jambo hili ni muhimu kulielewa. Mtu ambaye ameacha yeye mwenyewe upadre bila kurejeshewa hali yake ya ulei (yaani uumini wa kawaida) kwa mujibu wa taratibu za Kanisa basi mtu huyo bado ni padre na haruhusiwi kupewa Sakramenti ya Ndoa na anafungwa na vifungo vingi zaidi. [/FONT]
  [FONT=&quot]Hata hivyo, Kanisa Katoliki lina utaratibu wa kumfanya mtu aliyewahi kuwa padre kurejeshwa kwenye hali ya ulei (yaani kuondolewa kabisa kazi na haki ya kufanya kazi za upadre na kuwa muumini wa kawaida kabisa). Mtu ambaye ameondolewa upadre kwa utaratibu wa Kanisa (laicization –kufanywa mlei) na kibali cha Vatikani anaondolewa haki na majukumu yote ya mapadre wengine isipokuwa mambo mawili tu yaani useja (celibacy) na kusikiliza maungamo ya mtu aliyekaribu na kifo.

  Hilo la useja linahitaji kibali kingine kuondolewa ili aruhusiwe kuoa. Hata hivyo, kwa vile padre ni padre milele basi mtu aliyewahi kuwa padre anaweza kusikiliza maungamo na kutoa msamaha kwa mtu ambaye yuko katika hatari ya kifo tu. [/FONT]

  [FONT=&quot]Kwa mfano, wamesafiri mahali na gari limepinduka na hakuna msaada wa karibu na yupo mtu ambaye ni mkatoliki (au mtu mwingine mwenye imani hiyo ya maungamano) na akaomba kama kuna padre asikilize maungamano yake basi yule aliyekuwa padre anaweza kabisa kusikiliza maungamo hayo na kumpatia ondoleo la dhambi. Japo kama na yeye atanusurika kuna utaratibu wa kutoa taarifa kwa Askofu wa eneo hilo juu ya tukio hilo bila kutoa taarifa ya kilichoungamwa. Sasa basi, si ajabu kabisa kwa padre kufuata utaratibu na kurejeshewa hali yake ya ulei. Pindi hilo linapotokea basi padre huyo hupewa masharti yake mapya ya hali yake hiyo mpya ya jinsi gani aishi kama asiye padre. [/FONT]
  [FONT=&quot]Miongoni mwa mambo hayo ni kukatazwa kuvaa nguo yoyote ya kipadre (kama kola ya kirumi shingoni), kukatazwa kukaa katika eneo la kanisa, kunyimwa haki za matunzo atakapostaafu kama mapadre wengine, kukatazwa hata kuwa mhudumu wa komunio ndani ya kanisa ili isije kuwachanganya watu na wengine wanaopewa masharti ya kutofundisha elimu ya theolojia katika vyuo visivyo vya kikatoliki n.k Lengo ni kuhakikisha kuwa mtu huyo anabakia ni padre jina tu na si mhudumu.[/FONT]
  [FONT=&quot]Jambo kubwa, hata hivyo, ni kuwa watu wanachanganya masharti ya Sheria ya Kanisa yanayomkataza padre mhudumu kushiriki kugombea nafasi ya kisiasa. Sheria ya Kanisa namba 285 kwenye mojawapo ya sehemu zake ndogo inakataza kwa padre mhudumu kushiriki katika nafasi ya kuchaguliwa katika mambo ya siasa. Hivyo, paroko au paroko msaidizi mahali au padre mwingine yeyote ambaye bado yuko katika huduma haruhusiwi kugombea uchaguzi au nafasi ya kisiasa. [/FONT]
  [FONT=&quot]Hii kanuni hata hivyo haifuatwi wakati wote. Historia inao mapadre kadhaa ambao kutokana na matakwa yao wenyewe waliamua kushiriki katika nafasi za kisiasa wakati mwingine kinyume na maelekezo ya uongozi wa juu wa Kanisa (maaskofu wao au Vatican). Mwaka jana huko Ufilipino Padre Edd Panlilio alitamani kuwa Rais wa nchi hiyo mojawapo yenye Wakatoliki wengi duniani. Kwa vile alikuwa bado ni padre mhudumu sheria za Kanisa zilikataza yeye kufanya hivyo. Hata hivyo, alikuwa tayari kuomba kuruhusiwa kuwa mlei ili agombee nafasi hiyo. [/FONT]
  [FONT=&quot]Mfano mzuri wa kuelewa hili ni aliyekuwa Askofu Ferdando Lugo wa San Pedro huko Paraguay. Askofu Lugo alitaka kuingia katika siasa kitu ambacho kinakatazwa na Kanuni za Kanisa Katoliki. Askofu Lugo aliomba Kanisa Katoliki limruhusu arejee katika hali ya ulei ili aweze kushiriki katika siasa lakini Kanisa lilimkatalia, yeye aliendelea kugombea na aliposhinda uchaguzi Mkuu wa Paraguay Kanisa Katoliki lilikubali kumuondolea Upadre wake na kumrejesha katika Ulei. Hivyo, Rais wa sasa wa Paraguay ni Askofu wa zamani wa Kanisa Katoliki ambaye alirejeshwa katika ulei.

  Hii ina maana ya kwamba, Dk. Slaa si tu ni mlei lakini anayo haki kama wakatoliki wengine walei kushiriki katika nafasi ya uongozi kwani hajavunja sheria yoyote ya Kanisa, wala hajaenda nje ya haki zake za kikatiba. Dk. Slaa sasa hivi ni muumini Mlei kama wengine na atakapoamua kupata sakramenti nyingine yoyote ya Kanisa ataweza kufanya hivyo kwa uamuzi wake yeye mwenyewe kwani alifuata taratibu za Kanisa za kurejeshwa katika maisha ya mlei.

  Hivyo, Dk. Slaa si mtumishi wa Kanisa Katoliki na si padre kwa maana ya kuwa anahaki na majukumu yote ya mapadre wengine. Yeye ni muumini mlei ambaye kutokana na nafasi yake ya kuwa aliwahi kuwa padre anabakia na haki za waumini wengine walei ndani ya kanisa hilo na vile vile uwezo wa kusikiliza maungamano ya mtu aliye katika hatari ya kifo TU. [/FONT]

  [FONT=&quot]Hii ina maana ya kwamba Dk. Slaa anayo haki kama Mtanzania mwingine bila kujali dini yake au nafasi yake katika dini hiyo kugombea nafasi ya Urais. Hili ni muhimu kuelewa kuwa Katiba yetu haimkatazi hata padre mhudumu kugombea nafasi ya Urais au ubunge kama akitaka, makatazo hayo yako kwenye Kanisa na si kwenye Katiba yetu. Hivyo, hata kama leo akatokea padre, shehe, mchungaji n.k akataka kugombea nafasi yoyote ya ubunge basi anazo haki hizo. [/FONT]
  [FONT=&quot]Tayari tunajua wapo wasomi wengi tu wa dini zetu kubwa mbili ambao wamekwishakuingia bungeni. Dk. Slaa ameshakuwa Mbunge kwa vipindi vitatu. Wapo na wabunge wengine na hata katika nafasi nyingine za kisiasa za watu ambao wamewahi kushika elimu ya juu ya dini za Kikristu na Kiislamu na hatukuwahi kuona watu wanalalamika kuwa kwanini watu waliowahi kuwa wachungaji (au walio bado wachungaji), mashehe au walimu wa dini kuingia na kuchaguliwa kwenye siasa. Kama tunakubali kuwa watu hao wote wameweza kutimizwa matakwa ya Katiba yetu na tukawakubali kwa nini inapofika kwenye suala la Urais tuanze kutoa sababu zisizo na kichwa wala miguu? Hivi leo kama Kikwete angekuwa ni msomi wa dini ya Kiislamu au mtu aliyewahi kuwa shehe huko nyuma kweli tungeweza kwa haki kusema kuwa hilo peke yake linamfanya asistahili kuwa Rais wetu kama tunamkubali? [/FONT]
  [FONT=&quot]Lakini jambo la mwisho ambalo linaonekana kuwasumbua watu wengine na halihitaji maneno mengi kwa sababu hapo juu tayari nimeliashiria ni hofu ya baadhi ya watu kuwa ati Dk. Slaa kwa vile aliwahi kuwa padre basi akiingia madarakani atakuwa chini ya maelekezo ya Baraza la Maaskofu au Vatican yenyewe. Kwa vile nimekwishakusema hapo juu kuwa mtu akisharudishwa kwenye hali ya ulei hawi tena chini ya utawala, nidhamu au maelekezo ya askofu wake kama mapadre wengine kumbe Dk. Slaa hayuko chini ya Askofu wa Mbulu, Baraza la Maaskofu au Vatican kiutawala. Yuko kama Mkatoliki mwingine yoyote ambaye anaweza kwenda popote, kufanya biashara yoyote, kuishi popote na yeyote bila kulazimishwa kuulizwa au kutoa maelezo kwa mtu yeyote. [/FONT]
  [FONT=&quot]Hii ina maana ya kwamba hakuna mtu wa Baraza la Maaskofu ambaye anaweza kumuita Dk. Slaa ati ampatie maelezo au mtu ambaye anaweza kuingilia shughuli zake za kisiasa. Viongozi wa Kanisa wameachiwa eneo la kiroho tu kama ilivyo kwa wachungaji, mashehe, na viongozi wengine wa dini kwa imani ya waumini wao. Tukikubali kuwa ati kwa vile mtu amewahi kuwa Mkatoliki basi atapokea maelekezo toka kwa uongozi wa Kanisa kwenye mambo ya kisiasa ni lazima tukubali kuwa mtu wa dini nyingine au dhehebu jingine naye ataweza kuburuzwa na viongozi wake wa dini. [/FONT]
  [FONT=&quot]Hadi hivi sasa tunaweza kuona wazi kuwa mambo kadhaa ambayo Dk. Slaa ameyafanya au kuyasema hadharani nina uhakika baadhi ya viongozi wa dini wasingependa ayaseme jinsi hiyo au wangeweza hata kumkalisha chini. Dk. Slaa ameweza kujionyesha kuwa ni mtu wa kuthubutu, yuko huru na haangalii nyani usoni. Kama alivyozungumza siku chache zilizopita staili yake hiyo ya utawala inafahamika hata kwa mapadre na viongozi wengine wa Kanisa ambao aligongana nao wakati akiwa katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki. [/FONT]
  [FONT=&quot]Tanzania haimhitaji padre kuwa rais, Tanzania haihitaji mchumi kuwa Rais, Tanzania haihitaji daktari kuwa Rais, Tanzania haihitaji mwalimu kuwa Rais, na vile vile haihitaji shehe kuwa Rais. Hizo zote si sifa za kuwa Rais. Tanzania inahitaji Mtanzania mwenye kutimiza masharti ya Katiba kuwa Rais na awe ni mtu mwenye uwezo wa kutuongoza tunakotaka kwenda na ambaye atakuwa tayari kutupa uongozi bora tunaouhitaji kuelekea katika safari ya ujenzi mpya wa Taifa.[/FONT]
  [FONT=&quot]Kama hilo litamhusisha mtu aliyewahi kuwa mchumi, mkuu wa wilaya, waziri wa mambo ya nje au mtaalamu wa nyota na iwe! Lakini kama itamtaka mtu aliyewahi kuwa padre basi na iwe, kwani tukianza ubaguzi kwa sababu ya maisha ya kidini ambayo mtu amewahi kuyaishi, itakuwaje kwa wale ambao leo wanagombea na wamewahi kuwa waganga wa kienyeji au bado ni waganga wa kienyeji?[/FONT]
   
 15. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Hayo mbayo ya vyumbani kama tutayaeleza hapa nadhani hakuna atakayepona, na huenda JK akaathirika zaidi. Hilo la fedha ndugu yangu ni lazima uwe na uthibitisho wa kutosha. Itoshe tu kusema kuwa umefika wakati wa kujadili hoja na si mtu na maisha yake binafsi. Kama yale anayoahidi kuyasimamia unaona kuwa hayawezekani sema tu hivyo kistaarabu kuliko kupandisha kwa jazba. Hiyo haisaidii, na inakudhalilisha tu.
   
 16. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  NAjipasulia Umejipasulia, hadanganyiki mtu hapa. Go Slaa go.
   
Loading...