Uchaguzi 2020 Mambo Kumi niliyoyasikia leo kwa mara ya kwanza kuhusu Tanzania kutoka kwa Tundu Lissu akiwa Mbarali

Taso

JF-Expert Member
Jun 12, 2010
2,461
2,288
MOJA: Reli nyingine zilizopo na zenyewe ni standard gauge - TAZARA, RELI YA KATI, (DAR -KIGOMA) na ya TANGA-ARUSHA

MBILI: Marais wengine wote na wenyewe walianzisha mabwawa ya umeme, kuanzia Kidatu na Mtera (Nyerere), wengine wakajenga Kihansi (Morogoro - MKAPA), Hale (Tanga - NYERERE), Pangani (Tanga - MWINYI), Nyumba ya Mungu (Kilimanjaro - NYERERE), Rusumo (Kagera- KIKWETE), Songwe (Mbeya - KIKWETE)

TATU: Wakati wa uhuru kulikuwa na mbuga moja tu, ya Serengeti, iliyotengwa na Mkoloni. Nyingine zote zilianzishwa kwa amri za marais kwa kuhamisha watu, hizi za Magufuli wanahamisha wanyama, wanawapeleka Chato ambako naturally hakuna mbuga, hakuna wanyama. Na wanapounda mbuga mpya wanaingilia maeneo ya watu na hawawalipi fidia, wanasababisha maafa na migogoro ya ardhi. Anaijua migogoro yote ya mipaka ya hifadhi nchi hii, na ardhi za wananchi zilizopokwa bila fidia, kwa sababu alilifanyia utafiti katika kazi yake ya kwanza akitoka chuo.


NNE: Daktari muanzilishi wa Hospitali ya Masana Mbezi, Dar es Salaam, alikufa kwa pressure baada ya kukutwa na mashine alizonunua kwenye mnada wa vifaa chakavu, Muhimbili, akasahau kufuta zile alama za MUHIMBILI MKWAJU SERIKALI MKWAJU HOSP MKWAJU RUFAA MKWAJU SIFURI SIFURI MBILI MKWAJU.... Alifunguliwa kesi ya uhujumu uchumi isiyo na dhamana, akafa na pressure halafu wakakuta ni kweli alinunua Muhimbili.

TANO: Mbunge wa CCM, Salim Hassan Abdullah Turki, amekufa na pressure baada ya kubambikwa madai ya kodi ya mabilioni. Mheshimiwa Turki ndie aliyekodi ndege ya kumpeleka Tundu Lissu Nairobi akiwa mahututi. Hii Tundu Lissu amesema ameambiwa na familia ya marehemu.

SITA: Mtoto wa Dada yake Magufuli, Doto James, ambae kwa sasa ndie ana saini miamala yote ya serikali, alirushwa vyeo ghafla kutoka kuwa afisa TANROADS mpaka katibu mkuu HAZINA pindi mjomba wake alipopata Urais; Na kwamba, sasa hivi kuna watu wawili tu nchi hii, Doto James na mjomba wake, ambao wanajua hela za kununua ndege na za Bwawa la Rufiji ni shiing ngapi na zimetoka wapi.

SABA: Familia ya Mwinyi, Mkapa kila mmoja anamiliki ekari 60,000, Sumaye 45,000 za ardhi ambazo awali zilikuwa mashamba ya serikali, ikiwemo NAFCO, kabla ya kujimilikisha wakiwa marais na wa mawaziri wakuu. Viongozi wengine na matajiri wenye ekari chini ya hapo, elfu 35, elfu 20, elfu 15, elfu 10, elfu 5 ni wengi, wengi, wengi mno. Ambao walipeana kama "wawekezaji" lakini wamezikalia tu. Na ni sababu moja kubwa na migogoro ya wakulima na wafugaji, kupungua kwa ardhi.

NANE: Miaka saba baada ya kuwa tushapata uhuru, Nyerere aliandika kitabu kuelekezea kwamba bado tunahitaji uhuru licha ya kuwa tulishawaondoa wakoloni, kinaitwa Uhuru na Maendeleo. Hoja kuu ya kitabu cha Nyerere inasema jamii inapimwa kwa maendeleo ya watu, sio ya vitu na miundombinu.

TISA: Mkandarasi wa Uwanja wa Ndege Chato, Mayanga Construction (Steven Makigo), ni mme mwenza wa Magufuli, wameoa nyumba moja. Mme mwenza aliambiwa jenga uwanja! Mpwa (Doto James) akaambiwa toa hela!

KUMI: Kiwanja kimoja tu cha ndege kimejengwa na Mkoloni, Mwingereza, kile cha Air Wing, Ukonga. Nyerere alijenga Kilimanjaro na wakaendelea kujenga vingine vyote nchini, Magufuli si Mtanzania wa kwanza kujenga uwanja wa ndege.

-----------------------------------------------------------

WHAT'S THE POINT?
Anasema, wakati wote huu inajengwa hiyo miradi toka uhuru, airports, mbuga, reli, mabwawa ya umeme, mabarabara, hakuna Mtanzania aliyenyanyapaliwa, aliyeuawa kwa pressure ya kutishwa, kuhamishwa, kubambikwa kodi, kupigwa, kutiwa kizuizini miaka 5, au kumiminiwa risasi kwa kuhoji miradi au kwa kigezo kwamba nawaletea maendeleo.
 
Huu ni ukweli mchungu..Katika hoja hizi Mgombea wa Chama tawala lazma ajibu point moja baada ya nyingine na hii ndyo mana ya siasa. Haya sio matusi kisiasa unahitaji kujibu kublok hoja ya m pinzani wako..Vijana wa Chama fulani jitokezeni kujibu hoja hizi!!vingnevo mtajikuta mnaanza kudai eti ni matusi hili neno" matusi limegeuka mbinu ya kukwepa kumjibu "Machine Lissu "!!!
 
Huu ni ukweli mchungu..Katika hoja hizi Mgombea wa Chama tawala lazma ajibu point moja baada ya nyingine na hii ndyo mana ya siasa. Haya sio matusi kisiasa unahitaji kujibu kublok hoja ya m pinzani wako..Vijana wa Chama fulani jitokezeni kujibu hoja hizi!!vingnevo mtajikuta mnaanza kudai eti ni matusi hili neno" matusi limegeuka mbinu ya kukwepa kumjibu "Machine Lissu "!!!

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
Mikutano ya kampeni Sio sehemu ya maswali Ni sehemu ya kunadi sera na kuomba kura sehemu ya maswali na majibu Ni bungeni alikokuwa huko angeuliza maswali yote apewe majibu na serikali hakuuliza anakuja kuuliza Nani kwenye mikutano ya kampeni

Mkutano wa kampeni Hakuna Spika Wala waziri anapotezea muda watu tu

Anadi sera zake aombe kura . Aondoke aende Kwingine
 
Mikutano ya kampeni Sio sehemu ya maswali Ni sehemu ya kunadi sera na kuomba kura sehemu ya maswali na majibu Ni bungeni alikokuwa huko angeuliza maswali yote apewe majibu na serikali hakuuliza anakuja kuuliza Nani kwenye mikutano ya kampeni

Mkutano wa kampeni Hakuna Spika Wala waziri anapotezea muda watu tu

Anadi sera zake aombe kura . Aondoke aende Kwingine
Usituamulie cha kuongea.
 
Kwa hiyo hayo mambo kumi aliyoongea ndio mnahitaji wanayohitaji watanzania akichaguliwa kuwa Raisi?

Na hizo ndizo sera za Chadema aalizowaambia Wana Mbarali?
Zote naona porojo tu hamna sera hata Moja Happ kawapotezea muda tu watu wa mbalali
Kazi kubwa hapa
1:kutengeneza wananchi waliorubuniwa kwa mda mrefu sana toka miaka ya 60 kuwa Chama kimoja tu kimetumia ujinga wao wananchi kuendelea kukaa madarakan...hivo kubadil akili zao!
2:kumwambia mwananch kuwa huyu anaekupenda au anaedai amekupenda kwa mda mrefu mbona vitendo vyake havireflect ukweli?mfn.yeye ndg zake 4 ama 5 ama zaidi wamejaa ofs moja halaf wewe hapa kijjn watoto wako wamekosa ajira na wamesoma.
3:kuwambia wananchi kuwa kinachobiriwa na mtawala kuwa amefanya hata wengine walifanya?kwanini atake sifa tu yeye?
4:nk nk

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom