Uchaguzi 2020 Mambo Kumi niliyoyasikia leo kwa mara ya kwanza kuhusu Tanzania kutoka kwa Tundu Lissu akiwa Mbarali

Taso

JF-Expert Member
Jun 12, 2010
2,121
2,000
MOJA: Reli nyingine zilizopo na zenyewe ni standard gauge - TAZARA, RELI YA KATI, (DAR -KIGOMA) na ya TANGA-ARUSHA

MBILI: Marais wengine wote na wenyewe walianzisha mabwawa ya umeme, kuanzia Kidatu na Mtera (Nyerere), wengine wakajenga Kihansi (Morogoro - MKAPA), Hale (Tanga - NYERERE), Pangani (Tanga - MWINYI), Nyumba ya Mungu (Kilimanjaro - NYERERE), Rusumo (Kagera- KIKWETE), Songwe (Mbeya - KIKWETE)

TATU: Wakati wa uhuru kulikuwa na mbuga moja tu, ya Serengeti, iliyotengwa na Mkoloni. Nyingine zote zilianzishwa kwa amri za marais kwa kuhamisha watu, hizi za Magufuli wanahamisha wanyama, wanawapeleka Chato ambako naturally hakuna mbuga, hakuna wanyama. Na wanapounda mbuga mpya wanaingilia maeneo ya watu na hawawalipi fidia, wanasababisha maafa na migogoro ya ardhi. Anaijua migogoro yote ya mipaka ya hifadhi nchi hii, na ardhi za wananchi zilizopokwa bila fidia, kwa sababu alilifanyia utafiti katika kazi yake ya kwanza akitoka chuo.


NNE: Daktari muanzilishi wa Hospitali ya Masana Mbezi, Dar es Salaam, alikufa kwa pressure baada ya kukutwa na mashine alizonunua kwenye mnada wa vifaa chakavu, Muhimbili, akasahau kufuta zile alama za MUHIMBILI MKWAJU SERIKALI MKWAJU HOSP MKWAJU RUFAA MKWAJU SIFURI SIFURI MBILI MKWAJU.... Alifunguliwa kesi ya uhujumu uchumi isiyo na dhamana, akafa na pressure halafu wakakuta ni kweli alinunua Muhimbili.

TANO: Mbunge wa CCM, Salim Hassan Abdullah Turki, amekufa na pressure baada ya kubambikwa madai ya kodi ya mabilioni. Mheshimiwa Turki ndie aliyekodi ndege ya kumpeleka Tundu Lissu Nairobi akiwa mahututi. Hii Tundu Lissu amesema ameambiwa na familia ya marehemu.

SITA: Mtoto wa Dada yake Magufuli, Doto James, ambae kwa sasa ndie ana saini miamala yote ya serikali, alirushwa vyeo ghafla kutoka kuwa afisa TANROADS mpaka katibu mkuu HAZINA pindi mjomba wake alipopata Urais; Na kwamba, sasa hivi kuna watu wawili tu nchi hii, Doto James na mjomba wake, ambao wanajua hela za kununua ndege na za Bwawa la Rufiji ni shiing ngapi na zimetoka wapi.

SABA: Familia ya Mwinyi, Mkapa kila mmoja anamiliki ekari 60,000, Sumaye 45,000 za ardhi ambazo awali zilikuwa mashamba ya serikali, ikiwemo NAFCO, kabla ya kujimilikisha wakiwa marais na wa mawaziri wakuu. Viongozi wengine na matajiri wenye ekari chini ya hapo, elfu 35, elfu 20, elfu 15, elfu 10, elfu 5 ni wengi, wengi, wengi mno. Ambao walipeana kama "wawekezaji" lakini wamezikalia tu. Na ni sababu moja kubwa na migogoro ya wakulima na wafugaji, kupungua kwa ardhi.

NANE: Miaka saba baada ya kuwa tushapata uhuru, Nyerere aliandika kitabu kuelekezea kwamba bado tunahitaji uhuru licha ya kuwa tulishawaondoa wakoloni, kinaitwa Uhuru na Maendeleo. Hoja kuu ya kitabu cha Nyerere inasema jamii inapimwa kwa maendeleo ya watu, sio ya vitu na miundombinu.

TISA: Mkandarasi wa Uwanja wa Ndege Chato, Mayanga Construction (Steven Makigo), ni mme mwenza wa Magufuli, wameoa nyumba moja. Mme mwenza aliambiwa jenga uwanja! Mpwa (Doto James) akaambiwa toa hela!

KUMI: Kiwanja kimoja tu cha ndege kimejengwa na Mkoloni, Mwingereza, kile cha Air Wing, Ukonga. Nyerere alijenga Kilimanjaro na wakaendelea kujenga vingine vyote nchini, Magufuli si Mtanzania wa kwanza kujenga uwanja wa ndege.

-----------------------------------------------------------

WHAT'S THE POINT?
Anasema, wakati wote huu inajengwa hiyo miradi toka uhuru, airports, mbuga, reli, mabwawa ya umeme, mabarabara, hakuna Mtanzania aliyenyanyapaliwa, aliyeuawa kwa pressure ya kutishwa, kuhamishwa, kubambikwa kodi, kupigwa, kutiwa kizuizini miaka 5, au kumiminiwa risasi kwa kuhoji miradi au kwa kigezo kwamba nawaletea maendeleo.
 

ostrichegg

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
9,325
2,000
Mikutano ya kampeni Sio sehemu ya maswali Ni sehemu ya kunadi sera na kuomba kura sehemu ya maswali na majibu Ni bungeni alikokuwa huko angeuliza maswali yote apewe majibu na serikali hakuuliza anakuja kuuliza Nani kwenye mikutano ya kampeni

Mkutano wa kampeni Hakuna Spika Wala waziri anapotezea muda watu tu

Anadi sera zake aombe kura . Aondoke aende Kwingine
Hivi kweli yatoka moyoni mwako hayo?
Bunge lipi? La Ndugai?
Bunge la ndiyoooo, kushangilia na kupongeza Jiwe akipokea zamu ya kushika kijiti.
Bunge la kuandaliwa hotuba ya Upinzani?
 

ostrichegg

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
9,325
2,000
Kazi kubwa hapa
1:kutengeneza wananchi waliorubuniwa kwa mda mrefu sana toka miaka ya 60 kuwa Chama kimoja tu kimetumia ujinga wao wananchi kuendelea kukaa madarakan...hivo kubadil akili zao!
2:kumwambia mwananch kuwa huyu anaekupenda au anaedai amekupenda kwa mda mrefu mbona vitendo vyake havireflect ukweli?mfn.yeye ndg zake 4 ama 5 ama zaidi wamejaa ofs moja halaf wewe hapa kijjn watoto wako wamekosa ajira na wamesoma.
3:kuwambia wananchi kuwa kinachobiriwa na mtawala kuwa amefanya hata wengine walifanya?kwanini atake sifa tu yeye?
4:nk nk

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
Ujobile AMEN
 

Distinction

JF-Expert Member
Sep 20, 2014
638
500
Yanawahusu Nini watu wa Mbalali alipokuwa akihutubia? Kaanza kugeuza mikutano ya kampeni vijiwe vya story
Yajayo yanafurahisha.. hawajui watanzania tunataka maendeleo sio taarab na mipasho..
Rais Magufuli kafanya mengi sana wenye akili timamu ndio watakaoelewa tu...
 

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
2,790
2,000
Kwa hiyo hayo mambo kumi aliyoongea ndio mnahitaji wanayohitaji watanzania akichaguliwa kuwa Raisi?

Na hizo ndizo sera za Chadema aalizowaambia Wana Mbarali?
Zote naona porojo tu hamna sera hata Moja Hapo kawapotezea muda tu watu wa mbalali
Kwani magufuli Jana aliyosema atampa kazi tibaijuka ndio sera ya ccm? Hizo mambo zinakuwepo tu kwenye kampen acha kujitoa akili ya kutaka kutuaminisha kuwa kila kitu anacho ongea mgombea ndio sera yake
 

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
2,790
2,000
Yajayo yanafurahisha.. hawajui watanzania tunataka maendeleo sio taarab na mipasho..
Rais Magufuli kafanya mengi sana wenye akili timamu ndio watakaoelewa tu...
Kila Rais kafanya mengi sana, tatizo la awamu hii mmekuwa na hofu Sana, kiasi kwamba hata ukila kuku nyumbani kwako unaona kama ni hisani ya Rais
 

NAWATAFUNA

JF-Expert Member
Nov 14, 2019
4,987
2,000
Nyie kizazi cha nyoka....
Na bado!! Mtachanganyikiwa sana mwaka huu

Kwani hakuongea Sera za Chama chake ??? Kubadirisha mfumo wa utawala ni nini??? Kuifanya nyanda za juu kusini kuwa kanda maalumu ya uzalishaji wa kilimo na biashara za kilimo kwa nchi za kusini mwa Africa nini???

Kutoa Bima ya Afya kwa watu wote ni nini???? Kuwafidia wote waliohamishwa kuongeza mbuga ya ruaha ni nini????

Kwa kifupi CCM mmechanganyikiwa na hamna cha kumjibu Tundu Antiphas Lissu mnaishia kuchanganyikiwa na kutoa propaganda uchwara
"Kufanya nyanda za juu kusini kuwa kituo cha kilimo cha biashara kusini mwa nchi za Africa"uwezo wa Lissu umeishia hapa.
hawezi,hawezi,hawezi kudadavua ataweka mfumo upi au mazingira yepi,pesa zitatoka mfuko upi,atawawezesha vipi wakulima,pembejeo,soko ili kufanikisha hili.
hawezi,hana icho kipaji.wakina Lipumba ni wabobezi wabobezi wa kuchanganua lakini kusema na kutenda nintofauti.
 

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
2,790
2,000
Mikutano ya kampeni Sio sehemu ya maswali Ni sehemu ya kunadi sera na kuomba kura sehemu ya maswali na majibu Ni bungeni alikokuwa huko angeuliza maswali yote apewe majibu na serikali hakuuliza anakuja kuuliza Nani kwenye mikutano ya kampeni

Mkutano wa kampeni Hakuna Spika Wala waziri anapotezea muda watu tu

Anadi sera zake aombe kura . Aondoke aende Kwingine
Ingekuwa ni hivyo kusingekuwa Fiesta kwa baadhi ya mikutano ya kampen
 

Parvovirus

Senior Member
May 24, 2020
192
250
standard-gauge railway is a railway with a track gauge of 1,435 mm. The standard gauge is also called Stephenson gauge after George Stephenson, International gauge, UIC gauge, uniform gauge, normal gauge and European gauge in Europe.

Jihadharini sn na story za vijiwe vya lumumba nyie misukuke
We k kweli ndo umejibu nn hapo sasa.. mleta mada kasema lisu alisema tazara nayo ni sgr... Tazara ni 1067mm thats mean sio sgr... Mimi nimeuliza.
Acha mnduku mnduku msukule ni waliokuzaa
 

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
2,790
2,000
"Kufanya nyanda za juu kusini kuwa kituo cha kilimo cha biashara kusini mwa nchi za Africa"uwezo wa Lissu umeishia hapa.
hawezi,hawezi,hawezi kudadavua ataweka mfumo upi au mazingira yepi,pesa zitatoka mfuko upi,atawawezesha vipi wakulima,pembejeo,soko ili kufanikisha hili.
hawezi,hana icho kipaji.wakina Lipumba ni wabobezi wabobezi wa kuchanganua lakini kusema na kutenda nintofauti.
Kumbe Hiko ni kipaji
Sasa si ndio maana Kuna wataalam?
Kwani kahawa na korosho zimekuwaje? Mwenye kipaji amefanya nn?
 

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
2,790
2,000
Kama ni utaalam mbona kashindwa hata kusema atatumia wataalam,anabaki anabwabwaja?
Hahaha ndio maana una akili na umeenda shule, mambo mengine unajiongeza tu

Kwani ww ujui kuwa Rais anakuwa na team ya washauri?

Au nyie ndio wale mnadhan hata Rais hasikii njaa wala hachoki
 

This is...

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
1,235
2,000
Kwa hiyo hayo mambo kumi aliyoongea ndio mnahitaji wanayohitaji watanzania akichaguliwa kuwa Raisi?

Na hizo ndizo sera za Chadema aalizowaambia Wana Mbarali?
Zote naona porojo tu hamna sera hata Moja Hapo kawapotezea muda tu watu wa mbalali
Dada yangu,Hujawahi kuwa na hoja ya maana.Wenye akili wamemwelewa Lissu.Ukisoma tu hilo hitimisho unaelewa lengo la hizo hoja.
 

Distinction

JF-Expert Member
Sep 20, 2014
638
500
Kila Rais kafanya mengi sana, tatizo la awamu hii mmekuwa na hofu Sana, kiasi kwamba hata ukila kuku nyumbani kwako unaona kama ni hisani ya Rais
Hawafanyi wao, ni kwa niaba ya watanzania wote na kodi zetu na mali asili zetu na utekelezaji wa matakwa ya watanzania, kikubwa hapa ni usimamizi na uzalendo tu. Nchi hii ilikua inaelekea kubaya mkuu tuweke unafiki pembeni, Mzee Magu kajitahidi sana.
Yeye si malaika .....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom