Mambo kumi niliyoyaona mechi ya Yanga vs Polisi

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
1: WHAT A MATCH Kimbinu, Kiufundi, wachezaji na makocha walijitahidi sana kuthamini viingilio vya mashabiki. Mechi ilikuwa ya wazi na Timu imepata matokeo

2: Mwanzo mzuri Cedric Kaze Kuna mabadiliko ya kiuchezaji yameonekana. Alianza na mfumo wa 4-2-3-1 kabla ya baadae kuswitch kwenda kwenye 4-1-2-3. 'Build up' ilikuwa nzuri kutokea chini, changamoto pekee ni kwenye utengenezaji wa nafasi kwenye eneo la mwisho

3: Malale Hamsini alipata tabu dakika 30 za kwanza, Yanga walipoamua kukaba 'zone'. Wakalazimishwa kupiga mipira mirefu. Kipindi cha pili, wakaja na 'plan' nzuri ya kuvunja mistari ya ulinzi ya Yanga kwa kukokota mpira. Kama safu ya Ushambuliaji ya Polisi ingekuwa makini kiasi, wangeweza kupata bao

4: Feisal Salum 'FeiToto' ndio roho ya syteam mpya ya 'Kaze'. Movement zake kwenye kuattack box la wapinzani ilikuwa Fantastic sana. Nimependa pia alivyokuwa anachuka chini na kuanzisha mashambulizi

5: Kama kuna kitu cha kwanza Kaze anatakiwa kukifanyia kazi ni kutengeneza chemistry kati ya viungo na washambuliaji wake. Timu inamiliki mpira lakini inapata kigugumizi kwenye pasi ya mwisho ya maamuzi

6: Ukuta wa Lamine na Mwamnyeto una majibu mengi kwanini Yanga imeruhusu bao 1 mpaka sasa. Achana na ukabaji wao, rudi angalia akili yao kwenye kupiga pasi nzuri kutokea chini. Viungo wa Yanga wanarelax sana kucheza mbele ya ukuta huu

7: Yassin Mustafa WoW si mabeki wote wa pembeni wanaweza kushinda vita ya Rashid Juma. Yassin amelimudu hili katika ubora mkubwa. Alikaba vyema hatua za Rashid na kusukuma timu mbele kwa 'Spirit' kubwa sana

8: Nassoro Maulidi..Yule rasta wa Polisi katikati ya kiwanja Jamaa yuko Tough sana. Kama akiboresha 'dribling' yake anaweza kuwa kiungo bora sana nchini

9: Farid Mussa bado kidogo. Anahitaji muda wa kujiamini zaidi akiwa na mpira na maamuzi yake. Aina yake ya uchezaji akiwa kwenye ubora wako, ni kitu Yanga wanachokihitaji msimu huu

10: Nimefurahishwa sana na umakini wa mabeki wa kati wa Polisi. Yule Mohammed Kassim yuko fiti mno. Ana kasi, nguvu na timing nzuri ya kunusa hatari

Nb: Kuna Kikosi Kipana halafu kuna KIKUNDI CHA WACHEZAJI
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom