Mambo kumi kwanini idadi kubwa ya kada ya vijana wanaichukia ccm.....

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
Watanzania wanasababu nyingi za kuichukia CCM na hizi ndio sababu ya msingi kwanini CCM haikubaliki kwa watanzania hasa kada ya vijana...
  1. Ni chama kisichoumia na matatizo ya watanzania hasa umaskini wao....hakuna jitihada za wazi kuwasaidia watanzania zaidi ya kupewa sababu kuwa ni wazungu na matatizo yao..
  2. Ni chama kilichokosa muelekeo na kutumia hoja nyepesi kama udini,ukabila kuua vyama vingine walifanikiwa kwa CUF miaka ya 2000 mwanzoni na sasa wanataka kufanya hivyo kwa CDM...
  3. Ni chama kilichokubali kuwabeba wahuaji wa kimya kimya wa watanzania...hawana uwezo wa kukemea uovu wa viongozi wake...
  4. Ni chama kilichoruhusu familia saba tu zitutawale...ya EL,RA,AC,JK,YM nk..ndio wachague nani awe waziri na kwanini..
  5. Ni chama kisichoangalia utu na ubinadamu wa mtanzania...kipo radhi kuwaamisha watanzania 1000 kwenye ardhi moja kwa nguvu ili apewe kigogo mmoja mfano Dodoma kijiji cha Njedengwa wakazi zaidi ya 1000 walivunjiwa nyumba na kupewa mtu mmoja kwa kivuli cha Aggrey Mwanri waziri....mpaka leo watanzania hawa hawajui pa kwenda...
  6. Ni chama kinachoongoza kwa kuuza maliasili zetu nje ya nchi..wanyama,madini nk kwa mrahaba wa asilimia 3...tena bila aibu....
  7. Ni chama kinachowabeba viongozi waovu hata kama makosa na upuuzi wao upo wazi...tazama ya masharobaro wawili Ngeleja na Malima...kazi yao ni kuweka wave kwenye nywele bila kufanya kazi...
  8. Ni chama kilichoruhusu mpasuko wa wazi ambao unaathiri maisha ya watanzania bila kuchukua hatua..tazama ya kujivua gamba na mengineyo...
  9. Ni chama kilichijaza viongozi wasio wazalendo kwao maslahi yao kwanza,then chama halafu taifa baadae...ni chama kilichojaza wahuni na vilaza mfano Livngstone Lusinde..huyu sio kiongozi ila ni vuvuzela tu...
  10. Ni chama pekee kinachoongoza kuwa na kauli mbiu za kutosha...Maisha bora kwa kila mtanzania, Ari mpya,nguvu mpya na kasi mpya, Mapinduzi ya kijani, Kilimo kwanza, Elimu kwanza by EL, na Hii kali ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika..Tumethubutu,tumeweza na tunasonga mbele.....
Haya ni kwa uchache..itaendelea....
 
sasa kama ccm kiko hivyo ushauri wako kwa sisi vijana twende chama gani?Nalog off
 
Back
Top Bottom